CHUKIZO LA UHARIBIFU (The abomination of desolation)

Ev. Peter Jeftah

Ev. Peter Jeftah

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Peter I. Jefter

Simu: 0757916891/ 0653401497

Downloadable Version: CHUKIZO LA UHARIBIFU

Mathayo 24:15, Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Daniel, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu).

Sura ya 24 ya kitabu cha Mathayo (Mathayo 24) ni sura maarufu na maalum kwa matukio au dalili (ishara) za kurudi kwa Kristo. Yesu akiwa na wanafunzi wake akiwafundisha kuhusu ishara za marejeo yake hakuwaficha pia juu ya chukizo la uharibifu.

Lakini Je, chukizo la uharibifu ni nini??

Katika kipindi cha wana wa Israeli zamani hizo kitu chochote kilichokuwa kinyume na sheria za wayahudi au kilikuwa tofauti na ibada zao kilikuwa ni chukizo kwao. Kwa mfano kushikamana na wamataifa (wasiotahiriwa) ilikuwa ni chukizo kwa kuwa waliku najisi.

Tangu Misri Bwana hakuruhusu huduma zake takatifu zifanyike huko kwakuwa wamisri waliabudu miungu mingine. Huduma zozote za kiibada zilizofanywa kinyume na ibada takatifu yalikuwa ni machukizo. Kutoka 8:26, Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwakuwa tutamchinjia sadaka BWANA, Mungu wetu na hayo machukizo ya Wamisri; Je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe. Soma pia mwanzo 42:32 na 46:34. Wamisri na Waebrania kuchangamana ilikuwa ni machukizo.

Katika kipindi cha utawala wa Sulemani Je? Kitendo cha Sulemani kuoa wanawake wengi pia kilikuwa ni machukizo kwa MUNGU 1Wafalme 11:5- 7 Kwakuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, Mungu mke wa wasidoni na Milkomu, chukizo la waamoni Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea Komeshi, chukizo la wamoabu, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu na Moleki, chukizo la wana wa Amon. Soma pia 2Wafalme 23:13

Baada ya kuona maana ya chukizo. Turejee katika fungu letu la mathayo 24:15. Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Daniel ni nini?? Na nini ishara zake?

Daniel 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka ya dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo hata ukomo, na gadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

Mafungu haya ni muendelezo wa mafungu ya nyuma yakizungumzia juu ya unabii wa majuma 70 yaliyotabiriwa juu ya wayahudi na huduma ya YESU na kukataliwa kwa injili ndani ya uyahudi kisha kutoa nafasi kwa wamataifa kusikia injili.

Katika tafsiri ya majuma 70 tumeona ilianza mwaka wa 457 K.K na kuishia mwaka wa 34 A.D. juma moja la mwisho ambalo Yesu anaweka agano thabiti na watu wengi huanzia mwaka wa 27 A.D ambapo YESU alianza huduma yake duniani nayo huishia mwaka wa 34 A.D kukataliwa kwa injili na kuuawa kwa Stephano (matendo 7:54-60) ambapo nusu ya juma hilo. (kwakuwa juma lina siku 7 nusu yake itakuwa ni 31/2) huanza mwaka wa 27 A.D Kristo anapoanza huduma yake hadi 301/2 A.D anapokatiliwa na kuuawa. Nayo nusu nyingine huanza 301/2 A.D injili kwa wayahudi kwanza hadi 34 A.D wanaikataa injili na kuwaua watumishi wa MUNGU kisha mlango wa injili kwa wamataifa inafunguliwa.

Baada ya hayo ndipo litakaposimama chukizo la uharibifu, hii humaaisha kuwa baada ya huduma ya Yesu kukataliwa nao wayahudi pia kuikataa injili badala yake litasimama uharibifu mkubwa na machukizo mengi. Daniel 11:31 na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu hapa Biblia hutuambia juu ya pembe ndogo iliyoinuka katika (Daniel 8:9.) ambayo katika Daniel 8:11 Naam ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa.

(patakatifu palipoangushwa hapa ni hekalu la Yerusalemu liliangushwa na utawala wa kirumi katika mwaka wa 70 A.D Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Yesu alitabiri juu ya anguko la Yerusalemu katika Mathayo 24:2……. Amin nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa

Daniel 12:11 Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itakapoondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na sitini. (siku elfu mia mbili na sitini sawa na miaka 1260 huanza 538-1798 kuinuka kwa upapa hadi kutiwa kwake jeraha la mauti, Dan 7:25, Ufunuo 13:3).

Yesu anazungumzia anguko la mji wa Yerusalemu kama chukizo la uharibifu. Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Kubomolewa kwa hekalu la Yerusalemu mnamo mwaka 70A.D huashiria mwisho wa taifa la Israeli na ambapo wengi wao walikimbilia katika mataifa mengine, wengine walichukuliwa mateka. Baada ya kipindi hicho ndipo ukainuka utawala wa upapa ulioleta mafundisho ya uongo na kutengua sheria za MUNGU na kulazimisha watu kuyashika yaliyo kinyume na kweli nacho kilikuwa kipindi kilichoitwa zama za giza ambacho kilidumu kwa miaka 1260……….

Chukizo la uharibifu unafananishwa na kipindi kinachokuja mbele yetu, atakaposimama Yule mharibifu mpinga Kristo. 2 Wathesalonike 2:1-4 Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitishwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo, Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa kwanza YULE MTU WA KUASI, MWANA WA UHARIBIFU………..akijionesha nafsi yake ya kwamba yeye ni Mungu.

Atakapo simama Yule mpinga kristo na kuhalallisha mafundisho ya uongo (angalia fungu la 9), pale sabato bandia itakapochukua nafasi ya Sabato halisi (Jumapili kuchukua nafasi ya Jumamosi) haya yote yatakuwa ni machukizo mbele za Mungu.

Ahadi ya MUNGU kwako.

Ufunuo 3:10 kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi name nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwenguwote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

BWANA AKUBARIKI.

Imeandaliwa na

PETER I. JEFTER 0757916891/ 0653401497

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s