UBATIZO WA KWELI

Ev. Mujaya MujayaNa. Ev. Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122 and +255768678122

Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version: UBATIZO WA KWELI

Huenda hujawahi kujiuliza swali hili kuwa ubatizo wa kweli ni upi? Ni kwanini kuna aina nyingi za ubatizo; yaani ubatizo wa maji mengi au maji machache? Au wa watu wazima au watoto?

Labda nianze na Waefeso.4:5, “Bwana mmoja, imani moja, na ubatizo mmoja”. Biblia inasema kuna AINA MOJA TU ya ubatizo nami napenda tuuangalie kwa undani. Na katika kuangalia aina hii ya ubatizo tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia katika ubatizo ili uwe wa kweli. Ujuzi ambao utawezesha kulinganisha na ubatizo unaoufahamu kwa kuupima kwa kipimo cha maandiko matakatifu ya kuwa niwa ukweli au uwongo.

Mambo ya kuzingatia katika ubatizo wa kweli ni:-

 1. ANAYEBATIZWA ANAPASWA AAMINI, ATUBU NA AUNGAME DHAMBI.
  Ubatizo wa kweli unapaswa kutanguliwa na mambo makubwa manne ambayo ni Kuamini, Kutubu na Kuungama. Marko.16:16, “AAMINIYE na KUBATIZWA ataokoka“; Mathayo.3:6, inasema “naye AKAWABATIZA katika Mto yordani, huku WAKIZIUNGAMA DHAMBI zao” Matendo.2:38, “TUBUNI MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo”.John baptizing
 2. MBATIZAJI NA MBATIZWA WOTE WANAINGIA NDANI YA MAJI.

Wakati Filipo anambatiza Towashi Biblia inasema, Matendo.8:38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Hili ni jambo la muhimu sana, mbatizwa na anayebatizwa wote walikuwa ndani ya maji. Na baada ya ubatizo “…walipopanda kutoka majini…” Matendo.8:39 towashi akaondoka akifurahi. Katika aya hii tunaona jambo la muhimu pia sambamba na mbatizwa na mbatizaji kuwa ndani ya maji, ni kwamba lazima kuwepo na maji mengi.

 1. NI WAKUZAMISHWA KATIKA MAJI MENGI.

Yohana mbatizaji kipindi cha Yesu alikuwa akibatiza katika sehemu iliyokuwa inaitwa Ainoni maana kulikuwa na maji tele, Yohana 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.” Yesu alibatizwa katika mto Yordani, na baada ya ubatizo Mathayo.3:16-17, …mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Mungu hupendezwa nasi kama alivyopendezwa na Yesu tunapotoka katika maji ya ubatizo maana ndivyo inavyotupasa kuitimiza haki yote (Mathayo.3:15) na Yesu alitupatia kielelezo. Lakini pia hutupatia Roho Mtakatifu kama vile hua alivyoshuka kwa Yesu ili atukamilishe kwa kutupatia tabia inayofanana na Yesu, ushindi wa dhamdi na atuongoze na atutie katika kweli yote.

Hivyo mambo haya matatu yanatosha kutuambia ubatizo wa kweli wa Biblia. Ubatizo wa watoto wachanga haufundishwi katika Biblia na wala hatuna mfano wa mtu yeyote tangu MWANZO hadi UFUNUO aliyebatizwa hivyo. Maana mtoto hawezi kuamini, akaungama na kutubu ili abatizwe.
Pia ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani hauna msingi katika Biblia maana haufundishwi katika Biblia bali ni utaratibu ambao umewekwa na wanadamu tu.

Hebu leo turudi katika ubatizo wa kweli maana Yesu anakwambia “amini amini nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Yohana.3:5.

Bwana akubariki sana unapoamua kufanya matengenezo katika jambo hili.

Kwa maoni, maswali au ushauri usisite kuwasiliana nasi.

Advertisements

Mambo Mhimu ya Kuzingatia Katika Chakula Ili Kiwe na Matokeo Mema Mwilini.

