TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTIMIZA MWAKA MMOJA WA HUDUMA!!!

ShareHope Ministries tunayofuraha kubwa sana kwa kutimiza mwaka mmoja wa huduma. Mungu amekuwa mwema sana kwetu kwa hatua aliyotufikisha hasa kwa wanufaika wa huduma yetu. Tunaomba mzidi kutuombea, kutushauri na kutuunga mkono.

Kupata taarifa ya utendaji kazi ingia hapa: TAARIFA YA SHAREHOPE MWAKA MMOJA WA KAZI

Haya ni baadhi ya matukio tu yaliyofanyika:

Muinjilisti John Mafuru akiwa katika huduma kwa jamii

Muinjilisti John Mafuru akiwa katika huduma kwa jamii

Mkurugenzi mkuu wa SHM, Muinjilisti Basilio Maliwanga akiwa katika huduma kwa jamii

Mkurugenzi mkuu wa SHM, Muinjilisti Basilio Maliwanga akiwa katika huduma kwa jamii

Mkurugenzi mkuu wa ShareHope, Ev. Basilio Maliwanga akiwa katika kazi za kujitolea za huduma kwa jamii.

Mkurugenzi mkuu wa ShareHope, Ev. Basilio Maliwanga akiwa katika kazi za kujitolea za huduma kwa jamii.

Mkurugenzi Mkuu wa ShareHope akifundisha darasa maalumu la watoto wakati ShareHope ikiendesha mkutano wa ATF(Almost Time To Fly) katika kijiji cha Peko Misegese.

Mkurugenzi Mkuu wa ShareHope akifundisha darasa maalumu la watoto wakati ShareHope ikiendesha mkutano wa ATF(Almost Time To Fly) katika kijiji cha Peko Misegese.

Timu ya wahudumu kutoka ShareHope Ministries wakiwa tayari kuelekea Peko Misegese kwajili ya Mkutano wa Injili ATF. Kuanzia kulia ni Ev. John Mafuru, Peter Jefta na Janeth Christopher.

Timu ya wahudumu kutoka ShareHope Ministries wakiwa tayari kuelekea Peko Misegese kwajili ya Mkutano wa Injili ATF. Kuanzia kulia ni Ev. John Mafuru, Peter Jefta na Janeth Christopher.

Waasisi wa SHM

Waasisi wa SHM

Baadhi ya wahudumu wa ShareHope Ministries baada ya kikao cha ughaguzi

Waumini wa kundi la Peko Misegese na Mongwe wakiwa katika ibada ya pamoja miezi miwili baada ya kuasisiwa kwa kundi la Mongwe.

Waumini wa kundi la Peko Misegese na Mongwe wakiwa katika ibada ya pamoja miezi miwili baada ya kuasisiwa kwa kundi la Mongwe.

Muinjilisti Basilio Maliwanga akitoa Neno La Uzima kwa waumini wa kundi la Peko na Mongwe katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika kundi la Peko Misegese.

Muinjilisti Basilio Maliwanga akitoa Neno La Uzima kwa waumini wa kundi la Peko na Mongwe katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika kundi la Peko Misegese.

Wahudumu wa ShareHope wakitoa huduma ya uimbaji kanisa la Mlali

Wahudumu wa ShareHope wakitoa huduma ya uimbaji kanisa la Mlali

Baadhi ya wahudumu wa ShareHope Ministries baada ya huduma maalumu ya utambulisho wa kikundi kwa TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe

Baadhi ya wahudumu wa ShareHope Ministries baada ya huduma maalumu ya utambulisho wa kikundi kwa TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe

IMG_20150531_161926

Mkurugenzi wa ShareHope Ministries akihutubia wanakundi wa Peko Misegese

Mkurugenzi wa ShareHope Ministries akihutubia wanakundi wa Peko Misegese

Baadhi ya Viongozi wa ShareHope Ministries baada ya kutembelea wagonjwa, kuanzia kulia ni Mkurugenzi wa Uinjilisti na Mikutano ya Injili Ndg. Musa Daudi Mwakisya; Mhazini Ms. Rebecca Mchome; Mkurugenzi wa Mawasiliano Ndg. Mujaya Mujaya na Mkaguzi wa Hesabu wa Ndani Ndg. John Mafuru.

