MUHURI WA MUNGU DHIDI YA ALAMA YA MNYAMA

Ev. Mujaya MujayaNa. Muinjilisti: Mujaya Mujaya
Simu Na: +255715678122 au +255768678122
Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version: MUHURI WA MUNGU DHIDI YA ALAMA YA MNYAMA

Tunaishi kipindi cha mwishoni mwa wakati wa historia ya dunia. Unabii wote uliotabiriwa katika maandiko unatimia kwa kasi na ufasaha wa ajabu. Hivi sasa tupo katika nyayo za vidole za sanamu wa Danieli 2 ambapo muda si mrefu jiwe lililochongwa pasipo kazi ya mikono ya wanadamu (Yesu) litakuja kuiponda sanamu ile (tawala za dunia) na kusimamisha ufalme wake wa milele. Pote tunaona dalili na viashiria vya ujio wa Yesu vikitimia kama ilivyotabiriwa kutoka katika kinywa cha mwanahistoria na nabii mkuu Yesu wa Nazareti kwenye Luka 21 na Mathayo 24. Hali ilivyo ndani ya kanisa na nje ya kanisa lake pia huakisi utimilifu wa unabii wa Mathayo 25.

Lakini Yesu atakapokuja tena kutakuwapo na makundi mawili tu. Kundi moja nila wateule, watakatifu wa Mungu na kundi la pili ni waovu watu waliokataa kuishi kulingana na matakwa ya Mungu pamoja na waliopo upande wa katikati yani wakisema wapo upande wa Mungu huku hawajajisalimisha kwa Yesu awafanye upya nia zao.

Makundi haya mawili yanafananishwa tena na:- Ngano na Magugu; Kondoo na Mbuzi; Wana wa nuru na Wana wa Giza; na Wenye Muhuri wa Mungu na Wenye alama ya Mnyama.

Kuhusu Mihuri ndiyo kiini cha somo hili. Yesu atakapokuja kutakuwapo na makundi mawili kundi la kwanza ni la wale wenye muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao na kundi la pili ni wale wenye muhuri au alama ya mnyama katika vipaji vya nyuso na viganja vya mikono yao ya kuume.
“Kunawezekana kuwepo matabaka mawili tu. Kila kundi limepigwa muhuri tofauti, ama muhuri wa Mungu aliye hai, au chapa ya mnyama au sanamu yake” MSM uk. 166

Muhuri hutumika kutofautisha, kutenga na kufanya kitu au mtu kuwa wa pekee. Wakati Yesu akibagua kondoo na mbuzi atakuwa akiangalia katika vipaji vya nyuso zetu kama kuna muhuri wake au hakuna.

Muhuri hutumika kuelezea mamlaka au utawala na cheo cha mtu fulani. Hivyo kwa muhuri tulionao tunajibainisha ya kuwa sisi tupo chini ya mamlaka ipi au tunatawaliwa na mtawala gani aidha Mungu wa mbinguni au shetani.
Muhuri wa Mungu.

Muhuri wa Mungu maana yake ni “Kutulia katika ukweli, kiakili na kiroho kiasi kwamba hawawezi kuyumbishwa”. MSM uk.169, 4BC 1162 (1902). Mara tu watu wa Mungu wanapotiwa muhuri katika vipaji vya nyuso zao Pepeto litakuja ambao umeshaanza tayari.

Muhuri wa Mungu unafananishwa na alama ya damu ya mwanakondoo iliyowekwa Seal of God 2katika miimo ya milango ya nyumba za waebrania usiku ule kabla ya kutoka Misri ili kuwahifadhi dhidi ya maangamizi ya jumla.
“Alama inawekwa juu ya kila mmoja wa watu wa Mungu, kwa hakika ni kama vile alama iliyowekwa juu ya milango ya makazi ya waebrania ili kuwahifadhi watu dhidi ya maangamizi ya jumla.” MSM uk. 170

Hivyo wakati wa maangamizi ya mwisho, malaika watazuiwa wasiwadhuru watu waliotiwa muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao. Ezekieli 9:6.

