Matukio Mbalimbali ya mkutano wa injili wa ATF

Matukio Mbalimbali ya Mkutano mkubwa wa Injili wa ATF unaofanyika katika kijiji cha Peko Misegese ukiendeshwa na ShareHope wakishirikiana na Kanisa la Wadventista wa Sabato Mzumbe, Mlali peyapeya na TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe.

Mkurugenzi mkuu wa ShareHope, Ev. Basilio Maliwanga akiwa katika kazi za kujitolea za huduma kwa jamii.

Mkurugenzi mkuu wa ShareHope, Ev. Basilio Maliwanga akiwa katika kazi za kujitolea za huduma kwa jamii.

Baadhi ya wanakijiji(wenyeji) wa Peko Misegese walishirikiana na ShareHope katika huduma kwa jamii. Kulia katika picha ni Ev. John Mafuru Musibha Mkaguzi wa Ndani ShareHope akilima.

Baadhi ya wanakijiji(wenyeji) wa Peko Misegese walishirikiana na ShareHope katika huduma kwa jamii. Kulia katika picha ni Ev. John Mafuru Musibha Mkaguzi wa Ndani ShareHope akilima.

Baadhi ya wahudumu wa semina ya mapishi ya kikristo wakiwa katika semina. Katikati ni Ev. Janeth Christopher, Mkurugenzi wa Afya na Kiasi wa ShareHope akiendesha semina hiyo. Kushoto kwake ni Ev. Suleiman Ally, Muinjilisti mlei wa kundi la Peko Misegese.

Baadhi ya wahudumu wa semina ya mapishi ya kikristo wakiwa katika semina. Katikati ni Ev. Janeth Christopher, Mkurugenzi wa Afya na Kiasi wa ShareHope akiendesha semina hiyo. Kushoto kwake ni Ev. Suleiman Ally, Muinjilisti mlei wa kundi la Peko Misegese.

Mapishi yakichemka wakati darasa la semina za mapishi ya kikristo likiendelea

Mapishi yakichemka wakati darasa la semina za mapishi ya kikristo likiendelea

Mkurugenzi Mkuu wa ShareHope akifundisha darasa maalumu la watoto wakati ShareHope ikiendesha mkutano wa ATF(Almost Time To Fly) katika kijiji cha Peko Misegese.

Mkurugenzi Mkuu wa ShareHope akifundisha darasa maalumu la watoto wakati ShareHope ikiendesha mkutano wa ATF(Almost Time To Fly) katika kijiji cha Peko Misegese.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in News

Mkutano Mkubwa Wa Injili(ATF) Kuanza Rasmi

Na ShareHope Ministries

Ule mkutano mkubwa wa kihistoria wa injili wenye dhima inayokwenda kwa jina la Almost Time to Fly (ATF) unategemewa kuanza rasmi leo tarehe 12-07-2015 katika kijiji cha Peko Misegese. Tayari timu ya watoa huduma kutoka ShareHope Ministries imewasili na kupata mapokezi yenye ukarimu wa pekee kuakisi kiu ya muda mrefu ya wana Peko Misegese kusikia maneno ya kweli ya uzima. Tunamshikuru sana Mungu maandalizi yote yamekamilika kwa ushirikiano wa kanisa la SDA Mlali Peyapeya, Mzumbe na TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe.

Wahudumu katika Mkutano huo ni:-

  1. Mhudumu Neno la Uzima: Ev. Peter Jefta
  2. Ujasiriamali, Afya na kiasi: Ev, Basilio Maliwanga

  3. Semina za mapishi ya kikristo na malezi: Ev. Janeth Christopher

  4. Huduma kwa jamii, watoto na michezo: Ev. John Mafuru

  5. Mkuu wa kambi, ushuhudiaji na ukarimu: Ev. Suleiman Ally

Tuombee kazi ya Mungu Peko Misegese. Ni wakati wa kupaa….

