HERI ASOMAYE, ASIKIAYE NA KUSHIKA!!!

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Mujaya Mujaya

Simu: +255 715 678 122 au +255 768 678 122

Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: Heri Asomaye, Asikiaye na Kushika

 

“Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu. Ufunuo. 1:3

Ni nini unachoamini sana? Ambapo umeweka matumaini na mategemeo yako yote? Kama ukialikwa leo kuonana na mtu mhimu sana utafanya nini? Huenda ukachagua nguo nzuri unayoiamini sana. Kumwamini MUNGU ni jambo la msingi kwa kila mtu. Je, tunamwamini MUNGU kwa kiwango gani? Tatizo letu kubwa wanadamu hatumwamini Mungu kwa asilimia zote, mara nyingi MUNGU si tegemeo na kimbilio wakati wote, tunaona MUNGU anaweza baadhi ya mambo fulani tu na mengine hawezi. Pia watu wengi humwabudu MUNGU na wengine humtumikia lakini cha ajabu hawamwamini.

Mungu anatwambia mambo kabla hayajatokea ili yatakapotokea tumwamini, Yesu anasema katika Yohana. 13:19, “Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye.” Hivyo Mungu anatangaza mambo ya siku za usoni kabla hayajatukia ili tuyaonapo yakitimia tumwamini, Yohana. 14:29 inaongeza “Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini.” Hebu tazama Mika anatoa unabii wa kuzaliwa Yesu katika bethlehemu, Mika. 5:2 “Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliyemdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala wa Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele.” Jambo hili likatimia miaka mingi baadaye kama unabii ulivyosema, Mathayo. 2:1 inasema “Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode… kisha mfalme Herode akawaita wakuu wa makuhani wote na waandishi kuwauliza Kristo azaliwa wapi? Ndipo alipojibiwa, Mathayo. 2:5 “Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi: maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii.” Hivyo Yesu alizaliwa kama ilivyatabiriwa na nabii Mika.

Jambo hili linathibitisha imani yetu kuwa Mungu ni mkuu, na linatupatia sababu ya kumwamini MUNGU wa mbinguni.

Unabii ni taa inayotuangaza, biblia inasema katika 2 Petro. 1:19, “Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia kama taa ing’aayo katika giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.” Ili tusiwe katika giza, Mungu hutupatia unabii kwa kuwafunulia manabii siri yake, imeandikwa katika Amosi. 3:7 kuwa, “Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.” Na unabii ni imara zaidi maana hutimia sawasawa na ulivyotabiliwa nasi tunapouangalia unabii biblia inasema tunafanya vema kwani hatutakuwa gizani.

Pia kabla hatujauangalia unabii lazima tujue neno hili kwanza kwamba, unabii unatakiwa utafsiriwe si kama apendavyo mtu fulani, 2 Petro.1:20-21; 1 Wakorintho. 1:13,

Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu. Maana unabii hukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, waliongozwa na Roho Mtakatifu”. “Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni”

Unabii unapaswa kutafsiriwa kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu maana kwa kupitia Yeye(Roho Mtakatifu) ulitolewa kwa watumishi wa Mungu manabii, na kwakuwa ni mambo ya rohoni lazima yatafsiriwe kwa maneno ya rohoni. Yesu alizungumza habari za kuja Roho Mtakatifu kwa kusema, Yohana. 16:13 “Lakini atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena na mambo yajayo atawapasha habari zake.” Hapa tunaona kuwa Roho Mtakatifu ni (a) kiongozi katika kweli yote (b) ananena yote vilevile kama alivyoyasikia toka kwa Baba na (c) atapasha habari za mambo yajayo. 1 Wakorintho. 2:10, inasema pia “Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.” Sababu hizi pekee zinatuonesha kuwa, Roho Mtakatifu pekee ndiye aletaye unabii kwa manabii hivyo yeye peke yake ndiye anayetoa tafsiri yake.

Mungu ndiye anayetoa unabii na unapofikia utimilifu wa wakati jambo hilo linatokea kama lilivyotabiriwa. Pia BWANA ana uwezo wa kuona mambo ambayo wanadamu watafanya siku za usoni, hivyo hutoa wakati kamili ambapo mambo hayo yatadhihilika, na muda huo unapofika unabii unatimia. Haiwezekani unabii wa uwongo utimie kwa wakati sahihi.

Unabii huthibitika tunapoangalia historia, maana Mungu ambaye aliona mambo yatakayofanywa na wanadamu, alitoa unabii juu yao, na wanadamu wanapoingia katika utendaji na kutenda kama yalivyotabiriwa, wanahistoria wananakili mambo ya wanadamu ambayo sasa yakifananishwa na unabii yanafanana kabisa.

Na sasa mambo yote yaliyopita katika historia na tunayoona yanaendelea kutendeka yapo katika unabii usiokosewa. Unaweza kujua wapi ulipotoka, wapi ulipo na wapi unapokwenda kwa kuutazama unabii wa biblia jinsi ulivyo na unavyodhihilika kabisa kwa uhakika katika historia. Unabii hutuwezesha kujua matukio ambayo yatatokea mbeleni na kuthibitisha imani yetu kwa Mungu pamoja na kuongeza imani yetu kwa MUNGU aliyeona mambo hayo yakitendeka; na kwa kupitia Roho wake akawavuvia manabii wakaandika katika vyuo(vitabu). Pia kutimia kwa unabii, utupatia uthibitisho wa ukweli wa NENO la Mungu ambamo umeandikwa.

