MISAADA MBALIMBALI YA KIJAMII YATOLEWA SHAREHOPE MINISTRIES ILIPOTEMBELEA KITUO CHA AFYA MLALI

Misaada mbalimbali ya kijamii yatolewa kwa wagonjwa waliolazwa wakati ShareHope Ministries walipotembelea Kituo Cha Afya Mlali. Wakitoa shukrani kwa niaba ya uongozi wa kituo, Wauguzi wa zamu walishukuru sana kwa huduma iliyofanywa na kusisitiza wadau wengine wajikite katika kutoa huduma za kuwafariji wagonjwa.

Karibu Kituo Cha Afya Mlali

Karibu Kituo Cha Afya Mlali

Mzee Kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya alitoa maelekezo ya namna ambavyo huduma zitakavyotolewa.

Mzee Kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya Ndg. Benatus Muyenjwa akitoa maelekezo ya namna ambavyo huduma zitakavyotolewa.

Jengo la Kituo cha Afya Mlali kwa mbali

Jengo la Kituo cha Afya Mlali kwa mbali

Mlango wa kuingia katika wodi ya watoto kwenye kituo cha Afya Mlali.

Mlango wa kuingia katika wodi ya watoto kwenye kituo cha Afya Mlali.

Mhazini wa ShareHope Ministries Ms. Rebecca Mchome akikabidhi baadhi ya mahitaji kwa mama mlezi wa mtoto kwa niaba ya ShareHope Ministries kama pole na faraja kwa mgonjwa na wauguzaji.

Mhazini wa ShareHope Ministries Ms. Rebecca Mchome akikabidhi baadhi ya mahitaji kwa mama mlezi wa mtoto kwa niaba ya ShareHope Ministries kama pole na faraja kwa mgonjwa na wauguzaji.

Ndg. Werema Rwabuhanga (katikati) akitoa Neno fupi la faraja kwa mgonjwa. Kulia ni Mzee kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya Ndg. Benatus Muyenjwa.

Ndg. Werema Rwabuhanga (katikati) akitoa Neno fupi la faraja na ombi kwa mgonjwa. Kulia ni Mzee kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya Ndg. Benatus Muyenjwa.

Baadhi ya Viongozi wa ShareHope Ministries baada ya kutembelea wagonjwa, kuanzia kulia ni Mkurugenzi wa Uinjilisti na Mikutano ya Injili Ndg. Musa Daudi Mwakisya; Mhazini Ms. Rebecca Mchome; Mkurugenzi wa Mawasiliano Ndg. Mujaya Mujaya na Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani Ndg. John Mafuru.

Baadhi ya Viongozi wa ShareHope Ministries baada ya kutembelea wagonjwa, kuanzia kulia ni Mkurugenzi wa Uinjilisti na Mikutano ya Injili Ndg. Musa Daudi Mwakisya; Mhazini Ms. Rebecca Mchome; Mkurugenzi wa Mawasiliano Ndg. Mujaya Mujaya na Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani Ndg. John Mafuru.

Jengo kuu la Kituo cha Afya Mlali

Jengo kuu la Kituo cha Afya Mlali

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in News

KUNA KANUNI GANI ZA KUISHI MILELE?

EDDIEe

KARIBUNI TENA KATIKA KUYATAFAKARI MAANDIKO YA MUNGU WETU

“INAWEZEKANA KUISHI MILELE”

SOMO LA TATU LINASEMA: Kuna Kanuni Gani Rahisi Za Kuishi Milele?

Fungu Kuu: “Na uzima wa milele ndio huu wa kujue wewe, MUNGU wa pekee wa kweli,

                      na YESU Kristo uliye mtuma” Yohana 17:3

Dr. Edward Mhina

Dr. Edward Mhina

Na. Dkt. Edward Raphael Mhina

Kuna Kanuni Gani Rahisi Za Kuishi Milele?(Download)

