UNABII NI NINI??

Ev. Peter Jeftah

Ev. Peter Jeftah

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Peter I. Jefter

Simu: 0757916891/ 0653401497

Downloadable Version:Unabii ni Nini?

2 Petro 1:19, Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi,ambalo, mkiliangalia, kama taa ing’aayo mahali penye giza…….

Mara nyingi kumekuwepo na maswali meni mbalimbali ambayo wengi wetu tumejiuliza kuhusu unabii, na wengi pia tumeshindwa kuelewa unabii, wengine hata wamediriki kuyakataa mafundisho ya unabii katika makanisa yao kwa sababu ya kutokueleweka kwake na baadhi wamesema muda bado wa kujifunza unabii kwa kuwa ni maandiko maalum kwa ajili ya kipindi cha mwisho ( Je, kipindi cha mwisho ni kipi???).

Unabii ni mafunuo ya Mungu aliyoyaleta kwa wanadamu kwa njia ya maono kupitia watu maalum (Manabii) walioteuliwa na Mungu kwa ajili ya kufikisha ujumbe uliokusudiwa kwa jamii au watu husika. Yeremia 1:5, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Unabii haukuletwa wala kufasiriwa kwa mapenzi ya mwanadamu yeyote, bali alipaswa kufikisha ujumbe kama alivyopokea kwa Mungu.2Petro 1:20,21 Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii haukuletwa popote kwa mapenzi ya wanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho mtakatifu. Mapenzi ya Mungu yalifika kama alivyo kusudia yeye mwenyewe. Yeremia 1:6 ……. maana utakwenda kwa kila mtu nitakaetuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru

Makusudi ya Mungu kuwateua manabii na kuwatuma kupeleka ujumbe ulikuwa ni kupeleka maonyo, mafundisho, maongozo nk. 2Timotheo 3:16,17 Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema. Maandiko yote katika Biblia ni hai kwa kuwa yanashuhudiwa kuwa yana pumzi ya Mungu na hivyo yafaa kwa kuelimisha na kuongoza katika haki na kweli.

UNABII ULILETWA KAMA UFUNUO/MAONO

Unabii wa Mungu uliletwa kwa wanadamu (manabii) kama maono au njozi lakini pia hawakuacha kuoneshwa tafsiri yake. Ufunuo 1:1 Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumwa wake Yohana; mtiririko wa maono haya ulianza kwa Mungu, akapewa Yesu kupitia mkono wa malaika unafika kwa Yohana. Malaki1:1 Ufunuo wa neno la Bwana kwa Israeli kwa mkono wa Malaki,

KWANINI TUSOME UNABII??

Imetupasa kusoma unabii kwakuwa yote yaliyotabiriwa hayana budi kutokea upesi na hivyo kuwa wanafunzi wa unabii kunatupelekea kuelewa makusudio ya Mungu kwetu hata leo Ufunuo 1:1….. Awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo hayana budi kuwako upesi……. kila kilichotabiriwa katika Biblia ni lazima kitatimia wala hakitapita kamwe. Mathayo 5:18 ….. mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka hata yote yatimie.

Wana heri hao wasomao na kuyashika maneno ya unabii. Ufunuo 1:3 Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Kinyume cha neno heri ni ole…. neno ole humaanisha onyo, kwahiyo kinye cha neno onyo ni bahati njema/nzuri. Tangazo la bahati njema Mungu anaitoa kwa hao wasomao maneno ya unabii na si kuyasoma tu bali pia kuyashika ikiwa na maana kuwa tuyasome maneno ya unabii huu na kuyashika/ kuyatii maagizo hayo, kwa sababu wakati u karibu.