Muhuri wa Mungu hauonekani kwa macho ya kibinadamu. Ni ishara ya ushindi juu ya dhambi yote…muhuri wa Mungu ni alama inayowatambulisha watu wa Mungu kuwa wake. Kutiwa katika vipaji vya nyuso zao huonesha kuwa ni katika tabia. Nguvu inayotia muhuri ni Roho Mtakatifu, Waefeso 4:30; Ufunuo, uk. 48.

Muhuri wa Mungu pia humaanisha utunzaji wa Sabato ya siku ya saba ya juma kikamilifu. Maana amri ya nne juu ya utunzaji wa Sabato ndiyo pekee yenye muhuri wa Mungu maana ndiyo kipimo cha uaminifu wetu kwa Mungu, muumbaji, mkombozi na mtakasaji wetu.

Ezekieli 20:12
“Tena naliwapa Sabato zangu , ziwe ishara (Muhuri) kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi Bwana ndimi niwatakasaye.”
“Uadhimishaji wa ukumbusho wa Bwana, Sabato iliyoanzishwa katika edeni, Sabato ya siku ya saba, ndiyo kipimo cha uaminifu wetu kwa Mungu.” Letter 94, 1900.

Sifa Za Watu Wanaowekwa Muhuri Wa Mungu.
Ili kutiwa muhuri wa Mungu katika kipaji cha uso wako ni lazima:-
Kushika kwa makini Sabato ya Bwana
“Muhuri wa Mungu aliye hai unawekwa juu ya wale ambao kwa makini wanaitunza Sabato ya Bwana…wale ambao wangependa kuwa na muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao lazima watunze Sabato ya amri ya nne” MSM uk. 169
Kufanana na Kristo kitabia. “Muhuri wa Mungu aliye hai utawekwa juu ya wale tu wanaofanana na Kristo kwa tabia”. 7BC 790 (1895)
“Wale wanaopokea muhuri wa Mungu aliye hai na wanalindwa katika wakati wa taabu lazima waakisi sura ya Yesu kikamilifu” EW 71 (1851)
Kushinda ulimwengu, tamaa za mwili na yule mwovu.
“Wale watakaoushinda ulimwengu, tama za mwili, na yule mwovu, ndio watakaopata upendeleo maalumu wa kupokea muhuri wa Mungu aliye hai.” TM 445
Kutenda kazi ya Mungu. “Wale wanaompenda Mungu, wanao muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao, na hutenda kazi ya Mungu.” SD 51

seal of God 3Je, Muhuri Wa Mungu Utapigwa Wakati Gani?
Ufunuo 7:1-4,
“Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini”

Tukio hili la kutia muhuri watumwa wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao linatokea kati ya kufunguliwa kwa muhuri wa sita na wa saba yani karibu na marejeo ya Yesu mara ya pili lakini baada ya tukio la kuanguka kwa nyota za mbinguni katika mihuri ya sita mwaka 1833 usiku wa Novemba 13 ambapo nyota zilianguka kama vile mti upukutishavyo mapooza.

Neno “Upepo” katika unabii humaanisha mashindano, vita na machafuko kati ya mataifa. Yeremia 25:32. Machafuko, vita na mashindano hayo huzuia maendeleo ya kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu. Wakati pepo nne zitakapo achiwa kutakuwa na machafuko makubwa sana, ndiyo vita ya Halmagedoni ya Ufunuo 16 hivyo Mungu amemtuma malaika wake kuzuia hadi atakapowatia muhuri watumwa waaminifu wake.

Wakati wa kutiwa muhuri wa Mungu kwa kuzingatia kipimo cha utunzaji wa Sabato ya siku ya saba umeanza tangu Yesu alipoingia katika chumba cha patakatifu pa patakatifu katika hekalu la mbinguni kuanzia mwezi wa saba 1844 hadi sasa. Wakati hukumu ya upelelezi inaendelea uamuzi unatolewa aidha kwajili ya uzima na wengine kwajili ya mauti. Wale wanaomkiri Yesu kama Bwana na mwokozi wao binafsi wakikuza uhusiano wao na Yesu kila siku wanatiwa muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

“Niliona kuwa kipimo cha sasa kuhusu Sabato kisingeweza kuja mpaka uombezi wa Yesu katika patakatifu umemalizika naye amehama kuingia pazia la pili…kabla ya kuingia mlango wa patakatifu pa patakatifu…kwa sababu hawakuwa na nuru, na kipimo kuhusu sabato ambacho sasa tunacho tangu mlango ule ulipofunguliwa…
Shetani sasa anatumia kila mbinu katika wakati huu wa kutiwa muhuri kuzuia nia za watu wa Mungu dhidi ya ukweli wa sasa na kuwasababisha wayumbe.” EW 42,43.