Washiriki wa kundi la Mongwe Kariakoo wakijifunza neno la uzima lililotolewa kupitia Ev. Daniel Kitigani

Washiriki wa kundi la Mongwe Kariakoo wakijifunza neno la uzima lililotolewa kupitia Ev. Daniel Kitigani

Kwaya ya muungano kati ya kundi la Peko Misegese na Mongwe Kariakoo ikiimba wimbo wa kumkaribisha Mhudumu mkuu wakati wa ibada

Kwaya ya muungano kati ya kundi la Peko Misegese na Mongwe Kariakoo ikiimba wimbo wa kumkaribisha Mhudumu mkuu wakati wa ibada

Wajumbe wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa katika kikao cha mipango ya kazi.

Wajumbe wakisikiliza hoja mbalimbali zilizotolewa katika kikao cha mipango ya kazi.

Mhazini wa ShareHope Ministries, Ms. Rebecca Mchome (kulia) akisikiliza kwa makini wakati kikao kikiendelea. Pembeni yake ni mwanachama mpya aliyepokelewa Ms. Winnie Makoye

Mhazini wa ShareHope Ministries, Ms. Rebecca Mchome (kulia) akisikiliza kwa makini wakati kikao kikiendelea. Pembeni yake ni mwanachama mpya aliyepokelewa Ms. Winnie Makoye

Wanachama wa ShareHope Ministries wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wakati wa kikao hicho makini.

Wanachama wa ShareHope Ministries wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wakati wa kikao hicho makini.

Wajumbe wa kikao wakisikiliza kwa makini agenda zikiwakilishwa

Wajumbe wa kikao wakisikiliza kwa makini agenda zikiwakilishwa

Mhazini wa ShareHope Ministries Ms. Rebecca Mchome akikabidhi baadhi ya mahitaji kwa mama mlezi wa mtoto kwa niaba ya ShareHope Ministries kama pole na faraja kwa mgonjwa na wauguzaji.

Mhazini wa ShareHope Ministries Ms. Rebecca Mchome akikabidhi baadhi ya mahitaji kwa mama mlezi wa mtoto kwa niaba ya ShareHope Ministries kama pole na faraja kwa mgonjwa na wauguzaji.

Ndg. Werema Rwabuhanga (katikati) akitoa Neno fupi la faraja kwa mgonjwa. Kulia ni Mzee kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya Ndg. Benatus Muyenjwa.

Ndg. Werema Rwabuhanga (katikati) akitoa Neno fupi la faraja kwa mgonjwa. Kulia ni Mzee kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya Ndg. Benatus Muyenjwa.

Mzee Kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya alitoa maelekezo ya namna ambavyo huduma zitakavyotolewa.

Mzee Kiongozi wa Kanisa la Mlali Peya Peya alitoa maelekezo ya namna ambavyo huduma zitakavyotolewa.

Jengo kuu la Kituo cha Afya Mlali

Jengo kuu la Kituo cha Afya Mlali

Semina kubwa ya Neno la Mungu kwa njia ya Mtandao ilifanyika ikiongozwa na Dr. Edward Mhina kutoka IMTU.

Semina kubwa ya Neno la Mungu kwa njia ya Mtandao ilifanyika ikiongozwa na Dr. Edward Mhina kutoka IMTU.

Ndg. Steven Wilson akitoa semina ya mahusiano

Ndg. Steven Wilson akitoa semina ya mahusiano

Mzee wa Kanisa la Mbeya Mjini SDA, Dr. Mkeni (Aliyevalia koti la suti). Akitoa semina kwa vijana ambao wapo katika ndoa wakati walipokuwa katika matembezi ya mafunzo wilayani Rungwe katika mkoa wa Mbeya.