Ndugu msomaji katika mambo ambayo wengi wanapotea au kupoteza fursa ya kuishi milele ni kwa kukosa kujua ukweli kutoka ndani ya biblia. Miongoni mwa kweli hizo ni pamoja na kanuni rahisi ambazo MUNGU kwa mkono wake aliziandika na kumpatia mwanadamu ili kwa kumwamini Yesu aishi milele. Ukisoma katika kitabu cha Kutoka 31:18 “Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, ZILIZOANDIKWA KWA CHANDA(KIDOLE) CHA MUNGU”. Hivi tunaona ya kwamba ni za muhimu kiasi gani kuzifuata sababu MUNGU ameziandika kwa mkono wake mwenyewe. Hii ni kuonyesha ya kwamba atuwezi ishi maisha ya amani bila kuzifuata amri hizi katika ulimwengu huu ambao shetani anafanya kila njia, ili tusifanye yale MUNGU anayotuagiza kuya tenda. Kanuni hizi ni nyepesi kuzifuata ikiwa tutajikabidhi kwa Yesu kwamba atusaidie maana biblia inasema si nzito, ukisoma 1 Yohana 5:3, “Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.” Ili mtu azishike kanuni za Mungu kwa ukamilifu wake anahitaji msaada wa Yesu na Roho mtakatifu atukamilishae katika mambo yote, “Nayaweza mambo yote katika Yeye anitiaye nguvu”Jesus and the Law

Paulo katika kitabu cha Warumi 7:12 anasema kanuni hizi ni takatifu na haki tena ni njema : “Basi torati ni takatifu , na ILE AMRI NI TAKATIFU, NA YA HAKI, NA NJEMA”.
Hata ukitazama vitu vyote vinavyo tengenezwa vina vijitabu vinavyo beba maelekezo ya namna ya kuvitumia ili vidumu kwa muda mrefu bila matatizo. Vivyo hivyo kwa mwanadamu ili aweze kuishi maisha yamilele akimpendeza yule aliye muumba hana budi kuishi kulingana na amri kumi za MUNGU kanuni rahisi za upendo za kuishi milele. Kanuni hizo huonesha tabia ya Mungu kwa mwanadamu kuwa ni ya upendo, ukamilifu, utakatifu na njema.

Ukweli ni kwamba kuna amri kumi za MUNGU ambazo ni kanuni za upendo nazo zinapatikana katika kitabu cha kutoka 20:1-17na kimsingi amri hizi zimegawanyika katika makundi mawili kama vile YESU alivyo jibu katika kitabu cha Mathayo22:36-40 pale alipo ulizwa swali
“Mwalimu, katika torati ni amri ipi iliyo kuu? 37 Akawaambia, Mpende Bwana MUNGU wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa akili zako zote.38 Hii ndio amri iliy kuu tena ya kwanza, 39. Nayapili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yakokama nafsi yako .40. Katika amri hizi mbili hutegemea torai yote na manabii”

Ndugu msomaji ukiangalia kwa umakini YESU alikuwa akimaanisha ya kwamba kutoka kanuni/amri ya kwanza mpaka ya nne huonesha mahusiano ya upendo yaliyopo katiya MUNGU na mwanadamu na kuanzia kanuni/amri ya tano mpaka kumi huonesha mahusiano ya upendo kati ya wanadamu. Ukweli ni kwamba tukitaka kumpenda YESU nilazima tuzishike amri zake yeye mwenyewe anasema katika, Yohana 14:15 “Mkinipenda, mtazishika amri zangu.”

Tahadhari ni kwamba twapaswa kuzishika amri zote kama yeye mwenyewe alivyozitoa hatuna mamlaka yakubadili wala kuiacha moja wapo Yakobo 2: 10 anatuambia ya kwamba “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja , amekosa juu ya yote.” Sapphire 10 CommandmentsHakika nakuambia ya kwamba MUNGU amesema kitabu hiki ni kitakatifu kwa sababu amekindika yeye mwenyewe kupitia mitume na manabii kwa njia ya Roho Mtakatifu hivyo si kwa mawazo ya binadamu, hivyo mtu yoyote atakaye jaribu kuondoa hata neno katika kitabu hiki naye ametoa onyo katika kitabu cha Ufunuo 22:18-19 “Namshudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu yeyote akiyaongeza,MUNGU atamuongezea hayo mapigo yaliyo andikwa katika kitabu hiki,19 Na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya unabii wakitabu hiki,MUNGU atamuondolea sehemu yake katika ule mti wa uzima , na katika ule mji matakatifu, ambao habari zake zimeandikwa katika kitabu hiki”

Napendekeza kwako ya kwamba tuifuate ile amri ambayo MUNGU wetu wa mbinguni kwa mkono wake alituandikia na wala si zile ziliowekwa na wanadamu maana hii ndiyo jumla itupasayo ili tuwe katika maisha ya uzima kwa kumwamini Yesu mwenye kuanzisha na kuhitimisha imani yetu. Mhubiri 12:13, “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe UZISHIKE AMRI ZAKE, MAANA KWA JUMLA NDIYO IMPASAYO MTU.”

