UNABII WA MIAKA 2300

Ev. Peter Jeftah

Ev. Peter Jeftah

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Peter I. Jefter

Simu: 0757916891/ 0653401497

Downloadable Version: Unabii wa Miaka 2300

Daniel 8:13, 14…. 13, Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14, Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Ni katika kipindi cha utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli mwana wa mfalme Nebukadneza (Daniel 5:2) ndipo Daniel anaoneshwa maono haya Daniel 8:1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya yaliyonitokeahapo kwanza. Akiwa katika wilaya ya Elimu, shushani ngomeni katika mto ulai huko Babeli

Mwanzo wa njozi ya Danieli anaoneshwa kondoo mwenye pembe mbili akisimama na kutawala dunia akisukuma upande wa magharibi na kaskazini na kusini (Daniel 8:3, 4). Kisha anaona beberu akiinuka upande wa mashariki akiwa na pembe mashuhuri kati ya macho (Daniel 8:5). (kwa faida ya msomaji pembe katika unabii huwakilisha ufalme au utawala). Akamkaribia Yule kondoo akamkasirikia kwa ghadhabu nyingi naye akampiga hata kuvunja pembe zake, akamwangusha chini hata kumkanyaga-kanyaga

Baadaye ile pembe ikavunjika kwa kujitukuza hata zikatokea pembe nne zikaielekea pepo nne za mbingu nazo zikatwala kwa kipindi Fulani (Daniel 8:8). Daniel 8:9 Na katika moja ya hizo pembe ilitokea pembe ndogo, iliyokuwa sana, upande wa kusini, na upande wa magharibina upande wan chi ya uzuri. Pia katika fungu la 23; Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo………atasimama. Hii humaaniasha wakati wa mwisho wa utawala wa falme nne zilizoinuka kutoka kwa Yule beberu ndipo utainuka tena ufalme mwingine unaowakilishwa na pembe ndogo, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo.

Daniel 8:10-14 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni ; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na nyota ikazikanyaga. Naam ikajitukuza hata juu ya aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Kuinuka kwa pembe hii ndogo na matendo yake ndiko kunamhuzunisha mtakatifu mmoja na hivyo inampelekea kutaka kujua hatima ya haya yote. Nayo ni nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu (2300).

Nini tafsiri yake miaka hii 2300??

Katika sura ya Daniel 8:14 tunaambiwa matukio haya yatachukua muda nyakati za jioni na asubuhi 2300 lakini hatuambiwi chochote kuhusu mwanzo wala mwisho wake.

Katika kuelewa tafsiri hii lazima tuelewe mambo yafuatayo.

  1. nyakati za jioni na asubuhi ni sawa na siku nzima amabyo pia huanza jioni hata jioni. Mwanzo 1:5………… ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. kwahiyo nyakati za jioni na asubuhi 2300 ni sawa na siku kamili 2300
  2. Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja Ezekiel 4:6………siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza kwahiyo siku 2300 za kiunabii ni sawa na miaka iliyokamilika 2300.. Hivyo tunasema ili haya yote yafikie mwisho ni mpaka kukamilika kwa miaka 2300.
  3. Unabii wa miaka 2300 ndio unabii mrefu kwenye biblia kuliko mengine yote, hivyo unabii mwingine kama vile miaka 1260, majuma 70, miaka 1335 na 1290 zote huangukia kwenye miaka 2300.

Mwanzo wa miaka hii ni upi?

Mwanzo wa miaka hii tunaelewa kwa kuelewa mianzo ya majuma 70 katika Daniel 9:24. Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu………,25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya mji wa Yerusalemu….. kutakuwa na majuma saba………….

Majuma sabini ni sawa na miaka 490. 70×7=490. Hii hutuambia kuwa kulikuwa na miaka 490 ulioamriwa juu ya taifa la Israeli.