Katibu wa AY na Mwalimu wa kwaya ya Vijana Mbeya Mjini SDA Ndg. Hezbon Sengere akiwa pamoja na Ndg. Vitus Chalo na Mujaya Mujaya, juu ya daraja la Mungu

Katibu wa AY na Mwalimu wa kwaya ya Vijana Mbeya Mjini SDA Ndg. Hezbon Sengere akiwa pamoja na Ndg. Vitus Chalo na Mujaya Mujaya, juu ya daraja la Mungu

Mkurugenzi wa Mawasiliano na TEHAMA wa ShareHope Ministries akiwa na Mwenyekiti wa chama cha AY Mbeya Mjini SDA, Master Guide Ndg. Steven Wilson

Mkurugenzi wa Mawasiliano na TEHAMA wa ShareHope Ministries akiwa na Mwenyekiti wa chama cha AY Mbeya Mjini SDA, Master Guide Ndg. Steven Wilson

Muinjilisti Mujaya Mujaya katika mti wa mparachichi ambao kwa mujibu wa wenyeji una maajabu yake pia.

Muinjilisti Mujaya Mujaya katika mti wa mparachichi ambao kwa mujibu wa wenyeji una maajabu yake pia.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na TEHAMA toka ShareHope Ministries akimhoji mwenyeji mwelekezi juu ya maajabu ya Kijungu na nini hufanya iwe ni sehemu ya pekee.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na TEHAMA toka ShareHope Ministries akimhoji mwenyeji mwelekezi juu ya maajabu ya Kijungu na nini hufanya iwe ni sehemu ya pekee.

Mzee Eliya Kalyenge (88) ndiye alikuwa mwelekezaji wa vijana kuhusu historia na maajabu ya Kijungu. Miongoni mwa maajabu ni Kijungu kutoa mwanga mkali unaong'aa wakati wa usiku pia inasemekana kwa mujibu wa Mzee Kalyenge, mwanga huo unatokana na nyoka wa asili mwenye vichwa 12 aliyepo katika eneo hilo.

Mzee Eliya Kalyenge (88) ndiye alikuwa mwelekezaji wa vijana kuhusu historia na maajabu ya Kijungu. Miongoni mwa maajabu ni Kijungu kutoa mwanga mkali unaong’aa wakati wa usiku pia inasemekana kwa mujibu wa Mzee Kalyenge, mwanga huo unatokana na nyoka wa asili mwenye vichwa 12 aliyepo katika eneo hilo.

Muinjilisti Mujaya Mujaya akifurahia maajabu ya Mungu kwa kupiga picha mbele ya kijungu.

Muinjilisti Mujaya Mujaya akifurahia maajabu ya Mungu kwa kupiga picha mbele ya kijungu.

Karibu Kijungu

Karibu Kijungu

Baadhi ya wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari ya wasichana ya Loleza wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa kanisa la Mbeya Mjini mara baada ya Ibada ya pekee sana iliyofanyika Tar. 22/11/2014 nakushuhudia wasichana 15  miongoni mwao wakipokea ubatizo.

Wanafunzi wa LOLEZA wakiwa katika picha ya pamoja.

Wanafunzi wa LOLEZA wakiwa katika picha ya pamoja.

Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika ibada iliyofanyika Makumira University mbeya campus.

Mamia ya wanafunzi wa vyuo vikuu katika ibada iliyofanyika Makumira University mbeya campus.

Wanasemina kutoka Iringa Zone katika picha ya pamoja, kulia kabisa ni Ev. Mujaya Mujaya

Wanasemina kutoka Iringa Zone katika picha ya pamoja, kulia kabisa ni Ev. Mujaya Mujaya

Mjadala wa makundi ukiendelea

Mjadala wa makundi ukiendelea

Wanasemina wakijadiliana maswali ya mjadala ili kupima uelewa wa kila mmoja na uwezo wao wa kusaidiana katika kazi ya Mungu

Wanasemina wakijadiliana maswali ya mjadala ili kupima uelewa wa kila mmoja na uwezo wao wa kusaidiana katika kazi ya Mungu

Ev. Mujaya Mujaya akiteta jambo pamoja na Mhazini na Mkaguzi wa fedha wa TUCASA SHC baada ya Semina

Ev. Mujaya Mujaya akiteta jambo pamoja na Mhazini na Mkaguzi wa fedha wa TUCASA SHC baada ya Semina

Ev. Mujaya Mujaya akiendesha semina za wahazini Iringa zone

Ev. Mujaya Mujaya akiendesha semina za wahazini Iringa zone

Wanasemina wakisikiliza kwa makini sana mafunzo muhimu kwa ufanikishaji wa ukusanyaji na utunzaji wa hazina ya Bwana