Timu ya wahudumu kutoka ShareHope Ministries wakiwa tayari kuelekea Peko Misegese kwajili ya Mkutano wa Injili ATF. Kuanzia kulia ni Ev. John Mafuru, Peter Jefta na Janeth Christopher.

Timu ya wahudumu kutoka ShareHope Ministries wakiwa tayari kuelekea Peko Misegese kwajili ya Mkutano wa Injili ATF. Kuanzia kulia ni Ev. John Mafuru, Peter Jefta na Janeth Christopher.

Ev. Janeth Christopher katika picha akiwa safarini

Ev. Janeth Christopher katika picha akiwa safarini

Mkazi wa kijiji cha Peko ambaye pia ni mshiriki wa kanisa la SDA Mlali Peyepeya akijilukana kama mama. Isaac akifurahia kuwapokea wainjilisti.

Mkazi wa kijiji cha Peko ambaye pia ni mshiriki wa kanisa la SDA Mlali Peyepeya akijilukana kama mama. Isaac akifurahia kuwapokea wainjilisti.

Muinjilisti Peter Jefta akifurahia baraka za Bwana kwa kipande cha muwa. Hakika nchi hii imebarikiwa sana, tumwombe Mungu ATF ipate matunda mengi yatakayoleta chachu kwa wokovu wa kijiji kizima.

Muinjilisti Peter Jefta akifurahia baraka za Bwana kwa kipande cha muwa. Hakika nchi hii imebarikiwa sana, tumwombe Mungu ATF ipate matunda mengi yatakayoleta chachu kwa wokovu wa kijiji kizima.

Muinjilisti Janeth Christopher akiwa katika kutembelea washiriki kama sehemu ya maandalizi ya ATF. Bibi aliye katika picha ni Binti. Kaungo ambaye hakumbuki mwaka wake wa kuzaliwa ila anakumbuka alishuhudia vita ya kwanza ya dunia mwaka 1918 akiwa binti mdogo.

Muinjilisti Janeth Christopher akiwa katika kutembelea washiriki kama sehemu ya maandalizi ya ATF. Bibi aliye katika picha ni Binti. Kaungo ambaye hakumbuki mwaka wake wa kuzaliwa ila anakumbuka alishuhudia vita ya kwanza ya dunia mwaka 1918 akiwa binti mdogo.

Kelele za mbuzi zimezimwa kuacha Mungu aseme na wanakijiji wa Peko Misegese. Tuombee kazi ya Mungu katika kijiji cha Peko Misegese.

Kelele zote zimezimwa kimya ili kuacha Mungu aseme na wanakijiji wa Peko Misegese. Tuombee kazi ya Mungu katika kijiji cha Peko Misegese.

By ShareHope Ministries Posted in News

MUHURI WA MUNGU DHIDI YA ALAMA YA MNYAMA

Ev. Mujaya MujayaNa. Muinjilisti: Mujaya Mujaya
Simu Na: +255715678122 au +255768678122
Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version: MUHURI WA MUNGU DHIDI YA ALAMA YA MNYAMA

Tunaishi kipindi cha mwishoni mwa wakati wa historia ya dunia. Unabii wote uliotabiriwa katika maandiko unatimia kwa kasi na ufasaha wa ajabu. Hivi sasa tupo katika nyayo za vidole za sanamu wa Danieli 2 ambapo muda si mrefu jiwe lililochongwa pasipo kazi ya mikono ya wanadamu (Yesu) litakuja kuiponda sanamu ile (tawala za dunia) na kusimamisha ufalme wake wa milele. Pote tunaona dalili na viashiria vya ujio wa Yesu vikitimia kama ilivyotabiriwa kutoka katika kinywa cha mwanahistoria na nabii mkuu Yesu wa Nazareti kwenye Luka 21 na Mathayo 24. Hali ilivyo ndani ya kanisa na nje ya kanisa lake pia huakisi utimilifu wa unabii wa Mathayo 25.

