Je, Siku ya Jumapili Ina Utakatifu Wowote Kwa Sababu Yesu Alifufuka?

Ev. Mujaya MujayaMuinjilisti Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122 au +255768678122

Barua Pepe: ev.mujaya@yahoo.com

Downloadable Version: Je, Siku Ya Jumapili Ina Utakatifu Wowote Kwa Sababu Yesu Alifufuka?

Katika juma moja kuna siku 7 tu ambazo zinajirudia rudia. Ili kujua utakatifu wa siku ni lazima tuangalie chimbuko la kila siku yenyewe ya kwamba itokana na nini? Zipo kwajili gani na makusudi ya uwepo wake ni nini?

Siku ya kwanza katika juma ni Jumapili na siku ya mwisho ni Jumamosi, hivyo juma huanzia siku ya Jumapili na kuishia siku ya Jumamosi. Yesu alifufuka katika wafu siku ya kwanza ya juma, siku ambayo wakristo wengi wanasherekea kufufuka kwa Bwana Yesu kutoka katika wafu yani ikiitwa Jumapili ya pasaka. Luka. 24:1-3, “Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu.” Ukifatilia pia katika kalenda na kamusi utathibitika katika jambo hili kwamba juma huanzia Jumapili na kuishia Jumamosi.Jesus Resurrection-17

Chimbuko la siku zote hizi huanzia katika uumbaji wa Mungu. Na kutokea kwa Muumbaji tunaweza kujua umuhimu au utakatifu wa siku kama uliwekwa na Muumbaji. Mwanzo.2:1-3, “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya.” Biblia inasema kwamba Mungu aliibariki na kuitakasa siku ya saba yani Jumamosi baada ya kumaliza kufanya kazi yake ya uumbaji kwa siku sita. Siku hii ya saba ikatengwa itumike kwa makusudi matakatifu, na siku ambayo Muumbaji alipumzika na kustarehe, siku hii ndiyo Sabato.

Biblia inasema tunapaswa kuitunza siku ya Saba maana ndiyo Sabato ya Bwana Mungu wetu; katika siku hiyo tunalazimika kujipumzisha kazi zetu kama Mungu muumbaji wetu alivyitupatia kielelezo. Siku ya saba ni Sabato ya Bwana Mungu wetu, Kutoka. 20:9-11 inasema, Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa.” Sabato ni siku pekee ya juma iliyobarikiwa na kutakaswa.

Kubarikiwa na kutakaswa kwa siku ya Sabato hakubadiliki maana alichokianzisha Mungu hudumu milele, Mhubiri 3:14, “Najua ya kwamba kila kazi aifanyayo Mungu itadumu milele; haiwezekani kuizidisha kitu, wala kuipunguza kitu; nayo Mungu ameifanya ili watu wamche Yeye.” Mungu hana kigeugeu wala hatalihalifu neno lililotoka katika kinywa chake, Malaki 3:6, Zaburi 89:34 “Kwa kuwa mimi, Bwana, sina kigeugeu;…Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu.” Baraka na utakatifu wa siku ya Sabato hauwezi kubadilika kwenda siku nyingine maana baraka hizo niza milele, 1 Nyakati.17:27 “…kwa maana wewe, Bwana, umebarikia, nayo imebarikiwa milele.” Siku ya Sabato imebarikiwa milele wala baraka hizo za Bwana haziwezekani kutanguka, Hesabu 23:20 “Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.”

work daySiku ya kwanza hadi ya sita huitwa siku za kazi, Ezekieli 46:1 “Bwana MUNGU asema hivi; Lango la ua wa ndani, lielekealo upande wa mashariki litafungwa siku sita za kazi; lakini siku ya sabato litafunguliwa, na siku ya mwezi mpya litafunguliwa.” Hapa tunaona siku zote za juma zikiwekwa katika makundi makubwa mawili ya siku sita za kazi(siku ambazo Mungu alifanya kazi) na siku ya Sabato(Siku ambayo Mungu alipumzika akaibariki na kuitakasa). Siku hizo sita za kazi ni tofauti kabisa na siku ya saba ambayo inaitwa Sabato ya Bwana, starehe takatifu.