Wanasemina wakisikiliza kwa makini sana mafunzo muhimu kwa ufanikishaji wa ukusanyaji na utunzaji wa hazina ya Bwana

Wanasemina walipata nafasi ya kufanya mazoezi ili  kujipima uelewa wao kwa mafunzo waliyoyapokea

Wanasemina walipata nafasi ya kufanya mazoezi ili kujipima uelewa wao kwa mafunzo waliyoyapokea

Wahazini kutoka Tucasa kanda  ya Mbeya wakati walipokuwa katika semina za Wahazini na Wakaguzi wa fedha zilizofanyika Chuo kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST). Kulia kabisa ni Mhazini wa SHC Ndg. Giliad Godson na Mwezeshaji wa semina Ev. Mujaya Mujaya.

Washiriki wa kundi la Peko Misegese wakiwa na Miunjilisti Mujaya Mujaya baada ya kuendesha juma la uamsho kwa juma moja

Washiriki wa kundi la Peko Misegese wakiwa na Miunjilisti Mujaya Mujaya baada ya kuendesha juma la uamsho kwa juma moja

IMG_20140712_120450 IMG_20140710_141005

Wanafunzi wakipokea zawadi zao baada ya kutembelewa na SHM shuleni Misegese Primary

Wanafunzi wakipokea zawadi zao baada ya kutembelewa na SHM shuleni Misegese Primary

Wanafunzi wa Misegese Primary wakifatilia huduma ya SHM

Wanafunzi wa Misegese Primary wakifatilia huduma ya SHM

IMG_20140710_124443 IMG_20140710_120336 IMG_20140708_124303 IMG_20140711_181333

Muinjilisti Mujaya Mujaya akiendesha semina ya mapishi ya kikristo

Muinjilisti Mujaya Mujaya akiendesha semina ya mapishi ya kikristo

IMG_20140711_163720 IMG_20140711_163449

Semina ya ujasiriamali: Unaweza Ukajua Faida Halisi ya Mradi Wako

Semina ya ujasiriamali: Unaweza Ukajua Faida Halisi ya Mradi Wako

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in News

UNABII WA MIAKA 2300

Ev. Peter Jeftah

Ev. Peter Jeftah

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Peter I. Jefter

Simu: 0757916891/ 0653401497

Downloadable Version: Unabii wa Miaka 2300

Daniel 8:13, 14…. 13, Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? 14, Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Ni katika kipindi cha utawala wa Belshaza mfalme wa Babeli mwana wa mfalme Nebukadneza (Daniel 5:2) ndipo Daniel anaoneshwa maono haya Daniel 8:1 Katika mwaka wa tatu wa kumiliki kwake mfalme Belshaza maono yalinitokea mimi, naam, mimi Danieli, baada ya yaliyonitokeahapo kwanza. Akiwa katika wilaya ya Elimu, shushani ngomeni katika mto ulai huko Babeli

Mwanzo wa njozi ya Danieli anaoneshwa kondoo mwenye pembe mbili akisimama na kutawala dunia akisukuma upande wa magharibi na kaskazini na kusini (Daniel 8:3, 4). Kisha anaona beberu akiinuka upande wa mashariki akiwa na pembe mashuhuri kati ya macho (Daniel 8:5). (kwa faida ya msomaji pembe katika unabii huwakilisha ufalme au utawala). Akamkaribia Yule kondoo akamkasirikia kwa ghadhabu nyingi naye akampiga hata kuvunja pembe zake, akamwangusha chini hata kumkanyaga-kanyaga

Baadaye ile pembe ikavunjika kwa kujitukuza hata zikatokea pembe nne zikaielekea pepo nne za mbingu nazo zikatwala kwa kipindi Fulani (Daniel 8:8). Daniel 8:9 Na katika moja ya hizo pembe ilitokea pembe ndogo, iliyokuwa sana, upande wa kusini, na upande wa magharibina upande wan chi ya uzuri. Pia katika fungu la 23; Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosao watakapotimia, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo………atasimama. Hii humaaniasha wakati wa mwisho wa utawala wa falme nne zilizoinuka kutoka kwa Yule beberu ndipo utainuka tena ufalme mwingine unaowakilishwa na pembe ndogo, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo.