Lakini Yesu atakapokuja tena kutakuwapo na makundi mawili tu. Kundi moja nila wateule, watakatifu wa Mungu na kundi la pili ni waovu watu waliokataa kuishi kulingana na matakwa ya Mungu pamoja na waliopo upande wa katikati yani wakisema wapo upande wa Mungu huku hawajajisalimisha kwa Yesu awafanye upya nia zao.

Makundi haya mawili yanafananishwa tena na:- Ngano na Magugu; Kondoo na Mbuzi; Wana wa nuru na Wana wa Giza; na Wenye Muhuri wa Mungu na Wenye alama ya Mnyama.

Kuhusu Mihuri ndiyo kiini cha somo hili. Yesu atakapokuja kutakuwapo na makundi mawili kundi la kwanza ni la wale wenye muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao na kundi la pili ni wale wenye muhuri au alama ya mnyama katika vipaji vya nyuso na viganja vya mikono yao ya kuume.
“Kunawezekana kuwepo matabaka mawili tu. Kila kundi limepigwa muhuri tofauti, ama muhuri wa Mungu aliye hai, au chapa ya mnyama au sanamu yake” MSM uk. 166

Muhuri hutumika kutofautisha, kutenga na kufanya kitu au mtu kuwa wa pekee. Wakati Yesu akibagua kondoo na mbuzi atakuwa akiangalia katika vipaji vya nyuso zetu kama kuna muhuri wake au hakuna.

Muhuri hutumika kuelezea mamlaka au utawala na cheo cha mtu fulani. Hivyo kwa muhuri tulionao tunajibainisha ya kuwa sisi tupo chini ya mamlaka ipi au tunatawaliwa na mtawala gani aidha Mungu wa mbinguni au shetani.
Muhuri wa Mungu.

Muhuri wa Mungu maana yake ni “Kutulia katika ukweli, kiakili na kiroho kiasi kwamba hawawezi kuyumbishwa”. MSM uk.169, 4BC 1162 (1902). Mara tu watu wa Mungu wanapotiwa muhuri katika vipaji vya nyuso zao Pepeto litakuja ambao umeshaanza tayari.

Muhuri wa Mungu unafananishwa na alama ya damu ya mwanakondoo iliyowekwa Seal of God 2katika miimo ya milango ya nyumba za waebrania usiku ule kabla ya kutoka Misri ili kuwahifadhi dhidi ya maangamizi ya jumla.
“Alama inawekwa juu ya kila mmoja wa watu wa Mungu, kwa hakika ni kama vile alama iliyowekwa juu ya milango ya makazi ya waebrania ili kuwahifadhi watu dhidi ya maangamizi ya jumla.” MSM uk. 170

Hivyo wakati wa maangamizi ya mwisho, malaika watazuiwa wasiwadhuru watu waliotiwa muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao. Ezekieli 9:6.

Muhuri wa Mungu hauonekani kwa macho ya kibinadamu. Ni ishara ya ushindi juu ya dhambi yote…muhuri wa Mungu ni alama inayowatambulisha watu wa Mungu kuwa wake. Kutiwa katika vipaji vya nyuso zao huonesha kuwa ni katika tabia. Nguvu inayotia muhuri ni Roho Mtakatifu, Waefeso 4:30; Ufunuo, uk. 48.

Muhuri wa Mungu pia humaanisha utunzaji wa Sabato ya siku ya saba ya juma kikamilifu. Maana amri ya nne juu ya utunzaji wa Sabato ndiyo pekee yenye muhuri wa Mungu maana ndiyo kipimo cha uaminifu wetu kwa Mungu, muumbaji, mkombozi na mtakasaji wetu.

Ezekieli 20:12
“Tena naliwapa Sabato zangu , ziwe ishara (Muhuri) kati ya mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi Bwana ndimi niwatakasaye.”
“Uadhimishaji wa ukumbusho wa Bwana, Sabato iliyoanzishwa katika edeni, Sabato ya siku ya saba, ndiyo kipimo cha uaminifu wetu kwa Mungu.” Letter 94, 1900.