Amri juu ya ujenzi wa mji wa yerusalemu ulitolewa na mfalme Artashasta mfalme wa uajemi mnamo mwaka wa 457 K.K (kabla ya kristo) Ezra 7:21-26 Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina…..hata kiasi cha cha talanta mia za fedha …. kila neon litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya ya nyumba ya Mungu wa mbinguni…….. Kuanzia mwaka wa 457 hitimisho la miaka 490 au majuma 70 hufikia 34 B.K (baada ya Kristo), (kumbuka kuna mwaka kutoka 0-1)….katika miaka 2300 baada ya kukamilika kwa miaka 490 tunasalia na miaka 1810.

490+1810=2300.na

Siku 2300 zilioneka kuanza wakati amri ya Artashasta kwa ajili ya urejeshwaji wa na ujenzi wa Yerusalemu ilipotolewa majira ya kipupwe ya mwaka 457 K.K. Kwahiyo mwanzo wa miaka 2300 ni mwaka 457 B.K na huishia mwaka 1844 B.K.

Bwana atubariki tukutane sehemu ya pili kujifunza matukio makubwa yaliyotabiriwa na kutokea katika kipindi hiki cha miaka 2300.

Imeandaliwa na

PETER I. JEFTER 0757916891/ 0653401497

Advertisements

THAMANI YA MWANADAMU KWA MUNGU

IMG_20150830_174425Na. Muinjilisti: John Mafuru Musibha

Simu Na.        +255 652 045 317

+255 764 736 335

Downloadable Version: THAMANI YA MWANADAMU KWA MUNGU

Ndugu msomaji wa mada mbalimbali katika blog ya ShareHope Ministries ni wasaa mwingine tena ambapo tunaendelea kukuletea mada mbalimbali za kumtukuza Mungu wetu wa mbinguni pia kujifunza ukuu wake katika maisha ya mwanadamu. Siku hii ya leo nimewiwa kukuletea mada hii ambayo tutajifunza thamani ya wanadamu kwa Mungu wetu wa Mbinguni.

Mpenzi msomaji somo hili linaturudisha nyuma mpaka kipindi cha uumbaji, Mwanzo 1:26 inasema, “Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi” katika aya hii tunagundua ya kwamba katika uumbaji wote, mwanadamu alithaminiwa sana kwa maana Mungu muumbaji alisema na “tumfanye mtu kwa mfano wetu,” ni thamani kubwa sana kuumbwa tena tukiwa tunamfanana Mungu wetu wa mbinguni, na jambo la pili ni kwamba alitupa mamlaka juu ya kila kitu alichokiumba kilichopo ardhini na majini. Tumepewa mamlaka ya kutawala viumbe vyote ambavyo Mungu ameviumba hivyo ni thamani iliyokubwa sana.

Mfano wa mamlaka aliyopewa mwanadamu yanapatikana katika kitabu cha Mwanzo 2:19-20 Mungu aliwaleta viumbe vyote alivyoviumba mbele ya Adamu ili aweze kuwapa majina na mpaka leo majina tunayoyatumia Adamu ndiye aliyewapa. Mfano chukulia katika familia yenu nyumbani, wazazi wako wanakupa mamlaka ya kutawala miradi yao yote na baadhi ya vitu muhimu, je utajiskiaje? Je ni thamani kubwa kiasi gani kwako? Jaribu kuelezea kwenye kipande cha karatasi kama umepitia uzoefu huo.

Katika kitabu kiitwacho Zaburi 8:4Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie”? mtunga Zaburi anaumuuliza Mungu je binadamu ni nani hata umkumbuke baada ya kuangalia ukuu wake na jinsi alivyoumba vitu vingi leo hii anamkumbuka mwanadamu na anaamua kumuokoa, hii yote ni thamani ya mwanadamu kwa Mungu, 5.Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu, Umemvika taji ya utukufu na heshima; fungu hili linaonesha katika uumbaji akitoka Mungu anaefatia mwanadamu. Mpenzi msomaji Malaika waliumbwa kama wajumbe kati ya mwanadamu na Mungu wetu.6. Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake 7.Kondoo na ng’ombe wote pia;Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini;Na kila kipitacho njia za baharini. Aya ya 6 mpaka ya 8, linatukumbusha kile ambacho Mungu alikisema katika kitabu cha Mwanzo kwamba, baada ya kumuumba mwanadamu alimpatia mamlaka ya kutawala kazi zote za mikono ya Mungu yaani viumbe vyote alivyoviumba.