Daniel 8:10-14 Nayo ikakua, kiasi cha kulifikilia jeshi la mbinguni ; ikaangusha chini baadhi ya jeshi lile, na nyota ikazikanyaga. Naam ikajitukuza hata juu ya aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa chini. Na jeshi likatolewa kwake pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya daima, kwa sababu ya makosa; nayo ikaangusha kweli hata chini; ikatenda ilivyopenda, na kufanikiwa. Ndipo niamsikia mtakatifu mmoja akinena na mtakatifu mwingine akamuuliza huyo aliyenena, Haya maono katika habari sadaka ya kuteketezwa ya daima, na lile kosa lifanyalo ukiwa, yataendelea hata lin, kukanyagisha patakatifu na jeshi? Akamwambia, Hata nyakati za jioni asubuhi elfu mbili na mia tatu; ndipo patakatifu patakapotakaswa.

Kuinuka kwa pembe hii ndogo na matendo yake ndiko kunamhuzunisha mtakatifu mmoja na hivyo inampelekea kutaka kujua hatima ya haya yote. Nayo ni nyakati za jioni na asubuhi elfu mbili na mia tatu (2300).

Nini tafsiri yake miaka hii 2300??

Katika sura ya Daniel 8:14 tunaambiwa matukio haya yatachukua muda nyakati za jioni na asubuhi 2300 lakini hatuambiwi chochote kuhusu mwanzo wala mwisho wake.

Katika kuelewa tafsiri hii lazima tuelewe mambo yafuatayo.

  1. nyakati za jioni na asubuhi ni sawa na siku nzima amabyo pia huanza jioni hata jioni. Mwanzo 1:5………… ikawa jioni ikawa asubuhi, siku moja. kwahiyo nyakati za jioni na asubuhi 2300 ni sawa na siku kamili 2300
  2. Katika unabii siku moja ni sawa na mwaka mmoja Ezekiel 4:6………siku arobaini, siku moja kwa mwaka mmoja, nimekuagiza kwahiyo siku 2300 za kiunabii ni sawa na miaka iliyokamilika 2300.. Hivyo tunasema ili haya yote yafikie mwisho ni mpaka kukamilika kwa miaka 2300.
  3. Unabii wa miaka 2300 ndio unabii mrefu kwenye biblia kuliko mengine yote, hivyo unabii mwingine kama vile miaka 1260, majuma 70, miaka 1335 na 1290 zote huangukia kwenye miaka 2300.

Mwanzo wa miaka hii ni upi?

Mwanzo wa miaka hii tunaelewa kwa kuelewa mianzo ya majuma 70 katika Daniel 9:24. Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu………,25 Basi ujue na kufahamu, ya kuwa tangu kuwekwa amri ya kutengeneza na kujenga upya mji wa Yerusalemu….. kutakuwa na majuma saba………….

Majuma sabini ni sawa na miaka 490. 70×7=490. Hii hutuambia kuwa kulikuwa na miaka 490 ulioamriwa juu ya taifa la Israeli.

Amri juu ya ujenzi wa mji wa yerusalemu ulitolewa na mfalme Artashasta mfalme wa uajemi mnamo mwaka wa 457 K.K (kabla ya kristo) Ezra 7:21-26 Na mimi, naam mimi, mfalme Artashasta, nawapa amri wote wenye kutunza hazina…..hata kiasi cha cha talanta mia za fedha …. kila neon litakaloamriwa na Mungu wa mbinguni, na litendeke halisi kwa ajili ya ya nyumba ya Mungu wa mbinguni…….. Kuanzia mwaka wa 457 hitimisho la miaka 490 au majuma 70 hufikia 34 B.K (baada ya Kristo), (kumbuka kuna mwaka kutoka 0-1)….katika miaka 2300 baada ya kukamilika kwa miaka 490 tunasalia na miaka 1810.

490+1810=2300.na

Siku 2300 zilioneka kuanza wakati amri ya Artashasta kwa ajili ya urejeshwaji wa na ujenzi wa Yerusalemu ilipotolewa majira ya kipupwe ya mwaka 457 K.K. Kwahiyo mwanzo wa miaka 2300 ni mwaka 457 B.K na huishia mwaka 1844 B.K.