Ev. Mujaya MujayaNa. Muinjilisti Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122

+255768678122

Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version:Kanuni Za Kuzingatia Katika Chakula Ili Kiwe na Matokeo Mema Yaliyokusudiwa

Chakula chema ambacho Muumbaji wetu ametupatia ili tukitumie imetupasa tukitumie kwa uangalifu na tahadhali tangu katika uchaguzi na maandalizi yake. Hata chakula kiwe kinafaa kwa namna gani lakini kama kikiandaliwa au kutumiwa vibaya mtu hawezi kunufaika kwacho. Katika sehemu hii tutaangalia kanuni muhimu za uchaguzi, maandalizi na matumizi bora ya chakula ili kifae kuleta matokeo mema yanayotarajiwa na mtumiaji.

Uchaguzi wa Chakula

Watu wengi wanachagua chakula ili kukidhi tamaa ya mwili, kumbe chakula kingechaguliwa kuzingatia utajiri wake wa viritubisho mwilini. Kanuni zifuatazo zafaa kuongoza uchaguzi wetu wa chakula kifaacho:

 1. Kama kuna wakati ambapo chakula tunachokula kinapaswa kuwa rahisi basi ni sasa. Chakula tunachotumia kiwe kinachopatikana kwa urahisi katika mazingira yanayotuzunguka.
 2. Kukidhi mazingira. Chakula tunachokula kinapaswa kiendane na msimu, hali ya hewa na kazi tunayofanya. Chakula kinachofaa kutumika katika msimu au hali ya hewa fulani hakifai kutumika katika mazingira ya msimu na hali ya hewa nyingine. Na pia kuna aina mbalimbali za chakula maalumu kwa kazi au shughuli fulani tu. Chakula cha mtu anaefanya kazi ngumu za nguvu ni tofauti na mtu anayefanya kazi za kukaa ofisini na kutumia akili. Mungu ametupatia aina mbalimbali za vyakula hivyo ni bora kuchagua chakula kukidhi mahitaji yetu.
 3. Utoshelevu, Utamu na aina mbalimbali. Meza zipambwe kwa vyakula vya nafaka, matunda na mbogamboga za aina mbalimbali, tamu sana na zenye utajiri wa virutubisho.

Maandalizi ya Chakula

Chakula kilichochaguliwa vema ili kifae kutumika pia kinapaswa kuandaliwa vema. Tatizo kubwa lipo katika maandalizi ya chakula kabla hakijaletwa mezani. Wanawake na wanaume wengi sana hawajui kuandaa chakula ambacho Mungu amewapatia na hivyo kukiweka mezani kikiwa tupu bila virutubisho au kikiwa kimejaa sumu mbalimbali na vimelea vya magonjwa. Taaluma ya kuandaa chakula bora katika mazingira ni muhimu sana kwa wanaume na wanawake wote. Kanuni zaSAM_0454 maandalizi ya chakula ni:

 1. Osha matunda na mbogamboga kwa maji safi kabla haiuazitumia. Vyombo vyote vya kuandalia chakula, mazingira ya kuandalia chakula na muandaaji wanapaswa kuwa safi. Kichwa kifunikwe kuzuia uchafu kutoka katika nywele kuvamia chakula.
 2. Kisichokobolewa au kusafishwa sana.
 3. Kisichoiva sana kama ni mbogamboga na nafaka mbichi/zenye ukijani. Matunda na mbogamboga mbichi/zenye ukijani zina manufaa sana zikitumiwa mbichi kuliko zikipikwa japo zingine ni lazima zipikwe kidogo. Unaweza kupika kwa kutumia mvuke ili kutunza/kuhifadhi virutubisho.
 4. Kamwe usimwage maji uliyotumia kuandaa mbogamboga bali uyaweke sehemu ya mboga yako maana ni tajiri ya virutubisho muhimu. Ili kufanikiwa katika hili, unapaswa kuweka kiasi kidogo cha sana maji wakati unaandaa mboga yako kitakachotosha kuivisha tu. Kama utahitaji mboga isiyo na majimaji, basi hakikisha unayanywa maji yote baada ya kuyatenga na mboga yako.
 5. Pika viazi na maboga pamoja na maganda yake, bila kumenya. Nusu nchi ya nje ya viazi na maboga ni sehemu muhimu kuliko zote za boga au kiazi hivyo hakikisha haumenyi kabla ya kupika kuzuia kutupa virutubisho. Fanya hivi hata kwa viazi mviringo.
 6. Kisichokolezwa kwa viungo na vichocheo vingi. Sukari. Chumvi, Amira na Soda
 7. Kitamu, kinapendeza kukitazama, kinanukia vizuri, ladha nzuri, virutubisho vingi vya hali ya juu, si cha gharama kubwa, urahisi wa kutayarisha na hakina gharama.
 8. Usitumie vyombo vya Aluminiamu kuandaa chakula. Usichemshe maji katika vyombo hivi wala usinywe juisi au maji yaliyotunzwa katika chombo cha aluminiamu.