Sifa Za Watu Wanaowekwa Muhuri Wa Mungu.
Ili kutiwa muhuri wa Mungu katika kipaji cha uso wako ni lazima:-
Kushika kwa makini Sabato ya Bwana
“Muhuri wa Mungu aliye hai unawekwa juu ya wale ambao kwa makini wanaitunza Sabato ya Bwana…wale ambao wangependa kuwa na muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao lazima watunze Sabato ya amri ya nne” MSM uk. 169
Kufanana na Kristo kitabia. “Muhuri wa Mungu aliye hai utawekwa juu ya wale tu wanaofanana na Kristo kwa tabia”. 7BC 790 (1895)
“Wale wanaopokea muhuri wa Mungu aliye hai na wanalindwa katika wakati wa taabu lazima waakisi sura ya Yesu kikamilifu” EW 71 (1851)
Kushinda ulimwengu, tamaa za mwili na yule mwovu.
“Wale watakaoushinda ulimwengu, tama za mwili, na yule mwovu, ndio watakaopata upendeleo maalumu wa kupokea muhuri wa Mungu aliye hai.” TM 445
Kutenda kazi ya Mungu. “Wale wanaompenda Mungu, wanao muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao, na hutenda kazi ya Mungu.” SD 51

seal of God 3Je, Muhuri Wa Mungu Utapigwa Wakati Gani?
Ufunuo 7:1-4,
“Baada ya hayo nikaona malaika wanne wamesimama katika pembe nne za nchi, wakizizuia pepo nne za nchi, upepo usivume juu ya nchi, wala juu ya bahari, wala juu ya mti wo wote. Nikaona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini”

Tukio hili la kutia muhuri watumwa wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao linatokea kati ya kufunguliwa kwa muhuri wa sita na wa saba yani karibu na marejeo ya Yesu mara ya pili lakini baada ya tukio la kuanguka kwa nyota za mbinguni katika mihuri ya sita mwaka 1833 usiku wa Novemba 13 ambapo nyota zilianguka kama vile mti upukutishavyo mapooza.

Neno “Upepo” katika unabii humaanisha mashindano, vita na machafuko kati ya mataifa. Yeremia 25:32. Machafuko, vita na mashindano hayo huzuia maendeleo ya kazi ya Mungu miongoni mwa wanadamu. Wakati pepo nne zitakapo achiwa kutakuwa na machafuko makubwa sana, ndiyo vita ya Halmagedoni ya Ufunuo 16 hivyo Mungu amemtuma malaika wake kuzuia hadi atakapowatia muhuri watumwa waaminifu wake.

Wakati wa kutiwa muhuri wa Mungu kwa kuzingatia kipimo cha utunzaji wa Sabato ya siku ya saba umeanza tangu Yesu alipoingia katika chumba cha patakatifu pa patakatifu katika hekalu la mbinguni kuanzia mwezi wa saba 1844 hadi sasa. Wakati hukumu ya upelelezi inaendelea uamuzi unatolewa aidha kwajili ya uzima na wengine kwajili ya mauti. Wale wanaomkiri Yesu kama Bwana na mwokozi wao binafsi wakikuza uhusiano wao na Yesu kila siku wanatiwa muhuri wa Mungu katika vipaji vya nyuso zao.

“Niliona kuwa kipimo cha sasa kuhusu Sabato kisingeweza kuja mpaka uombezi wa Yesu katika patakatifu umemalizika naye amehama kuingia pazia la pili…kabla ya kuingia mlango wa patakatifu pa patakatifu…kwa sababu hawakuwa na nuru, na kipimo kuhusu sabato ambacho sasa tunacho tangu mlango ule ulipofunguliwa…
Shetani sasa anatumia kila mbinu katika wakati huu wa kutiwa muhuri kuzuia nia za watu wa Mungu dhidi ya ukweli wa sasa na kuwasababisha wayumbe.” EW 42,43.