Wakati wana wa Israeli wakiwa njiani kuelekea nchi ya ahadi, Mungu alitaka waelewe umuhimu wa Sabato yake takatifu kwa kuwapatia mana(chakula kutoka mbinguni) posho siku sita za kazi na kutotoa posho hiyo siku ya saba(Sabato) badala yake kutoa ruhusa kuokota chakula cha siku mbili siku ya sita. Kutoka 16:22-30, “Basi ikawa siku ya sita wakaokota kile chakula sehemu maradufu, kila mtu pishi mbili; na wazee wote wa mkutano wakaenda na kumwambia Musa. Akawaambia, Ndilo neno alilonena Bwana Kesho ni starehe takatifu, Sabato takatifu kwa Bwana; okeni mtakachooka, na kutokosa mtakachotokosa; na hicho kitakachowasalia jiwekeeni kilindwe hata asubuhi. Basi wakakiweka hata asubuhi, kama Musa alivyowaagiza; nacho hakikutoa uvundo wala kuingia mabuu. Musa akasema, Haya, kuleni hiki leo; kwa kuwa leo ni Sabato ya Bwana; leo hamtakiona nje barani. Siku sita mtaokota; lakini siku ya saba ni Sabato, siku hiyo hakitapatikana. Ikawa siku ya saba wengine wakatoka kwenda kukiokota, wasikione. Bwana akamwambia Musa, Mtakataa kuyashika maagizo yangu na sheria zangu hata lini? Angalieni, kwa kuwa Bwana amewapa ninyi hiyo Sabato, kwa sababu hii huwapa siku ya sita chakula cha siku mbili; kaeni kila mtu mahali pake, mtu awaye yote asiondoke mahali pake kwa siku ya saba. Basi hao watu wakapumzika kwa siku ya saba.” Jambo la msingi pia katika aya hizi, ni kwamba Mungu alichukizwa kwa wana wa Israeli kutoheshimu Sabato yake na kwenda kuokota mana.

Kama ilivyokuwa kwa wana wa Israeli, Mungu amekusudia kuwaelekeza watu wa kila lugha, kabila, jamaa na mataifa yote wanaosafiri kuelekea nchi ya ahadi, Kaanani ya mbinguni kutambua umuhimu wa Sabato yake kwa kufanya kazi kwa siku sita na kupumzika siku ya saba na kuitakasa. Katika safari yetu kuelekea Kaanani ya mbinguni Mungu anataka tujue kutofautisha kati ya mambo matakatifu na mambo yakawaida, kati ya siku takatifu na siku za kawaida. Ezekieli 22:26, “… wametia unajisi vitu vyangu vitakatifu; hawakuweka tofauti ya vitu vitakatifu na vitu vya kutumiwa sikuzote;…nao wamefumba macho yao, wasiziangalie sabato zangu, nami nimetiwa unajisi kati yao…”Fall Worship 1

Kuna nadharia kwamba Utakatifu wa siku ya saba ulihama kutoka Jumamosi kwenda Jumapili maana ndiyo siku ambayo Yesu alifufuka. Na kwamba mitume na wakristo wa karne ya kwanza baada ya Kristo walihamisha utukufu au utakatifu na baraka toka Jumamosi kwenda Jumapili. Hebu tuichunguze nadharia hii kwa undani.

Ukifanya uchunguzi wa makini kuhusu siku ya kwanza ya juma, siku ya ufufuko wa Yesu utagundua kwamba haikuwa siku takatifu. Kama ilivyokuwa toka mwanzo wa uumbaji, siku ya Jumapili ni siku ya kazi. Katika sehemu zote ambapo siku ya Jumapili imetajwa katika maandiko matakatifu, hakuna hata sehemu moja ambayo inaitaja siku hiyo kama siku takatifu.

Katika biblia, agano la kale na jipya siku ya kwanza ya juma inatajwa mara 8 tu, kati ya mafungu hayo yote hakuna hata aya moja inayo onyesha kwamba utakatifu wa Sabato ya Jumamosi ulihamia katika siku ya Jumapili. Aya zote zinazungumzia siku ya kufufuka kwa Yesu katika wafu tu.