Bwana atubariki tukutane sehemu ya pili kujifunza matukio makubwa yaliyotabiriwa na kutokea katika kipindi hiki cha miaka 2300.

Imeandaliwa na

PETER I. JEFTER 0757916891/ 0653401497

THAMANI YA MWANADAMU KWA MUNGU

IMG_20150830_174425Na. Muinjilisti: John Mafuru Musibha

Simu Na.        +255 652 045 317

+255 764 736 335

Downloadable Version: THAMANI YA MWANADAMU KWA MUNGU

Ndugu msomaji wa mada mbalimbali katika blog ya ShareHope Ministries ni wasaa mwingine tena ambapo tunaendelea kukuletea mada mbalimbali za kumtukuza Mungu wetu wa mbinguni pia kujifunza ukuu wake katika maisha ya mwanadamu. Siku hii ya leo nimewiwa kukuletea mada hii ambayo tutajifunza thamani ya wanadamu kwa Mungu wetu wa Mbinguni.

Mpenzi msomaji somo hili linaturudisha nyuma mpaka kipindi cha uumbaji, Mwanzo 1:26 inasema, “Mungu akasema, na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu, wakatawale samaki wa baharini, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi” katika aya hii tunagundua ya kwamba katika uumbaji wote, mwanadamu alithaminiwa sana kwa maana Mungu muumbaji alisema na “tumfanye mtu kwa mfano wetu,” ni thamani kubwa sana kuumbwa tena tukiwa tunamfanana Mungu wetu wa mbinguni, na jambo la pili ni kwamba alitupa mamlaka juu ya kila kitu alichokiumba kilichopo ardhini na majini. Tumepewa mamlaka ya kutawala viumbe vyote ambavyo Mungu ameviumba hivyo ni thamani iliyokubwa sana.

Mfano wa mamlaka aliyopewa mwanadamu yanapatikana katika kitabu cha Mwanzo 2:19-20 Mungu aliwaleta viumbe vyote alivyoviumba mbele ya Adamu ili aweze kuwapa majina na mpaka leo majina tunayoyatumia Adamu ndiye aliyewapa. Mfano chukulia katika familia yenu nyumbani, wazazi wako wanakupa mamlaka ya kutawala miradi yao yote na baadhi ya vitu muhimu, je utajiskiaje? Je ni thamani kubwa kiasi gani kwako? Jaribu kuelezea kwenye kipande cha karatasi kama umepitia uzoefu huo.

Katika kitabu kiitwacho Zaburi 8:4Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie”? mtunga Zaburi anaumuuliza Mungu je binadamu ni nani hata umkumbuke baada ya kuangalia ukuu wake na jinsi alivyoumba vitu vingi leo hii anamkumbuka mwanadamu na anaamua kumuokoa, hii yote ni thamani ya mwanadamu kwa Mungu, 5.Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu, Umemvika taji ya utukufu na heshima; fungu hili linaonesha katika uumbaji akitoka Mungu anaefatia mwanadamu. Mpenzi msomaji Malaika waliumbwa kama wajumbe kati ya mwanadamu na Mungu wetu.6. Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake 7.Kondoo na ng’ombe wote pia;Naam, na wanyama wa kondeni; 8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini;Na kila kipitacho njia za baharini. Aya ya 6 mpaka ya 8, linatukumbusha kile ambacho Mungu alikisema katika kitabu cha Mwanzo kwamba, baada ya kumuumba mwanadamu alimpatia mamlaka ya kutawala kazi zote za mikono ya Mungu yaani viumbe vyote alivyoviumba.