Matumizi ya Chakula

 1. Kula kwa wakati. Chakula hakipaswi kuliwa mapema sana au kwa kuchelewa sana, inapaswa kuwe na ratiba ya chakula.
 2. Usile kupita kiasi. Tumia chakula kinachotosha tu kutosheleza njaa kisha acha. Kipimo cha chakula unachojipimia kulainapaswa uweze kula nusu yake tena ikiwa utapewa baada ya kumaliza.
 3. Usijaze chakula kingi mdomoni. Katika kula chakula, weka kiasi kidigi tu kinachotosha kutafunwa vema na kuchanganywa na mate.IMG_20131029_210909
 4. Tulia na kula taratibu. Usile chakula ukiwa katika harakaharaka, ukiwa una uchovu au hasira kali. Wakati mzuri wa kupumzika ni kabla yam lo na kutembeatembea baada yam lo.
 5. Tafuna chakula chako vizuri maana tumboni hamna meno mengine. Kwa kutafuna vizuri unaweza ukapata nguvu na virutubisho vingi katika kiasi kidogo tu cha chakula.
 6. Usile michanganyiko mingi ya chakula kwa wakati mmoja. Unahitaji aina tatu au nne tu ukiongeza chumvi na mafuta kidogo tu.
 7. Epuka michanganyiko mikali ya chakula. Chakula unachotumia kisiwe kimechanganywa sana maana kitavuruga tumbo na kuchelewesha mmeng’enyo.
 8. Badilisha chakula chako kati ya mlo mmoja na mwingine. Kama umekula viazi mlo mmoja basi kula ugali au ndizi mlo mwingine.
 9. Mbali na juisi ya matunda halisi au mbogamboga, kunywa maji kati ya milo wala si pamoja na chakula chako.
 10. Usichanganye matunda na mbogamboga, kama umekula matunda mlo mmoja basi kula mbogamboga mlo mwingine.
By ShareHope Ministries Posted in Health

Kuishi Maisha Ya Umilele

KARIBUNI TENA KATIKA SEMINA YETU TULITAFAKARI NENO LA MUNGU WETU
“INAWEZEKANA KUISHI MILELE”

tuinf

SOMO LA TANO LINASEMA: Kuishi Maisha ya Milele

Dr. Edward MhinaFungu Kuu: “Na uzima wa milele ndio huu wa kujue wewe, MUNGU wa pekee wa kweli,

                      na YESU Kristo uliye mtuma” Yohana 17:3

Na. Dkt. Edward Raphael Mhina

Downloadable Version: Kuishi Maisha Ya Umilele-Dkt. Edward Mhina

Somo la hili ndugu msomaji linanipa faraja sana katika moyo wangu, ya kwamba ijapokuwa tunaishi katika ulimwengu uliochoka lakini bado tunaweza kuchagua maisha ya milele ya kuishi katika faraja tele tukiwa na YESU Kristo. Hakika nakwambia ya kwamba tukitaka kuishi ndani ya YESU inatubidi kuzaliwa upya, Yohana 3:3-6 hapa YESU mwenyewe anasema ya kwamba kama hatutazaliwa upya ni vigumu kuuona ufalme wa mbinguni. Ijapokuwa tunaweza kuwa na maswali kama ya Nikodemo kwamba tunawezaje kuzaliwa mara ya pili? Lakini jibu YESU alilitoa katika fungu hilo la Yohana ya kwamba “ni lazima tuzaliwe tena kwa maji na roho” na amesema ya kwamba aliyezaliwa na mwili ni wa mwili na aliyezaliwa na roho ni wa roho.

