UBATIZO WA KWELI

Ev. Mujaya MujayaNa. Ev. Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122 and +255768678122

Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version: UBATIZO WA KWELI

Huenda hujawahi kujiuliza swali hili kuwa ubatizo wa kweli ni upi? Ni kwanini kuna aina nyingi za ubatizo; yaani ubatizo wa maji mengi au maji machache? Au wa watu wazima au watoto?

Labda nianze na Waefeso.4:5, “Bwana mmoja, imani moja, na ubatizo mmoja”. Biblia inasema kuna AINA MOJA TU ya ubatizo nami napenda tuuangalie kwa undani. Na katika kuangalia aina hii ya ubatizo tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia katika ubatizo ili uwe wa kweli. Ujuzi ambao utawezesha kulinganisha na ubatizo unaoufahamu kwa kuupima kwa kipimo cha maandiko matakatifu ya kuwa niwa ukweli au uwongo.

Mambo ya kuzingatia katika ubatizo wa kweli ni:-

  1. ANAYEBATIZWA ANAPASWA AAMINI, ATUBU NA AUNGAME DHAMBI.
    Ubatizo wa kweli unapaswa kutanguliwa na mambo makubwa manne ambayo ni Kuamini, Kutubu na Kuungama. Marko.16:16, “AAMINIYE na KUBATIZWA ataokoka“; Mathayo.3:6, inasema “naye AKAWABATIZA katika Mto yordani, huku WAKIZIUNGAMA DHAMBI zao” Matendo.2:38, “TUBUNI MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo”.John baptizing
  2. MBATIZAJI NA MBATIZWA WOTE WANAINGIA NDANI YA MAJI.

Wakati Filipo anambatiza Towashi Biblia inasema, Matendo.8:38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Hili ni jambo la muhimu sana, mbatizwa na anayebatizwa wote walikuwa ndani ya maji. Na baada ya ubatizo “…walipopanda kutoka majini…” Matendo.8:39 towashi akaondoka akifurahi. Katika aya hii tunaona jambo la muhimu pia sambamba na mbatizwa na mbatizaji kuwa ndani ya maji, ni kwamba lazima kuwepo na maji mengi.

  1. NI WAKUZAMISHWA KATIKA MAJI MENGI.

Yohana mbatizaji kipindi cha Yesu alikuwa akibatiza katika sehemu iliyokuwa inaitwa Ainoni maana kulikuwa na maji tele, Yohana 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.” Yesu alibatizwa katika mto Yordani, na baada ya ubatizo Mathayo.3:16-17, …mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Mungu hupendezwa nasi kama alivyopendezwa na Yesu tunapotoka katika maji ya ubatizo maana ndivyo inavyotupasa kuitimiza haki yote (Mathayo.3:15) na Yesu alitupatia kielelezo. Lakini pia hutupatia Roho Mtakatifu kama vile hua alivyoshuka kwa Yesu ili atukamilishe kwa kutupatia tabia inayofanana na Yesu, ushindi wa dhamdi na atuongoze na atutie katika kweli yote.

Hivyo mambo haya matatu yanatosha kutuambia ubatizo wa kweli wa Biblia. Ubatizo wa watoto wachanga haufundishwi katika Biblia na wala hatuna mfano wa mtu yeyote tangu MWANZO hadi UFUNUO aliyebatizwa hivyo. Maana mtoto hawezi kuamini, akaungama na kutubu ili abatizwe.
Pia ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani hauna msingi katika Biblia maana haufundishwi katika Biblia bali ni utaratibu ambao umewekwa na wanadamu tu.

Hebu leo turudi katika ubatizo wa kweli maana Yesu anakwambia “amini amini nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Yohana.3:5.

Bwana akubariki sana unapoamua kufanya matengenezo katika jambo hili.

Kwa maoni, maswali au ushauri usisite kuwasiliana nasi.

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s