Yapo mafungu mengi katika biblia yanayothibisha haya yote tuliyo yasoma. “USIDANGANYIKE.” Ninakualika kuuliza swali lolote linalo kutatiza uli upate majibu yaliyo sahihi kupitia kitabu cha MUNGU yani BIBLIA.

Sali nami sala hii tunapo hitimisha somo hili:

MUNGU unayetupenda sana na unayetamani tuishi kulingana na amri zako kanuni rahisi za kuishi milele na takatifu, fungua akili zetu ili tukupende wewe BWANA na kwa kufanya hivyo tukizishika amri zako kwa kuwezeshwa na Yesu pamoja na Roho wako Mtakatifu, nisaidie nisikose kujifunza neno lako tena, nimeomba kwa jina la YESU KRISTO amen!

KARIBUNI TENA TUTAENDELEA KUTAFAKARI NENO LA MUNGU WETU.

SOMO LINALOFUATA: Je, Ninawezaje Kupata Pumziko la Milele?

Maswali, Maoni au Ushauri wasiliana nami: +255652648737 au +255768678122

Inawezekanaje Kuishi Milele Wakati Kuna Kifo? Je, Wafu Wapo Wapi?

tuinf

Fungu Kuu: “Na uzima wa milele ndio huu wa kujue wewe, MUNGU wa pekee wa kweli,

                          na YESU Kristo uliye mtuma” Yohana 17:3

Dr. Edward Mhina

 

 

 

 

Na. Dkt. Edward Raphael Mhina

Downloadable Version: Inawezekanaje Kuishi Milele Wakati Kuna Kifo? Je, Wafu Wapo Wapi?

Natumaini msomaji wangu ni mzima kwa jina la mungu wetu aliye hai. Katika mambo ambayo yanawasumbua watu katika maisha ya sasa ni pamoja na habari ya kuwa mtu akifa anakwenda wapi. Wengine husema mtu akifa anakwenda akhera, wengine husema anakwenda kuzimu, wengine anaenda pagatori, wengine husema anaenda peponi na wengine husema anakwenda kuonana na kuishi na wazee au mababu zetu wa kale. Pia yametokea mafundisho mengi ya uongo yenye kupotosha na kuwafanya wanadamu kuamini katika kile ambacho MUNGU kamwe hajakisema kupitia maandiko yake matakatifu. Leo tutatazama pamoja ukweli wa mambo yote katika biblia ili tuepukane na mkanganyiko huu. Death

Kwanza kuna utofauti mkubwa kati ya nafsi kwa jinsi ilivyo tafsiriwa katika biblia ya Kiswahili kwa maana ya (soul) na roho kwa maana ya (spirit), kinacho mtoka mtu ni roho nayo umrudia MUNGU aliye itoa ukisoma katika Mhubiri 12:7, “Nayo mavumbi kuirudia nchi kama yalivyo kuwa, Nayo roho kumrudia MUNGU aliye itoa” ukitazama kwa undani roho ni pumzi ambayo MUNGU alimpulizia mwanadamu puani wakati alipomuumba katika Mwanzo 2:7 “Bwana MUNGU akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia PUANI PUMZI YA UHAI; mtu akawa nafsi hai”. Hivyo mtu anapokufa mavumbi hurudia ardhi yalipotolewa na roho au ile pumzi ya Mungu ya humrudia Mungu aliyeitoa. Roho ni hewa au upepo, ukisoma katika maandiko, Ayubu 27:3, “(Kwa kuwa uhai wangu ukali mzima ndani yangu, NA ROHO YA MUNGU I KATIKA PUA YANGU;)

Kwa maana hiyo tunaona kwamba roho umrudia MUNGU yeye aliye itoa. Je, mtu akifa anakumbuka? La! Hasha mtu akifa kumbukumbu hotoweka soma katika, Zaburi 146:4 “ PUMZI YAKE HUTOKA, huurudia udongo wake, SIKU HIYO MAWAZO YAKE HUPOTEA”. Kwa maana hiyo mtu akifa hajui neno lolote soma katika Mhubiri 9:5, “Kwa sababu walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini WAFU HAWAJUI NENO LOLOTE, wala hawana ijara tena, maana kumbukumbu lao limesahauliwa.”