Ndugu msomaji, thamani ya mwanadamu ni kubwa sana mbele za Mungu na ndio maana Mungu wetu wa mbinguni akaandaa mkakati wa kutuokoa ili baade tuje tuishi kama ambavyo Mungu wetu wa Mbinguni alivyopanga mwanadamu aishi. Wito wangu na wito wetu kwetu leo hii katika kipindi hiki cha mwisho ni kuurudisha uthamani ambao tunao mbele za Mungu. Tuchague kuishi maisha matakatifu yasiyo na mawaa. Mungu wetu anatukumbuka na atatusamehe na kuwa na mahusiano mazuri na sisi kwa sababu huwa yupo karibu na mwanadamu siku zote. Panga kuurudisha uthamani huu mbele za Mungu. Roho wa Mungu atakusaidia katika maamuzi hayo, usipange kukosa ufalme wa Mungu ajapo mara ya pili kutuchukua. Usisite na wala usiangalie mtu fulani, fanya maamuzi sahihi sasa wakati bado ungalipo kwa maana zitakuja nyakati ambazo hutaweza kupata nafasi kabisa. Wasiliana na kanisa la waadventista wasabato lililopo karibu nawe ili uweze kupata mafundisho zaidi kuhusu wokovu na biblia kiujumla.

Kwa maswali, maoni au ushauri;

Tafadhali wasiliana nami kupitia;

Simu Na.        +255 652 045 317

+255 764 736 335

CHUKIZO LA UHARIBIFU (The abomination of desolation)

Ev. Peter Jeftah

Ev. Peter Jeftah

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Peter I. Jefter

Simu: 0757916891/ 0653401497

Downloadable Version: CHUKIZO LA UHARIBIFU

Mathayo 24:15, Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Daniel, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu).

Sura ya 24 ya kitabu cha Mathayo (Mathayo 24) ni sura maarufu na maalum kwa matukio au dalili (ishara) za kurudi kwa Kristo. Yesu akiwa na wanafunzi wake akiwafundisha kuhusu ishara za marejeo yake hakuwaficha pia juu ya chukizo la uharibifu.

Lakini Je, chukizo la uharibifu ni nini??

Katika kipindi cha wana wa Israeli zamani hizo kitu chochote kilichokuwa kinyume na sheria za wayahudi au kilikuwa tofauti na ibada zao kilikuwa ni chukizo kwao. Kwa mfano kushikamana na wamataifa (wasiotahiriwa) ilikuwa ni chukizo kwa kuwa waliku najisi.

Tangu Misri Bwana hakuruhusu huduma zake takatifu zifanyike huko kwakuwa wamisri waliabudu miungu mingine. Huduma zozote za kiibada zilizofanywa kinyume na ibada takatifu yalikuwa ni machukizo. Kutoka 8:26, Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwakuwa tutamchinjia sadaka BWANA, Mungu wetu na hayo machukizo ya Wamisri; Je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe. Soma pia mwanzo 42:32 na 46:34. Wamisri na Waebrania kuchangamana ilikuwa ni machukizo.

Katika kipindi cha utawala wa Sulemani Je? Kitendo cha Sulemani kuoa wanawake wengi pia kilikuwa ni machukizo kwa MUNGU 1Wafalme 11:5- 7 Kwakuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, Mungu mke wa wasidoni na Milkomu, chukizo la waamoni Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea Komeshi, chukizo la wamoabu, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu na Moleki, chukizo la wana wa Amon. Soma pia 2Wafalme 23:13

Baada ya kuona maana ya chukizo. Turejee katika fungu letu la mathayo 24:15. Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Daniel ni nini?? Na nini ishara zake?