Ndugu msomaji, thamani ya mwanadamu ni kubwa sana mbele za Mungu na ndio maana Mungu wetu wa mbinguni akaandaa mkakati wa kutuokoa ili baade tuje tuishi kama ambavyo Mungu wetu wa Mbinguni alivyopanga mwanadamu aishi. Wito wangu na wito wetu kwetu leo hii katika kipindi hiki cha mwisho ni kuurudisha uthamani ambao tunao mbele za Mungu. Tuchague kuishi maisha matakatifu yasiyo na mawaa. Mungu wetu anatukumbuka na atatusamehe na kuwa na mahusiano mazuri na sisi kwa sababu huwa yupo karibu na mwanadamu siku zote. Panga kuurudisha uthamani huu mbele za Mungu. Roho wa Mungu atakusaidia katika maamuzi hayo, usipange kukosa ufalme wa Mungu ajapo mara ya pili kutuchukua. Usisite na wala usiangalie mtu fulani, fanya maamuzi sahihi sasa wakati bado ungalipo kwa maana zitakuja nyakati ambazo hutaweza kupata nafasi kabisa. Wasiliana na kanisa la waadventista wasabato lililopo karibu nawe ili uweze kupata mafundisho zaidi kuhusu wokovu na biblia kiujumla.

Kwa maswali, maoni au ushauri;

Tafadhali wasiliana nami kupitia;

Simu Na.        +255 652 045 317

+255 764 736 335

CHUKIZO LA UHARIBIFU (The abomination of desolation)

Ev. Peter Jeftah

Ev. Peter Jeftah

Imeandaliwa na :

Muinjilisti: Peter I. Jefter

Simu: 0757916891/ 0653401497

Downloadable Version: CHUKIZO LA UHARIBIFU

Mathayo 24:15, Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Daniel, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu).

Sura ya 24 ya kitabu cha Mathayo (Mathayo 24) ni sura maarufu na maalum kwa matukio au dalili (ishara) za kurudi kwa Kristo. Yesu akiwa na wanafunzi wake akiwafundisha kuhusu ishara za marejeo yake hakuwaficha pia juu ya chukizo la uharibifu.

Lakini Je, chukizo la uharibifu ni nini??

Katika kipindi cha wana wa Israeli zamani hizo kitu chochote kilichokuwa kinyume na sheria za wayahudi au kilikuwa tofauti na ibada zao kilikuwa ni chukizo kwao. Kwa mfano kushikamana na wamataifa (wasiotahiriwa) ilikuwa ni chukizo kwa kuwa waliku najisi.

Tangu Misri Bwana hakuruhusu huduma zake takatifu zifanyike huko kwakuwa wamisri waliabudu miungu mingine. Huduma zozote za kiibada zilizofanywa kinyume na ibada takatifu yalikuwa ni machukizo. Kutoka 8:26, Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwakuwa tutamchinjia sadaka BWANA, Mungu wetu na hayo machukizo ya Wamisri; Je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe. Soma pia mwanzo 42:32 na 46:34. Wamisri na Waebrania kuchangamana ilikuwa ni machukizo.

Katika kipindi cha utawala wa Sulemani Je? Kitendo cha Sulemani kuoa wanawake wengi pia kilikuwa ni machukizo kwa MUNGU 1Wafalme 11:5- 7 Kwakuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, Mungu mke wa wasidoni na Milkomu, chukizo la waamoni Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa BWANA, wala hakumfuata BWANA kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. Sulemani akamjengea Komeshi, chukizo la wamoabu, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu na Moleki, chukizo la wana wa Amon. Soma pia 2Wafalme 23:13

Baada ya kuona maana ya chukizo. Turejee katika fungu letu la mathayo 24:15. Chukizo la uharibifu lililonenwa na nabii Daniel ni nini?? Na nini ishara zake?

Daniel 9:27 Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka ya dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo hata ukomo, na gadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake mwenye kuharibu.

Mafungu haya ni muendelezo wa mafungu ya nyuma yakizungumzia juu ya unabii wa majuma 70 yaliyotabiriwa juu ya wayahudi na huduma ya YESU na kukataliwa kwa injili ndani ya uyahudi kisha kutoa nafasi kwa wamataifa kusikia injili.

Katika tafsiri ya majuma 70 tumeona ilianza mwaka wa 457 K.K na kuishia mwaka wa 34 A.D. juma moja la mwisho ambalo Yesu anaweka agano thabiti na watu wengi huanzia mwaka wa 27 A.D ambapo YESU alianza huduma yake duniani nayo huishia mwaka wa 34 A.D kukataliwa kwa injili na kuuawa kwa Stephano (matendo 7:54-60) ambapo nusu ya juma hilo. (kwakuwa juma lina siku 7 nusu yake itakuwa ni 31/2) huanza mwaka wa 27 A.D Kristo anapoanza huduma yake hadi 301/2 A.D anapokatiliwa na kuuawa. Nayo nusu nyingine huanza 301/2 A.D injili kwa wayahudi kwanza hadi 34 A.D wanaikataa injili na kuwaua watumishi wa MUNGU kisha mlango wa injili kwa wamataifa inafunguliwa.