Je? Wafu hufanya ibada kwa MUNGU ? La! Hasha hawawezi sababu hawajui lolote soma katika Zabiri 115:6, “zina vinywa lakini hazisemi, zina pua lakini hazisikii harufu” ukisoma pia Zaburi 6:5 inasema “ Maana mautini hapana kumbukumbu lako; KATIKA KUZIMU NI NANI ATAKAYEKUSHUKURU?” hii huthibitisha ya kwamba mtu mfu hawezi fanya jambo lolote lile, hawezi hata kufanya maombi, kuimba, kusifu au kushukuru. Kwa kweli si kwamba MUNGU hataki tujue habari za wafu hapana, yeye mwenyewe kupitia maandiko matakatifu ametuhabarisha. 1 Thesalonike 4:13 “Lakini, ndugu, HATUTAKI MSIJUE HABARI ZAO WALIOLALA MAUTI, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.”

Death 2Ndugu msomaji bila YESU hakuna tumaini jingine lolote pale utakapolala mauti, maana utasahau yote na utaacha yote ujivuniayo kwa sasa wakati ungali hai. Napendekeza kwako kutoa maisha yako kwa MUNGU aliye hai kwa kumwamini Yesu kama Bwana na mwokozi wako binafsi maana yeye ni ufufuo na uzima. Yohana 11:25, “Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi”. Hata ukilala mauti utakuwa unaishi maana wanaokufa katika Yesu huwa katika usingizi wa mauti tu, wanalala kwa muda kitambo kifupi kupumzika katika tumaini kuu la ufufuo siku Yesu atakapokuja kuwafufua na kuwapatia mwili mpya na kuishi naye mbinguni. Ukisoma 1Wathesalonike 4:14 inasema “Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye.”

Kamwe usidanganyike na mawazo ya watu Yesu ameyajibu ya maswali yako kati biblia. Napendekeza kwako huu uwe muongozo wa maisha yako tangu leo.

Sali nami tunapohitimisha somo hili:

MUNGU Mtakatifu uishie mbinguni nashukuru kwa ukweli huu nakuomba unisamehe dhambi zangu na unifanye niwe mtoto wako. BWANA nisaidie nitembee katika nuru yako, ili hata nilalapo mauti niwe katika tumaini la kuishi milele siku utakapokuja kuwafufua watu wote watakaolala mauti kwa nguvu na utukufu, niasaidie kuanzia leo kuyachunguza maandiko yako na unipatie fursa ya kusoma tena neno lako.

Nimeomba kupitia jina la YESU KRISTO amen!

KARIBU TENA TUENDELEE NA SEMINA ZETU “INAWEZEKANA KUISHI MILELE”

SOMO LINALOFUATA: Kuna Kanuni Gani Rahisi Za Kuishi Milele?

Maswali, Maoni au Ushauri wasiliana nami: +255652648737 au +255768678122

INAWEZEKANAJE KUISHI MILELE KATIKA MAISHA YA SHIDA?

tuinf

NDUGU MSOMAJI NA MFUATILIAJI KARIBU KATIKA SEMINA ZETU ZA PEKEE SANA ZA NENO LA MUNGU “INAWEZEKANA KUISHI MILELE”

SOMO LA KWANZA LINASEMA:

Inawezekanaje Kuishi Milele Katika Maisha ya Shida?

Fungu Kuu: “Na uzima wa milele ndio huu wa kujue wewe, MUNGU wa pekee wa kweli,

                          na YESU Kristo uliye mtuma” Yohana 17:3

Dr. Edward Mhina

 

 

 

 

 

Na. Dkt. Edward Raphael Mhina

Downloadable Version: Inawezekanaje Kuishi Milele Katika Maisha ya Shida?