Shetani hapendi kabisa watu wachunguze unabii, maana watajua hatma ya yale anayowaongoza kutenda na hivyo watamkataa na watamkimbia. Shetani huwafanya wajione wametingwa na kazi, huwapatia uchovu au hata usingizi na pengine kuweka jambo au kitu chochote ambacho kitatoa usikivu wao kwa neno la Mungu ili waokolewe. Wengine waliopata fursa ya kuujua unabii na kuona ukithibitika wazi katika historia, shetani anawaongoza wapuuzie ile neema ya Yesu iokowayo na maonyo waliyopata kutoka katika unabii. Haitatosha kujua unabii tu, kama hautaongeza uhusiano wako na MUNGU, na kukusogeza hadi kwenye msalaba wa Yesu ili uungame dhambi zote na kutokuamini, kutubu kwa dhati ili uhesabiwe haki kwa imani. Biblia inasema katika, Ufunuo. 1:3 “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.Hivyo heri si kwa anayeishia kusoma na kusikia unabii tu, bali kwa Yule anayeyashika yaliyoandikwa katika unabii. Tuna heri ndugu mpendwa kama tutatenga muda kusoma, kusikiliza na kushika maneno ya unabii.

 

Kwa maswali, Maoni au Ushauri usisite kuwasiliana nasi au kanisa lolote la waadventista wa Sabato lililo karibu nawe.

Advertisements

2 comments on “HERI ASOMAYE, ASIKIAYE NA KUSHIKA!!!

 1. Be blessed

  ShareHope Ministries wrote:

  >Post : HERI ASOMAYE, ASIKIAYE NA KUSHIKA!!! >URL : https://sharehopeministries.wordpress.com/2015/10/04/heri-asomaye-asikiaye-na-kushika/ >Posted : October 4, 2015 at 17:05 >Author : ShareHope Ministries >Categories : Bible Studies > >Imeandaliwa na : Muinjilisti: Mujaya Mujaya Simu: +255 715 678 122 au +255 768 678 122 Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com Downloadable Version: Heri Asomaye, Asikiaye na Kushika   “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo; kwa maana wakati u karibu.” Ufunuo. 1:3 Ni nini unachoamini sana? Ambapo umeweka matumaini na […] > >Read more of this post ( https://sharehopeministries.wordpress.com/2015/10/04/heri-asomaye-asikiaye-na-kushika/ ) > >Add a comment to this post: https://sharehopeministries.wordpress.com/2015/10/04/heri-asomaye-asikiaye-na-kushika/#respond > >– >WordPress.com | Thanks for flying with WordPress! > >Manage Subscriptions >https://subscribe.wordpress.com/?key=38017bb1269015908ba5f0ffb35ea7e3&email=mossesjohn.mj%40gmail.com > >Unsubscribe: >https://subscribe.wordpress.com/?key=38017bb1269015908ba5f0ffb35ea7e3&email=mossesjohn.mj%40gmail.com&b=acugxMH1J18.KK%5BS_%3Fe7D.%7CtX_MnYYjlOMz0s%2BC%3DTe37guJcvw >

  a:hover { color: red; } a { text-decoration: none; color: #0088cc; } a.primaryactionlink:link, a.primaryactionlink:visited { background-color: #2585B2; color: #fff; } a.primaryactionlink:hover, a.primaryactionlink:active { background-color: #11729E !important; color: #fff !important; }

  /* @media only screen and (max-device-width: 480px) { .post { min-width: 700px !important; } } */ WordPress.com

  ShareHope Ministries posted: ”

  Imeandaliwa na :

  Muinjilisti: Mujaya Mujaya

  Simu: +255 715 678 122 au +255 768 678 122

  Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

  Downloadable Version: Heri Asomaye, Asikiaye na Kushika

   

  “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashik”

  Like

 2. I was just looking at your HERI ASOMAYE, ASIKIAYE NA KUSHIKA!!! | ShareHope Ministries website and see that your website has the potential to become very popular. I just want to tell you, In case you don’t already know… There is a website network which already has more than 16 million users, and most of the users are looking for websites like yours. By getting your website on this network you have a chance to get your site more popular than you can imagine. It is free to sign up and you can read more about it here: http://likes.avanimisra.com/4owu – Now, let me ask you… Do you need your website to be successful to maintain your business? Do you need targeted visitors who are interested in the services and products you offer? Are looking for exposure, to increase sales, and to quickly develop awareness for your site? If your answer is YES, you can achieve these things only if you get your site on the service I am talking about. This traffic service advertises you to thousands, while also giving you a chance to test the service before paying anything at all. All the popular sites are using this service to boost their readership and ad revenue! Why aren’t you? And what is better than traffic? It’s recurring traffic! That’s how running a successful website works… Here’s to your success! Read more here: http://labviewni.com/news/5j8

  Like

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s