Mambo Mhimu ya Kuzingatia Katika Chakula Ili Kiwe na Matokeo Mema Mwilini.

Ev. Mujaya MujayaNa. Muinjilisti Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122

+255768678122

Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version:Kanuni Za Kuzingatia Katika Chakula Ili Kiwe na Matokeo Mema Yaliyokusudiwa

Chakula chema ambacho Muumbaji wetu ametupatia ili tukitumie imetupasa tukitumie kwa uangalifu na tahadhali tangu katika uchaguzi na maandalizi yake. Hata chakula kiwe kinafaa kwa namna gani lakini kama kikiandaliwa au kutumiwa vibaya mtu hawezi kunufaika kwacho. Katika sehemu hii tutaangalia kanuni muhimu za uchaguzi, maandalizi na matumizi bora ya chakula ili kifae kuleta matokeo mema yanayotarajiwa na mtumiaji.

Uchaguzi wa Chakula

Watu wengi wanachagua chakula ili kukidhi tamaa ya mwili, kumbe chakula kingechaguliwa kuzingatia utajiri wake wa viritubisho mwilini. Kanuni zifuatazo zafaa kuongoza uchaguzi wetu wa chakula kifaacho:

 1. Kama kuna wakati ambapo chakula tunachokula kinapaswa kuwa rahisi basi ni sasa. Chakula tunachotumia kiwe kinachopatikana kwa urahisi katika mazingira yanayotuzunguka.
 2. Kukidhi mazingira. Chakula tunachokula kinapaswa kiendane na msimu, hali ya hewa na kazi tunayofanya. Chakula kinachofaa kutumika katika msimu au hali ya hewa fulani hakifai kutumika katika mazingira ya msimu na hali ya hewa nyingine. Na pia kuna aina mbalimbali za chakula maalumu kwa kazi au shughuli fulani tu. Chakula cha mtu anaefanya kazi ngumu za nguvu ni tofauti na mtu anayefanya kazi za kukaa ofisini na kutumia akili. Mungu ametupatia aina mbalimbali za vyakula hivyo ni bora kuchagua chakula kukidhi mahitaji yetu.
 3. Utoshelevu, Utamu na aina mbalimbali. Meza zipambwe kwa vyakula vya nafaka, matunda na mbogamboga za aina mbalimbali, tamu sana na zenye utajiri wa virutubisho.

Maandalizi ya Chakula

Chakula kilichochaguliwa vema ili kifae kutumika pia kinapaswa kuandaliwa vema. Tatizo kubwa lipo katika maandalizi ya chakula kabla hakijaletwa mezani. Wanawake na wanaume wengi sana hawajui kuandaa chakula ambacho Mungu amewapatia na hivyo kukiweka mezani kikiwa tupu bila virutubisho au kikiwa kimejaa sumu mbalimbali na vimelea vya magonjwa. Taaluma ya kuandaa chakula bora katika mazingira ni muhimu sana kwa wanaume na wanawake wote. Kanuni zaSAM_0454 maandalizi ya chakula ni:

 1. Osha matunda na mbogamboga kwa maji safi kabla haiuazitumia. Vyombo vyote vya kuandalia chakula, mazingira ya kuandalia chakula na muandaaji wanapaswa kuwa safi. Kichwa kifunikwe kuzuia uchafu kutoka katika nywele kuvamia chakula.
 2. Kisichokobolewa au kusafishwa sana.
 3. Kisichoiva sana kama ni mbogamboga na nafaka mbichi/zenye ukijani. Matunda na mbogamboga mbichi/zenye ukijani zina manufaa sana zikitumiwa mbichi kuliko zikipikwa japo zingine ni lazima zipikwe kidogo. Unaweza kupika kwa kutumia mvuke ili kutunza/kuhifadhi virutubisho.
 4. Kamwe usimwage maji uliyotumia kuandaa mbogamboga bali uyaweke sehemu ya mboga yako maana ni tajiri ya virutubisho muhimu. Ili kufanikiwa katika hili, unapaswa kuweka kiasi kidogo cha sana maji wakati unaandaa mboga yako kitakachotosha kuivisha tu. Kama utahitaji mboga isiyo na majimaji, basi hakikisha unayanywa maji yote baada ya kuyatenga na mboga yako.
 5. Pika viazi na maboga pamoja na maganda yake, bila kumenya. Nusu nchi ya nje ya viazi na maboga ni sehemu muhimu kuliko zote za boga au kiazi hivyo hakikisha haumenyi kabla ya kupika kuzuia kutupa virutubisho. Fanya hivi hata kwa viazi mviringo.
 6. Kisichokolezwa kwa viungo na vichocheo vingi. Sukari. Chumvi, Amira na Soda
 7. Kitamu, kinapendeza kukitazama, kinanukia vizuri, ladha nzuri, virutubisho vingi vya hali ya juu, si cha gharama kubwa, urahisi wa kutayarisha na hakina gharama.
 8. Usitumie vyombo vya Aluminiamu kuandaa chakula. Usichemshe maji katika vyombo hivi wala usinywe juisi au maji yaliyotunzwa katika chombo cha aluminiamu.

Matumizi ya Chakula

 1. Kula kwa wakati. Chakula hakipaswi kuliwa mapema sana au kwa kuchelewa sana, inapaswa kuwe na ratiba ya chakula.
 2. Usile kupita kiasi. Tumia chakula kinachotosha tu kutosheleza njaa kisha acha. Kipimo cha chakula unachojipimia kulainapaswa uweze kula nusu yake tena ikiwa utapewa baada ya kumaliza.
 3. Usijaze chakula kingi mdomoni. Katika kula chakula, weka kiasi kidigi tu kinachotosha kutafunwa vema na kuchanganywa na mate.IMG_20131029_210909
 4. Tulia na kula taratibu. Usile chakula ukiwa katika harakaharaka, ukiwa una uchovu au hasira kali. Wakati mzuri wa kupumzika ni kabla yam lo na kutembeatembea baada yam lo.
 5. Tafuna chakula chako vizuri maana tumboni hamna meno mengine. Kwa kutafuna vizuri unaweza ukapata nguvu na virutubisho vingi katika kiasi kidogo tu cha chakula.
 6. Usile michanganyiko mingi ya chakula kwa wakati mmoja. Unahitaji aina tatu au nne tu ukiongeza chumvi na mafuta kidogo tu.
 7. Epuka michanganyiko mikali ya chakula. Chakula unachotumia kisiwe kimechanganywa sana maana kitavuruga tumbo na kuchelewesha mmeng’enyo.
 8. Badilisha chakula chako kati ya mlo mmoja na mwingine. Kama umekula viazi mlo mmoja basi kula ugali au ndizi mlo mwingine.
 9. Mbali na juisi ya matunda halisi au mbogamboga, kunywa maji kati ya milo wala si pamoja na chakula chako.
 10. Usichanganye matunda na mbogamboga, kama umekula matunda mlo mmoja basi kula mbogamboga mlo mwingine.
Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s