Baada ya hayo ndipo litakaposimama chukizo la uharibifu, hii humaaisha kuwa baada ya huduma ya Yesu kukataliwa nao wayahudi pia kuikataa injili badala yake litasimama uharibifu mkubwa na machukizo mengi. Daniel 11:31 na wenye silaha watasimama upande wake, nao watapatia unajisi mahali patakatifu, ndiyo ngome, nao wataondoa sadaka ya kuteketezwa ya kila siku, nao watalisimamisha chukizo la uharibifu hapa Biblia hutuambia juu ya pembe ndogo iliyoinuka katika (Daniel 8:9.) ambayo katika Daniel 8:11 Naam ikajitukuza hata juu yake aliye mkuu wa jeshi hilo, ikamwondolea sadaka ya kuteketezwa ya daima, na mahali pa patakatifu pake pakaangushwa.

(patakatifu palipoangushwa hapa ni hekalu la Yerusalemu liliangushwa na utawala wa kirumi katika mwaka wa 70 A.D Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Yesu alitabiri juu ya anguko la Yerusalemu katika Mathayo 24:2……. Amin nawaambieni, Halitasalia hapa jiwe juu ya jiwe ambalo halitabomoshwa

Daniel 12:11 Na tangu wakati ule ambapo sadaka ya kuteketezwa ya daima itakapoondolewa, na hilo chukizo la uharibifu litakaposimamishwa, itapata siku elfu na mia mbili na sitini. (siku elfu mia mbili na sitini sawa na miaka 1260 huanza 538-1798 kuinuka kwa upapa hadi kutiwa kwake jeraha la mauti, Dan 7:25, Ufunuo 13:3).

Yesu anazungumzia anguko la mji wa Yerusalemu kama chukizo la uharibifu. Luka 21:20 Lakini hapo mtakapoona mji wa Yerusalemu umezungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kwamba uharibifu wake umekaribia. Kubomolewa kwa hekalu la Yerusalemu mnamo mwaka 70A.D huashiria mwisho wa taifa la Israeli na ambapo wengi wao walikimbilia katika mataifa mengine, wengine walichukuliwa mateka. Baada ya kipindi hicho ndipo ukainuka utawala wa upapa ulioleta mafundisho ya uongo na kutengua sheria za MUNGU na kulazimisha watu kuyashika yaliyo kinyume na kweli nacho kilikuwa kipindi kilichoitwa zama za giza ambacho kilidumu kwa miaka 1260……….

Chukizo la uharibifu unafananishwa na kipindi kinachokuja mbele yetu, atakaposimama Yule mharibifu mpinga Kristo. 2 Wathesalonike 2:1-4 Basi ndugu, tunakusihini, kwa habari ya kuja kwake Bwana wetu Yesu Kristo, na kukusanyika kwetu mbele zake, kwamba msifadhaishwe upesi hata kuiacha nia yenu, wala msisitishwe, kwa roho wala kwa neno, wala kwa waraka unaodhaniwa kuwa ni wetu, kana kwamba siku ya Bwana imekwisha kuwapo, Mtu awaye yote asiwadanganye kwa njia yoyote; maana haiji, usipokuja kwanza ule ukengeufu, akafunuliwa kwanza YULE MTU WA KUASI, MWANA WA UHARIBIFU………..akijionesha nafsi yake ya kwamba yeye ni Mungu.

Atakapo simama Yule mpinga kristo na kuhalallisha mafundisho ya uongo (angalia fungu la 9), pale sabato bandia itakapochukua nafasi ya Sabato halisi (Jumapili kuchukua nafasi ya Jumamosi) haya yote yatakuwa ni machukizo mbele za Mungu.

Ahadi ya MUNGU kwako.

Ufunuo 3:10 kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi name nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwenguwote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.

BWANA AKUBARIKI.

Imeandaliwa na

PETER I. JEFTER 0757916891/ 0653401497