Baadhi ya watu ambao wamekufa tayari wametiwa muhuri kwasababu walikufa katika Kristo.
“Niliona kuwa Bi. Hastings alikuwa ametiwa muhuri na angeinuka wakati wa sauti ya Mungu na kusimama juu ya dunia, na angekuwa pamoja na wale 144,000. Niliona kuwa hatuhiaji kuomboleza kwajili yake ; angepumzika wakati wa tabu.” 2 SM 263

Kuna wazee walio hai wenye umri mkubwa wametiwa muhuri katika vipaji vya nyuso zao kwa kuwa wanamwamini Mungu nathe mark of the beast wanapendwa na Mungu. Wazee hao watakuwa miongoni mwa idadi ambayo Bwana amesema “Heri wafu wafao katika Bwana”. MSM uk. 172

“Kazi ya malaika ya kuwatia muhuri watu wa Mungu ndiyo kazi muhimu inayotendeka sasa katika ulimwengu. Itatendeka mpaka katika kila taifa, jamii, lugha na kabila wafuasi wa kweli wa Mungu watakapokuwa wametiwa muhuri. Hakuna nguvu yoyote inayoweza kuzuia kukamilishwa kwa kazi hii…Malaika wanaendeleza kazi ya kuzuia pepo za vita katika ulimwengu kwa muda kitambo…huzuia pepo hizo ili kazi ya injili iweze kuendelea…Sasa ni wakati wa kupokea muhuri wa Mungu.” Ufunuo u.k 50-51

Alama ya Mnyama
Alama ya mnyama maana yake ni utunzaji au uadhimishaji wa siku ya Jumapili. TM 133.
“Wakati wa kupimwa utakapofika, itaoneshwa dhahiri kile ilicho chapa ya mnyama. Ni uadhimishaji wa Jumapili…
Ishara au muhuri wa Mungu umefunuliwa katika uadhimishaji wa Sabato ya siku ya saba, ukumbusho wa Bwana wa uumbaji…Chapa ya mnyama ni kinyume na hili, uadhimishaji wa siku ya kwanza ya juma.” MSM uk. 172

Alama ya mnyama itawekwa katika mkono wa kuume au katika vipaji vya nyuso. Ufunuo 13:16,
“Naye awafanya wote, wadogo kwa wakubwa, na matajiri kwa maskini, na walio huru kwa watumwa, watiwe chapa katika mkono wao wa kuume, au katika vipaji vya nyuso zao;”

Hii haimaanishi kwamba katika mkono itaandikwa alama hiyo au itaandikwa katika vipaji vya uso bali:-
1. Katika mkono wa kuume: kukubali kutofanya kazi za mikono siku ya Jumapili kama Sabato.
2. Katika vipaji vya nyuso: kukiri bila budi kwamba Jumapili ni Sabato. MSM 173

Je, Alama ya Mnyama Itapigwa Wakati Gani?
666_mark_of_the_beastWakati wa kupigwa na kupokea alama ya mnyama bado haujafika. Utunzaji wa Jumapili kwa sasa si alama ya mnyama.
“Hakuna ambaye tayari amekwishapokea chapa ya mnyama…uadhimishaji wa Jumapili bado siyo chapa ya mnyama, na haitakuwa hadi amri kuu imetolewa kuianubudu sanamu hii ya Sabato. Wakati utafika ambapo siku hii itakuwa ndicho kipimo, lakini wakati huo bado haujafika” MSM 173

Wakati mtu anapopata nuru juu ya amri kumi za Mungu na utunzaji wa Sabato lakini anaendelea kutotii atapokea alama ya mnyama. Ni wale ambao wanaendelea katika uasi baada ya kufahamu nuru ya mbinguni ndio watapokea alama ya mnyama.
“Wote ambao watabakia kuwa wakweli kwa Mungu na Sabato watapokea muhuri wa Mungu, huku mtu yeyote atakayeacha Sabato, au wote ambao wataendelea kuadhimisha Jumapili baada ya kuufahamu ukweli watapokea alama ya mnyama”. Maranatha, uk. 164

UBATIZO WA KWELI

Ev. Mujaya MujayaNa. Ev. Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122 and +255768678122

Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version: UBATIZO WA KWELI

Huenda hujawahi kujiuliza swali hili kuwa ubatizo wa kweli ni upi? Ni kwanini kuna aina nyingi za ubatizo; yaani ubatizo wa maji mengi au maji machache? Au wa watu wazima au watoto?