Kwakweli ilitufanane maisha yetu kama YESU ni lazima tuwe katika ulimwengu wa roho yani tukiri ya kwamba YESU ni mwokozi wa maisha yetu kwa kubatizwa tena ubatizo wa maji mengi kama yeye alivyofanya akiwa hapa duniani, kwasababu 1Yohana 2:6 anasema “Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vilevile kama yeye alivyo enenda”

Nakama tayari umempokea YESU kristo katika maisha yako lipo fungu katika Wakolosai 2:6 “BasiSAM_3262 kama mlivyompokea kristo YESU , BWANA, enendeni vivyo hivyo katika yeye.”
Hakuna faida tutakayoipata rafiki yangu tusipochagua upande sahihi. Napendekeza kwako kumchagu a YESU awe mwongozo na kielelezo katika maisha yako. Nakwambia hili kwa uhakika ya kwamba utaona uso wa YESU katika maisha yako na kila kitu kitabadilika. Lakini tunawezaje kuzaa matunda mema basi? tukiwa nje ya YESU? La! hasha hatuwezi kama Yohana 15:4 “Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.”

Hivyo ili tupate matunda mazuri katika maisha yetu, kazi zetu, masomo yetu, biashara zetu na mambo yetu yote njia bora ni kukaa ndani ya YESU, ubarikiwe sana unapokwenda kufanya uamuzi.

Sali nami sala hii tunapo hitimisha mada hii:

Nakupenda sana MUNGU wangu sababu wewe ulinipenda upeo hapo mwanzo nab ado umenipa jinsi ya kuweza kuwa na wewe wakati wote ni saidie nifanye matengenezo, BWANA ikiwa nimapenzi yako nifanye nisome tena kesho neno lako, kwa jina la YESU kristo Amen!
KARIBUNI SANA KATIKA SOMO LINALOFUATA MAANA TUTAENDELEA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU.

SOMO LINALOFUATA: Kuja kwa Bwana wa Umilele

Maswali, Maoni au Ushauri wasiliana nami: +255652648737 au +255768678122

Yesu ni Mwanzilishi wa Pumziko la Milele?

KARIBUNI TENA KATIKA KULITAFAKARI NENO LA MUNGU WETU ALIYE HAI

“INAWEZEKANA KUISHI MILELE”

EDDIEe

SOMO LA NNE LINASEMA: Yesu ni Mwanzilishi wa Pumziko la Milele?
Dr. Edward MhinaFungu Kuu: “Na uzima wa milele ndio huu wa kujue wewe, MUNGU wa pekee wa kweli, na YESU Kristo uliye mtuma” Yohana 17:3

Downloadable Version: Yesu Ni Mwanzilishi Wa Pumziko La Milele?

Na. Dkt. Edward Raphael Mhina

Biblia inafundisha kuhusu habari za pumziko la milele. Siku ya Sabato. Sabato ni pumziko ambalo MUNGU alimpatia mwanadamu kama zawadi siku ya saba ya uumbaji. Ukisoma katika kitabu cha Mwanzo kinazungumzia uumbaji ambao MUNGU aliufanya kwa kutamka ‘Neno’, na katika kitabu cha Yohana 1:1-3 anazungumzia huyo ‘Neno’ ni YESU Kristo. Hii huthibitisha ya kwamba YESU aliiumba Sabato. Tunaona pia katika bustani ya Edeni MUNGU anawapa Sabato wazazi wetu wa kwanza Adamu na Hawa.

Pumziko hilo ni la milele zote, hadi mbingu mpya nan chi mpya zitakazofanywa na Mungu mahali ambapo watu watakaookolewa wataishi mbele za Mungu milele, watakatifu wa Mungu wataendelea kupumzika katika siku hii, Isaya 66:22-23, “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu, asema Bwana, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na sabato hata sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema Bwana.”