Nianze kwa kusema ya kwamba “nampenda sana MUNGU” kwa sababu alituumba wakamilifu sana. Ukitazama dunia jinsi alivyo iumba hakika ni ya pekee sana japo imeharibika bado lakini bado inaonekana yenye mvuto. Kwa mfano ukitazama mmea wa waridi, japo una miba mikali lakini bado limebeba ua zuri lenye harufu nzuri sana la waridi.

Napiga picha jinsi ilivyo kuwa hapo mwanzo kwa kweli najua kwa hakika ya kwamba ilikuwa nzuri na ya kupendeza sana, kwa uthibitisho huu tafakari nami kutoka katika Mwanzo 1:31,
“Mungu akaona KILA KITU alichokifanya, na tazama, NI CHEMA SANA. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita.” Hakukuwa na shida zozote katika dunia wakati MUNGU mwenyezi alipoiumba na alikusudia kwamba maisha ya mwanadamu yawe ya furaha, amani na mafanikio siku zote. Yeremia 29:1, “Maana nayajua MAWAZO NINAYOWAWAZIA NINYI, asema Bwana, NI MAWAZO YA AMANI WALA SI YA MABAYA…” Hakika nakuandikia yakuwa MUNGU wetu ni MUNGU mwenye pendo kubwa sana.Inawezekana Kuishi Milele 1

Wazo kuu; sasa kwanini shida ? Shida imeingia kwa kukiuka maagizo tuliyopewa na MUNGU wakati wazazi wetu wa kwanza walipokabidhiwa bustani ya Edeni. Wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa walikula matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya ambalo MUNGU aliwakataza. Ukitafakari nami katika Mwanzo 3inaonesha jinsi ambavyo wazazi wetu wa walishwawishiwa na shetani na kuingia katika shida(dhambi) kwa kukiuka maagizo ya Mungu. Tangu mwanzo MUNGU alikusudia binadamu wawe na akili ya ufahamu wa kutenda mema tu siku zote, lakini uchaguzi wetu umefanya tuwe katika shida hizi na matatizo tuliyo nayo kwa kuchagua kujua mema na mabaya. Ndivyo ilivyo hadi leo, kuna watu wengi sana ambao wanapitia maisha ya shida na utumwa kwa sababu wamekataa kufuata maagizo ya Mungu.

Lakini napenda kukuhabarisha ya kwamba MUNGU mwenyewe akiwa katika umbile la binadamu(Imanueli: Imanu—Pamoja Nasi na Eli—Mungu, Tazama Mathayo 1:23) alishuka na kufa kwa ajili ya shida hizi tulizo nazo naye aliishinda mauti ili tuwe na uzima wa milele kwa kumwamini. Ukisoma katika Yohana 3:16 “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na UZIMA WA MILELE.”

Hakika kwa habari hiyo tunafanywa huru endapo tutayatoa maisha yetu na kumkabidhi YESU ili ayatawChrist and Lamb - Copyale. Leo Yesu yupo kwa ajili yako na kwa ajili yangu, maana aliyatoa maisha yake, akaacha enzi na utukufu wake mbinguni ili aje afe kwa ajili yako na kwa ajili yangu ili tuishi milele. Anasema na kusihi tena kwa upole, “Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo(SHIDA/DHAMBI), nami nitawapumzisha.” Mathayo 11:28. Kama leo utaisikia sauti ya Bwana itii na uungane nami kumfuata, wala usiufanye moyo wako kuwa mgumu. Kumbuka kupitia kujitoa maisha yetu kwake, anatufanya viumbe vipya, hutuondolea shida zitusumbuazo na kufanya iwezekane kuishi milele maisha ya furaha, amani na mafanikio.

Kama umebarikiwa sali nami sala hii……:

“Nimejua ya kwamba shida zote zinazo nipata ni sababu sijayatoa maisha yangu kwako, rafiki yangu mpendwa na BABA yangu MTAKATIFU MUNGU uishie milele zote, ninakubali nimekutenda dhambi, nisamehe dhambi zangu, nipe moyo wa kujifunza zaidi Neno lako, kwa jina la YESU KRISTO ….. AMEN.”

KARIBU TENA KATIKA SOMO LIJALO LINALO SEMA:

“Inawezekanaje Kuishi Milele Wakati Kuna Kifo? Je, Wafu Wapo Wapi?”

 

Maswali, Maoni au Ushauri wasiliana nami: +255652648737 au +255768678122