Kundi Jipya la Kanisa Laanzishwa!!!! Watu 13 Wabatizwa!!!

Na Mujaya Mujaya

Kundi jipya la Mongwe Kariakoo limeanzishwa baada ya mkutano mkubwa wa injili kufanyika katika kijiji cha Mongwe Kariakoo, mkutano ambao uliendeshwa kwa ushirikiano kati ya Kanisa la Waadventista wa

Muinjilisti Emmanuel Samwel

Muinjilisti Emmanuel Samwel

Sabato Mzumbe na TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe. Mhutubu katika mkutano huo alikuwa muinjilisti Emmanuel Samwel(katika picha kulia) kutoka TUCASA Mzumbe ambaye pia ni mhudumu wa ShareHope Ministries. Mkutano huo uliendeshwa kwa muda wa majuma mawili na kushuhudia watu kumi na tatu(13) wakimkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wao binafsi na kubatizwa kwa maji mengi kama tangazo au uthibitisho wa imani hiyo.

Tangu mwaka 2013 kumekuwa na jitihada za TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe kufungua kazi ya Mungu katika jamii za kutoka safu za milima ya uluguru mkoani Morogoro. Mwaka 2013 kundi la Peko Misegese lilianzishwa ambalo hadi leo linaendelea vizuri kwa kuhudumiwa na muinjilisti mlei ambae anahudumia kundi la Mongwe pia. Washiriki na waumini wote kutoka Peko na Mongwe hukusanyika sehemu moja kila Sabato kwajili ya ibada ya pamoja na kutiana joto la kiroho.

Mwaka 2014 TUCASA Mzumbe walielekeza juhudi zao katika kundi kongwe la kanisa la Mzumbe SDA lililopo Tangeni lakini mwaka huu(2015) jitihada zilipelekwa Mongwe ambalo ni eneo jipya.

Mungu aibariki kazi yake katika safu ya milima ya Uluguru. Tuendelee kuombea maendeleo ya kazi ya Mungu katika nchi ya Tanzania na ulimwengu kwa ujumla.

Muinjilisti Emmanuel Sanwel akitoa hutuba kuu za mkutano ambazo ziligusa sana maisha ya watu wa Mongwe Kariakoo.

Ibada ya kufunga mkutano ilihudhuriwa na watu wengi sana

Kwaya ya TUCASA Mzumbe ikimtukuza Mungu kwa njia ya wimbo ambao uliwaandaa wana mkutano kukutana na Mungu katika Neno la Uzima.

Miss Rebeka Mchome akiendesha kipindi maalumu cha watoto katika mkutano(watoto hao hawakuwa wakiadventista lakini Mungu aliwaongoza kufanya vipindi vya pekee sana kwa utukufu wa jina lake).

Njoo! Njoo! Njoo! Unakawilia nini? Tazama kile ambacho Yesu amekifanya kwa ajili ya maisha yako!!! Njoo leo Njoo sasa usikawie. Wito wa pekee kuwainua wana mkutano wamtazame Yesu na kumfuata.

Wana mkutano wakisimama baada ya kuitikia wito wa kumkabidhi Mungu maisha yao

Waliojitoa kwa ubatizo wakisimama tayari kwa kuapishwa na kungoja zoezi la kihistoria maishani mwao la ubatizo wa maji mengi kama vile Yesu alivyobatizwa

Wabatizwa wakiwa mbele ya umma wa wanamkutano kwajili ya kuthibitishwa na kukili imani yao kwa Yesu kabla ya ubatizo

Mashuhuda wa ubatizo wakiwa pembezoni mwa mto wakati ubatizo ukiendelea

Ubatizo ulifanyika ambapo watu kumi na tatu(13) walitoa maisha yao na kumkili kwa njia ya ubatizo

SAM_3262 SAM_3235

Muinjilisti Basilio Maliwanga akitoa Neno La Uzima kwa waumini wa kundi la Peko na Mongwe katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika kundi la Peko Misegese.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in News

ShareHope Ministries Yafanya Ziara Ya Kimishenari Katika Makundi Mapya Ya Kanisa La Waadventista Wa Sabato Mzumbe Na Mlali Peya Peya

Kufanya kazi ya utume ndiyo moto wa Kanisa jipya la Mlali Peya Peya lililotengwa kutoka Kanisa la Mzumbe. Imekuwa shauku ya makanisa haya kupeleka mbele injili kwa jamii zote zinazowazunguka. Mwezi Aprili mwaka 2015 kanisa la Mzumbe lilifungua kundi jipya la Mongwe Kariakoo baada ya Mkutano wa majuma mawili ulioendeshwa kwa Ushirikiano kati ya TUCASA Mzumbe na Mzumbe SDA. ShareHope Ministries walitembelea kundi hili ili kujionea fursa za injili zilizopo na pia kwa maandalizi ya Mkutano Mkubwa wa Injili katika Kijiji Cha Peko Misegese mwezi Julai 2015.