Katika mafundisho ambayo watu wamesoma maanadiko na kuyaelewa vibaya ni pamoja na hili la Sabato ndio maana leo utakuta kuna makanisa/madhehebu mengi ya wanaoabudu siku tofauti tofauti za juma lakini tujiulize katika vichwa vyetu je, ni siku gani ambayo MUNGU wetu alikusudia tuitunze ikiwa kama zawadi yake kwetu?. Ukisoma katika kitabu cha Kutoka 20:8-11 “Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa..”

Utashangaa jinsi Mungu alivyo wa upendo maana hii ni amri/kanuni ya nne katika zile kanuni/ amri kumi ambazo MUNGU alitupatia ili tuishi milele. Lakini kanuni hii imeanza na neno ikumbuke ikiwa na maana ya kwamba MUNGU alikwisha itoa hapo mwanzo alipoiumba dunia na kuwapa wazazi wetu wa kwanza , hivyo anatukumbusha kuitunza kama alivyo kusudia.

jesus and the sabbathNdugu msomaji nisipo lisema hili ambalo moyo wangu unanisukuma kukuambia nita ulizwa na MUNGU kwanini sikuliandika. Ukweli ni kwamba watu wanajaribu kupindisha ukweli juu ya siku hii ya saba ya kila juma ambayo ni Sabato lakini napendekeza kwako kuiangalia biblia pekee kama mwongozo wa maisha yetu kwamba inatuambia nini. Wengi husema ya kwamba Sabato ilikoma pale msalabani lakini YESU mwenyewe anasema kupitia Mathayo 5:17-18
“Msidhani ya kwamba nilikuja kuitangua torati au manabii,la, sikuja kutangua ,bali kutimiliza,18 Kwa maana amini nawaambia ,mpaka mbingu na nchi zitakapo ondoka ,yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka , hata yote yatimie” Hakuna kilicho futwa katika amri za MUNGU ikiwemo sabato ndani yake.

Wote tunaamini ya kwamba YESU alifufuka siku ya tatu kutoka kaburini na wengi huamini ya kwamba Ijumaa kuu ni siku ambayo YESU alikufa alishinda kaburi Jumamosi na na siku ya tatu yani Jumapili akafufuka ambayo wengi husheherekea. Siku hiyo ya Jumapili katika maandiko matakatifu inaonesha ya kwamba ni siku ya kwanza ya juma soma nami katika Mathayo 28:1 “Hata sabato ilipo kwisha, ikapambazuka siku ya kwanza ya juma. Mariamu Magdalena na Mariam yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi” hivyo tunaweza kusema ya kwamba hata YESU alitunza Sabato kwa kutofufuka siku ya saba ya juma ambayo ni Jumamosi. Ukweli ni kwamba lazima tufuate kile kinachoelezwa katika biblia na kama sisi kweli ni wakristo ikiwa na maana ya kwamba tuna mfuata kristo yeye anasema hivi katika Marko 2:28 “Basi mwanawa Adamu ndiye BWANA wa sabato” hivyo twapaswa kufuata kile ambacho yeye anataka tufuate. Napendekeza kwako kuishika sabato ya MUNGU katika biblia na si ile iliyowekwa na mwanadamu hizo Sabato za kimapokeo ambayo watu wengi kwa kuifuata huku wakiijua Sabato ya kweli kama ilivyofunuliwa katika maandiko matakatifu watakosa uzima wa milele.
Sali nami sala hii ninapohitimasha somo hili:

MUNGU muumbaji wa Sabato nisaidie niuelewe ujumbe huu na kwa haraka nifanye matengenezo, kuwa mwalimu wangu ninapoendelea kujifunza masomo haya, kwa njia ya Roho wako Mtakatifu uwe kiongozi wangu pekee, ukinithibitisha imani yangu na kunituliza katika kweli ya Neno lako, na unisaidie nisikose somo linalofuata. Kwa jina la YESU KRISTO amen!
KARIBU TENA TUTAENDELEA KUTAFAKARI NENO LA MUNGU KATIKA SEMINA HII.

SOMO LA LINALOFUATA: Kuishi Maisha ya Milele

Maswali, Maoni au Ushauri wasiliana nami: +255652648737 au +255768678122