Katika biblia, agano jipya pia hakuna mfano hata mmoja wa mitume au wakristo wa kwanza waliohamisha utukufu toka siku ya Jumamosi kwenda Jumapili. Katika siku ya Jumapili kama ilivyo siku nyingine za kazi, wakristo waliambiwa wafanyapo kazi wakumbuke kutenga sehemu ya mapato yao nyumbani kwa kadiri wanavyofanikiwa katika kazi ili michango isifanyike wakati wanapotembelewa na mitume. 1 Korintho 16:1-2, “Kwa habari ya ile changizo kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo. Siku ya kwanza ya juma kila mtu kwenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja;” Pia katika siku hiyo watu waliendelea na shughuli za kilimo mashambani, Marko 16:12 “Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.” Hii ilikuwa siku ambayo Yesu alipofufuka aliwatokea watu wawili waliokuwa wanaenda shambani, kinyume chake siku ya Sabato walistarehe kama ilivyokuwa imeamriwa. Luka 23:56, “Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa.” Hapa Yesu alikuwa kaburini siku ya maandalio(ijumaa) jioni wakati Sabato ilikuwa inaingia. Tazama, Luka 23:54-55 na Marko 15:42.

Aya nyingine katika Biblia ya Matendo 20:7 inatumiwa kimakosa kusema kwamba mitume walikutana kwa ibada na kumega mkate katika siku ya Jumapili badala ya Sabato kama ilivyoamriwa na Mungu. Mkutano wa ibada unaozungumziwa katika Matendo 20:7 ulifanyika siku ya Jumamosi jioni kwa kuwa siku ya Jumapili asubuhi Paulo aliazimia kusafiri umbali mrefu maana ilikuwa siku ya kazi, jambo ambalo asingelifanya katika siku ya Sabato. Katika biblia siku huanza jioni jua linapozama na huisha pia wakati jua linapozama wala si saa.6 usiku. Hivyo siku ya Sabato inaanza siku ya Ijumaa jioni wakati wa kupunga jua na pia huishia siku ya Jumamosi wakati wa kupunga jua na kisha siku ya Jumapili inaanza. Biblia ya Kiswahili cha kisasa inaweka wazi kwamba “Na Jumamosi jioni tulipokutana ili kuumega mkate…”, huduma hii ilifanyika kama mwendelezo wa ibada ya kutwa ya Sabato kwakuwa Paulo alikusudia kusafiri asubuhi siku ya pili yake.

Pia ieleweke kwamba kumega mkate na kukutana kwa ibada inaweza ikawa siku yoyote ile ili tuweze kuwa na uhusiano mzuri na Mungu. Ili kukua kiroho tunapaswa kusoma neno la Mungu, ibada na sala kila siku. Mimi binafsi nafanya ibada kila siku ya juma. Lakini ibada ya kila siku inatakiwa iambatane na kufanya kazi kwa bidii yote wakati ibada ya siku ya Jumamosi inatakiwa iambatane na pumziko maana ni siku takatifu ya Mungu.

Katika Yohana 20:19 tunaona mkutano wa wanafunzi wa Yesu, siku ambayo Yesu alifufuka. “Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu.” Mkutano huu haukuwa wa ibada bali ulikuwa wa kujificha kwa hofu ya wayahudi maana waliogopa askari wa kirumi wasije wakawakamata na kuwauwa kama walivyofanya kwa BWANA wao. Hawakukutana kuadhimisha ufufuko wa Yesu maana hata walikuwa hawajaamini ya kwamba Yesu amefufuka.

Hakuna utakatifu wowote katika siku ya Jumapili na hakuna sehemu yoyote inayotoa mamlaka ya kuamisha utakatifu kutoka Jumamosi kwenda Jumapili maana kilichobarikiwa na Mungu hubaki kubarikiwa kwa kuwa Mungu hana kigeugeu kubadilisha maagizo na sheria zake. Yesu aliye Bwana wa Sabato ni yuleyule jana leo na hata milele (Waebrania 13:8) hivyo anakualika uanze katika juma hili kuadhimisha siku ya Jumamosi, siku ya utakatifu wake. Usichelewe wahi katika Sabato ya Bwana Mungu wako Jumamosi ya juma hili katika kanisa la waadventista wa Sabato lililopo karibu nawe.

Kuwasiliana nami kwa maombi, maswali, maoni au ushauri tumia njia zifuatazo:

Muinjilisti Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122 au +255768678122

Barua Pepe: ev.mujaya@yahoo.com

Advertisements

One comment on “Je, Siku ya Jumapili Ina Utakatifu Wowote Kwa Sababu Yesu Alifufuka?

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s