Labda nianze na Waefeso.4:5, “Bwana mmoja, imani moja, na ubatizo mmoja”. Biblia inasema kuna AINA MOJA TU ya ubatizo nami napenda tuuangalie kwa undani. Na katika kuangalia aina hii ya ubatizo tutaangalia mambo muhimu ya kuzingatia katika ubatizo ili uwe wa kweli. Ujuzi ambao utawezesha kulinganisha na ubatizo unaoufahamu kwa kuupima kwa kipimo cha maandiko matakatifu ya kuwa niwa ukweli au uwongo.

Mambo ya kuzingatia katika ubatizo wa kweli ni:-

  1. ANAYEBATIZWA ANAPASWA AAMINI, ATUBU NA AUNGAME DHAMBI.
    Ubatizo wa kweli unapaswa kutanguliwa na mambo makubwa manne ambayo ni Kuamini, Kutubu na Kuungama. Marko.16:16, “AAMINIYE na KUBATIZWA ataokoka“; Mathayo.3:6, inasema “naye AKAWABATIZA katika Mto yordani, huku WAKIZIUNGAMA DHAMBI zao” Matendo.2:38, “TUBUNI MKABATIZWE kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo”.John baptizing
  2. MBATIZAJI NA MBATIZWA WOTE WANAINGIA NDANI YA MAJI.

Wakati Filipo anambatiza Towashi Biblia inasema, Matendo.8:38 Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Hili ni jambo la muhimu sana, mbatizwa na anayebatizwa wote walikuwa ndani ya maji. Na baada ya ubatizo “…walipopanda kutoka majini…” Matendo.8:39 towashi akaondoka akifurahi. Katika aya hii tunaona jambo la muhimu pia sambamba na mbatizwa na mbatizaji kuwa ndani ya maji, ni kwamba lazima kuwepo na maji mengi.

  1. NI WAKUZAMISHWA KATIKA MAJI MENGI.

Yohana mbatizaji kipindi cha Yesu alikuwa akibatiza katika sehemu iliyokuwa inaitwa Ainoni maana kulikuwa na maji tele, Yohana 3:23 “Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa.” Yesu alibatizwa katika mto Yordani, na baada ya ubatizo Mathayo.3:16-17, …mara akapanda kutoka majini; na tazama, mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;na tazama, sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.” Mungu hupendezwa nasi kama alivyopendezwa na Yesu tunapotoka katika maji ya ubatizo maana ndivyo inavyotupasa kuitimiza haki yote (Mathayo.3:15) na Yesu alitupatia kielelezo. Lakini pia hutupatia Roho Mtakatifu kama vile hua alivyoshuka kwa Yesu ili atukamilishe kwa kutupatia tabia inayofanana na Yesu, ushindi wa dhamdi na atuongoze na atutie katika kweli yote.

Hivyo mambo haya matatu yanatosha kutuambia ubatizo wa kweli wa Biblia. Ubatizo wa watoto wachanga haufundishwi katika Biblia na wala hatuna mfano wa mtu yeyote tangu MWANZO hadi UFUNUO aliyebatizwa hivyo. Maana mtoto hawezi kuamini, akaungama na kutubu ili abatizwe.
Pia ubatizo wa kunyunyiza maji kichwani hauna msingi katika Biblia maana haufundishwi katika Biblia bali ni utaratibu ambao umewekwa na wanadamu tu.

Hebu leo turudi katika ubatizo wa kweli maana Yesu anakwambia “amini amini nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu.” Yohana.3:5.

Bwana akubariki sana unapoamua kufanya matengenezo katika jambo hili.

Kwa maoni, maswali au ushauri usisite kuwasiliana nasi.