Imetupasa pia kuyasoma na kuyashika maneno ya unabii kwa sababu yote yaliyotabiriwa sasa twayaona yakitokea. Ni bahati tu kwao hao wanayoyaelewa hayo yaliyosemwa kwa kuwa ndio nyakati zile zilizonenwa kuwa ni za mwisho. Daniel 12:9 Akasema enenda zako, Danieli maana maneno haya yamefungwa, na kutiwa muhuri, hata wakati wa mwisho. Na hivyo imetuapsa kuachana na dhana zisemazo ya kuwa unabii ni mgumu haueleweki au hakuna mwanadamu awezaye kuelewa kitabu cha unabii au hata hao wasemao wakati wa kujifunza unabii bado haujafika. Wana heri hao wazisomao na kuyatii hayo……… wakati wa kusoma unabii ndio sasa.

Wapo manabii wengi kwenye Biblia kama vile Eliya, Elisha, Samwel, Daniel, Yohana, Isaya nk. Wapo walioandika vitabu katika Biblia wengine wameelezewa tu kama walikuwepo. Katika Biblia kuna vitabu 18 vya unabii vikiwa katika mgawanyiko wa unabii mkubwa na unabii mdogo. Vitabu hivyo ni:-

Unabii mkubwa

1, Ufunuo 2, Danieli 3, Isaya 4, Ezekiel 5, Yeremia

Unabii mdogo

1, Hosea 2, Yoeli 3, Amosi 4, Obadia 5, Yona 6, Mika 7, Nahumu 8, Sefania 9, Hagai 10, Zekaria 11, Habakuki 12, Malaki 13, maombolezo ya Yeremia

Utoafauti unaofanya kuwa kwa unabii mdogo na mkubwa sio waandishi kama tutakavyodhani la! Manabii wote ni sawa isipokuwa utofauti wa udogo na ukubwa ni ujumbe. Wengine huitwa manabii wakubwa kwa sababu ya ukubwa wa ujumbe na wengine huitwa wadogo kwa sababu ya udogo wa ujumbe wao.

NABII NI NANI??

Nabii ni mteuliwa wa Mungu aliyeitwa kupeleka ujumbe kwa watumwa/ watu wa Mungu kama vile Yohana, Yeremia Ezekiel nk.,. Wengine waliitwa kufunua siri zilizofichwa kama vile Danieli. Nabii hakutokea tu kusikojulikana au mtu yeyote kutokea na kujitangaza kuwa yeye ni nabii kama ilivyo kwetu leo. Nabii aliandaliwa na Mungu na alitumwa na Mungu Yeremia 1:5

Onyo juu ya manabii wa uongo

Ieleweke kuwa katika kila kilicho halisi (valid) lazima kuna batili (invalid). Mungu kwa kutambua hilo alijua pia kwa kuwepo kwa manabii wake wa kweli lazima watakuwepo na manabii wa uongo na hivyo hakuacha kutuonya. 2 Petro 2:1 Lakini kuliondokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo,………. Mathayo 24:11, Na manabii wengi wa uongo watatokea, na kudanganya wengi. Kipindi cha mwisho kilitabiriwa kuwa manabii wengi wa uongo watatokea wakidanganya yumkini hata walio wateule, na hivyo imetupasa kusimama upande wa Kristo ili atuokoe na nguvu za upotevu

Tutawatambuaje?

Mathayo 7:15,16 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao…………

1 Yohana 4:1-3 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani…………. kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu………… Mungu aliyajua haya mapema wengi watatokea wakijiita wao ni manabii wakijaribu hata kutabiri mambo mengi ikiwemo habari ya kurudi kwa Yesu. Biblia imetuonya juu ya manabii hao na wala tusiwaamini hao wajiitao manabii bali tuwapime kwanza kwa maandiko, Je, wamekamilika hata katika AMRI za Mungu??? Nabii wa kweli wa Mungu hawezi kufundisha kuwa amri za Mungu hazina umuhimu, nabii wa kweli wa Mungu hawezi kutabiri kilicho kinyume na Biblia takatifu.

BWANA AKUBARIKI.

Imeandaliwa na

PETER I. JEFTER 0757916891/ 0653401497

Advertisements

One comment on “UNABII NI NINI??

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s