Baadhi ya watu ambao wamekufa tayari wametiwa muhuri kwasababu walikufa katika Kristo.
“Niliona kuwa Bi. Hastings alikuwa ametiwa muhuri na angeinuka wakati wa sauti ya Mungu na kusimama juu ya dunia, na angekuwa pamoja na wale 144,000. Niliona kuwa hatuhiaji kuomboleza kwajili yake ; angepumzika wakati wa tabu.” 2 SM 263

Kuna wazee walio hai wenye umri mkubwa wametiwa muhuri katika vipaji vya nyuso zao kwa kuwa wanamwamini Mungu nathe mark of the beast wanapendwa na Mungu. Wazee hao watakuwa miongoni mwa idadi ambayo Bwana amesema “Heri wafu wafao katika Bwana”. MSM uk. 172

“Kazi ya malaika ya kuwatia muhuri watu wa Mungu ndiyo kazi muhimu inayotendeka sasa katika ulimwengu. Itatendeka mpaka katika kila taifa, jamii, lugha na kabila wafuasi wa kweli wa Mungu watakapokuwa wametiwa muhuri. Hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia kukamilishwa kwa kazi hii…Malaika wanaendeleza kazi ya kuzuia pepo za vita katika ulimwengu kwa muda kitambo…huzuia pepo hizo ili kazi ya injili iweze kuendelea…Sasa ni wakati wa kupokea muhuri wa Mungu.” Ufunuo u.k 50-51

Alama ya Mnyama
Alama ya mnyama maana yake ni utunzaji au uadhimishaji wa siku ya Jumapili. TM 133.
“Wakati wa kupimwa utakapofika, itaoneshwa dhahiri kile ilicho chapa ya mnyama. Ni uadhimishaji wa Jumapili…
Ishara au muhuri wa Mungu umefunuliwa katika uadhimishaji wa Sabato ya siku ya saba, ukumbusho wa Bwana wa uumbaji…Chapa ya mnyama ni kinyume na hili, uadhimishaji wa siku ya kwanza ya juma.” MSM uk. 172

Alama ya mnyama itawekwa katika mkono wa kuume au katika vipaji vya nyuso. Ufunuo 13:16,
“Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;”

Hii haimaanishi kwamba katika mkono itaandikwa alama hiyo au itaandikwa katika vipaji vya uso bali:-
1. Katika mkono wa kuume: kukubali kutofanya kazi za mikono siku ya Jumapili kama Sabato.
2. Katika vipaji vya nyuso: kukiri bila budi kwamba Jumapili ni Sabato. MSM 173

Je, Alama ya Mnyama Itapigwa Wakati Gani?
666_mark_of_the_beastWakati wa kupigwa na kupokea alama ya mnyama bado haujafika. Utunzaji wa Jumapili kwa sasa si alama ya mnyama.
“Hakuna ambaye tayari amekwishapokea chapa ya mnyama…uadhimishaji wa Jumapili bado siyo chapa ya mnyama, na haitakuwa hadi amri kuu imetolewa kuianubudu sanamu hii ya Sabato. Wakati utafika ambapo siku hii itakuwa ndicho kipimo, lakini wakati huo bado haujafika” MSM 173

Wakati mtu anapopata nuru juu ya amri kumi za Mungu na utunzaji wa Sabato lakini anaendelea kutotii atapokea alama ya mnyama. Ni wale ambao wanaendelea katika uasi baada ya kufahamu nuru ya mbinguni ndio watapokea alama ya mnyama.
“Wote ambao watabakia kuwa wakweli kwa Mungu na Sabato watapokea muhuri wa Mungu, huku mtu yeyote atakayeacha Sabato, au wote ambao wataendelea kuadhimisha Jumapili baada ya kuufahamu ukweli watapokea alama ya mnyama”. Maranatha, uk. 164

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s