Daniel 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka ya dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo hata ukomo, na gadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

Mafungu haya ni muendelezo wa mafungu ya nyuma yakizungumzia juu ya unabii wa majuma 70 yaliyotabiriwa juu ya wayahudi na huduma ya YESU na kukataliwa kwa injili ndani ya uyahudi kisha kutoa nafasi kwa wamataifa kusikia injili.

Katika tafsiri ya majuma 70 tumeona ilianza mwaka wa 457 K.K na kuishia mwaka wa 34 A.D. juma moja la mwisho ambalo Yesu anaweka agano thabiti na watu wengi huanzia mwaka wa 27 A.D ambapo YESU alianza huduma yake duniani nayo huishia mwaka wa 34 A.D kukataliwa kwa injili na kuuawa kwa Stephano (matendo 7:54-60) ambapo nusu ya juma hilo. (kwakuwa juma lina siku 7 nusu yake itakuwa ni 31/2) huanza mwaka wa 27 A.D Kristo anapoanza huduma yake hadi 301/2 A.D anapokatiliwa na kuuawa. Nayo nusu nyingine huanza 301/2 A.D injili kwa wayahudi kwanza hadi 34 A.D wanaikataa injili na kuwaua watumishi wa MUNGU kisha mlango wa injili kwa wamataifa inafunguliwa.

Baada ya hayo ndipo litakaposimama chukizo la uharibifu, hii humaaisha kuwa baada ya huduma ya Yesu kukataliwa nao wayahudi pia kuikataa injili badala yake litasimama uharibifu mkubwa na machukizo mengi. Daniel 11:31 na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu hapa Biblia hutuambia juu ya pembe ndogo iliyoinuka katika (Daniel 8:9.) ambayo katika Daniel 8:11 Naam ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa.

(patakatifu palipoangushwa hapa ni hekalu la Yerusalemu liliangushwa na utawala wa kirumi katika mwaka wa 70 A.D Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Yesu alitabiri juu ya anguko la Yerusalemu katika Mathayo 24:2……. Amin nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa

Daniel 12:11 Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itakapoondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na sitini. (siku elfu mia mbili na sitini sawa na miaka 1260 huanza 538-1798 kuinuka kwa upapa hadi kutiwa kwake jeraha la mauti, Dan 7:25, Ufunuo 13:3).

Yesu anazungumzia anguko la mji wa Yerusalemu kama chukizo la uharibifu. Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Kubomolewa kwa hekalu la Yerusalemu mnamo mwaka 70A.D huashiria mwisho wa taifa la Israeli na ambapo wengi wao walikimbilia katika mataifa mengine, wengine walichukuliwa mateka. Baada ya kipindi hicho ndipo ukainuka utawala wa upapa ulioleta mafundisho ya uongo na kutengua sheria za MUNGU na kulazimisha watu kuyashika yaliyo kinyume na kweli nacho kilikuwa kipindi kilichoitwa zama za giza ambacho kilidumu kwa miaka 1260……….

Chukizo la uharibifu unafananishwa na kipindi kinachokuja mbele yetu, atakaposimama Yule mharibifu mpinga Kristo. 2 Wathesalonike 2:1-4 Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitishwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo, Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa kwanza YULE MTU WA KUASI, MWANA WA UHARIBIFU………..akijionesha nafsi yake ya kwamba yeye ni Mungu.

Atakapo simama Yule mpinga kristo na kuhalallisha mafundisho ya uongo (angalia fungu la 9), pale sabato bandia itakapochukua nafasi ya Sabato halisi (Jumapili kuchukua nafasi ya Jumamosi) haya yote yatakuwa ni machukizo mbele za Mungu.

Ahadi ya MUNGU kwako.

Ufunuo 3:10 kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi name nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwenguwote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

BWANA AKUBARIKI.