Washiriki wapya wa Mongwe Kariakoo wakiwa katika nyumba ndogo ya ibada chini ya mti wa mafenesi.

Nyumba ya muda ya ibada ya kundi la Mongwe Kariakoo. Nyumba hii haijakamilika na hivyo huleta usumbufu sana kwa waabuduo hasa wakati wa mvua

Washiriki wa kundi la Mongwe Kariakoo wakijifunza neno la uzima lililotolewa kupitia Ev. Daniel Kitigani

Washiriki wa kundi la Mongwe Kariakoo wakijifunza neno la uzima kwa makini na utulivu wa pekee lililotolewa kupitia Ev. Daniel Kitigani

Ev. Daniel Kitigani akimega mkate wa uzima

Baadhi ya washiriki wa kanisa la Mongwe mara baada ya ibada

Baadhi ya washiriki wa kanisa la Mongwe mara baada ya ibada wakiwa na wageni kutoka ShareHope Ministries

Viongozi wa kundi la Mongwe wakiwa pamoja na wageni kutoka ShareHope Ministries. Kuanzia ni Ev. Mujaya Mujaya; Ndg. Laurent Faustine; Ev. Basilio Maliwanga; Ev. Suleiman Ally; Ev. Daniel Kitigani na Ev. John Mafuru

Kwaya ya muungano kati ya kundi la Peko Misegese na Mongwe Kariakoo ikiimba wimbo wa kumkaribisha Mhudumu mkuu wakati wa ibada

Wanakundi wa Peko Misegese wakiwa katika ibada wakati wa Ziara ya ShareHope Ministries

Mkurugenzi Mkuu wa ShareHope Ministries Ndg. Basilio Maliwanga akihutubia wanakundi wa Peko Misegese wakati ShareHope Ministries ilipotembelea kundi hilo kwa ziara ya kimishenari.

Mkurugenzi Mkuu wa ShareHope Ministries Ndg. Basilio Maliwanga akihutubia wanakundi wa Peko Misegese wakati ShareHope Ministries ilipotembelea kundi hilo kwa ziara ya kimishenari.

By ShareHope Ministries Posted in News

Kikao Cha Mipango Ya Kazi ShareHope Ministries Chafana

ShareHope Ministries hivi juzi walikutana katika Chuo Kikuu Mzumbe kujadili mipango mbalimbali ya kazi ya utume. Maazimio makubwa yalipitishwa ambayo yatachochea mafanikio ya kazi ya Injili.

Mkurugenzi Mkuu wa ShareHope Minisries(kulia) Ev. Basilio Maliwanga akiwa na Katibu Mkuu Ev. Daniel Kitigani wakiendesha kikao cha mipango ya kazi.

Wajumbe wa kikao wakisikiliza kwa makini agenda zikiwakilishwa

Wajumbe wakipiga kura kuamua jambo lililopendekezwa katika kikao

Wajumbe wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa

Wajumbe wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa

By ShareHope Ministries Posted in News

ShareHope Ministries Yakutana Kwa Kikao Cha Uchaguzi

ShareHope wafanya kikao muhimu ambacho kiliweka viongozi wapya kwajili ya kuendeleza kazi ya injili ambapo:-

Muinjilisti: John Mafuru-Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani

Muinjilisti: Peter Jefta-Mkurugenzi wa Huduma kwa jamii

Muinjilisti: Mussa Daudi-Mkurugenzi wa Uinjilisti na Mikutano ya Injili

Muinjilisti: Janet Christopher-Mkurugenzi wa Afya

Muinjilisti: Costantine Masanyiwa-Mkurugenzi wa Mafunzo na Kujenga Uwezo

Sambamba na kikao hicho, ShareHope iliongeza idadi ya wanachama wake na kufikia 18.

Mhazini wa ShareHope Ministries, Ms. Rebecca Mchome (kulia) akisikiliza kwa makini wakati kikao kikiendelea. Pembeni yake ni mwanachama mpya aliyepokelewa Ms. Winnie Makoye

Wanachama wa ShareHope Ministries wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wakati wa kikao hicho makini.

Mkurugenzi wa Mawasiliano Ndg. Mujaya Mujaya akitoa maelezo mafupi kuhusu chimbuko la ShareHope Ministries.

Baadhi ya wahudumu wa ShareHope Ministries baada ya kikao cha ughaguzi