Imeandaliwa na

PETER I. JEFTER 0757916891/ 0653401497

JE, YESU NI MWANA WA MUNGU?

IMG_20150830_174425Na. Muinjilisti: John Mafuru Musibha

Simu Na.        +255 652 045 317

+255 764 736 335

Downloadable Version: JE, YESU NI MWANA WA MUNGU?

Hili ni swali ambalo linawasumbua watu wengi sana hasa wale wenye imani tofauti na ya Kikristo. Wamekuwa wakipata shida sana katika kulielewa hili jambo lakini kwa neema ya Mungu leo wote wanaenda kupata majibu ya swali hili tena ni jibu thabiti kibiblia. Ndugu zangu Mungu wetu wa mbinguni ndiye muumba wa mbingu na nchi na kila kilichomo.

Kutokana na baadhi ya imani zingine wanaamini kuwa Mungu hawezi kuzaa na hawezi kuwa na mke. katika hili jambo, watu wameshindwa kuelewa uzazi unaozungumziwa katika Biblia na wakati imani zao wanaamini ya kwamba Mungu ameumba viumbe vyote. Tatizo linaloonekana hapa ni uzazi tu na sio kitu kingine kwa sababu wamekuwa wakiuliza kwanini Mungu azae?

Kwa habari ya kuzaa, Je! Mungu anazaa au hazai?

Kwanza tuangalie kuna aina ngapi za uzazi. Yohana 3:6 inasema “kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho” kutokana na aya hii tunagundua ya kwamba kuna aina mbili za uzazi, nazo ni uzazi wa kimwili na uzazi wa kiroho. Na Biblia inasema kilichozaliwa kwa mwili ni mwili na kilichozaliwa kwa Roho ni roho, hivyo Wakristo wanaposema YESU ni mwana wa Mungu wanamaana ni mwana wa Mungu Kiroho na sio uzazi wa kimwili kama ambavyo mimi na wewe tumezaliwa kutoka kwa wazazi wetu. Mfano wa uzazi wa Kiroho Yakobo 1:18 “kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limbuko la viumbe vyake”. Ukisikia Mungu ana wana basi usifikirie kwamba ana mke, hapana yeye anatuzaa sisi kwa Roho.

Je, kutokana na Biblia wazo la YESU kuitwa mwana wa Mungu linatokana na nini?

Luka 1:34-35Mariamu akamwambia Malaika ,litakuwaje neno hili maana sijui mume? 35 Malaika akajibu akamwambia, Roho mtakatifu atakujilia juu yako , na nguvu zake aliye juu zitakufunika kama kivuli, kwa sababu hiyo hicho kitakachozaliwa kitaitwa kitakatifu, Mwana wa Mungu. Biblia ipo wazi sana hivyo imethibitisha kwamba YESU ni Mwana wa Mungu kiroho. Na katika maandiko ya Biblia takatifu YESU mwenyewe anakili ya kwamba ni Mwana wa Mungu Yohana 9:35-38 Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, wewe wamwamini Mwana wa Mungu? 36 Naye akajibu akasema, Ni nani Bwana, nipate kumwamini? 37 Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. 38 Akasema ,Naamini,Bwana. Akamsujudia.

Kwa kinywa chake YESU KRISTO anashuhudia ya kwamba yeye ni Mwana wa Mungu aliye hai. Natumaini mpenzi msomaji umeelewa dhana nzima ya YESU KRISTO kuitwa Mwana wa Mungu na wakristo katika ulimwengu wote. Kama una swali lolote uliza na kwa neema ya Mungu tutakujibu . Asante sana na Mungu akubariki

Wasiliana na kanisa la waadventista wasabato lililopo karibu nawe ili uweze kupata mafundisho zaidi kuhusu wokovu na biblia kiujumla.

Kwa maswali, maoni au ushauri;

Tafadhali wasiliana nami kupitia;

Simu Na.        +255 652 045 317

+255 764 736 335