NAMNA YA KUJUA FAIDA UNAYOIPATA KATIKA BIASHARA

Ev. Mujaya Mujaya

Ev.
Mujaya Mujaya

Na Ev. Mujaya Mujaya

Simu: +255715678122 au +255768678122

Barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version:Namna Ya Kujua Faida Unayoipata Katika Biashara Yako

Wafanya biashara wengi hawajui faida wanayoipata kutoka katika kila bidhaa wanayouza. Biashara inaendeshwa kwa ujumla tu bila ya ufahamu wa mchango wa kila bidhaa katika faida ya jumla anayoipata ndani ya biashara.

Faida ya kujua faida ya kila bidhaa inayouzwa, humsaidia mfanya biashara kufahamu bidhaa anayotakiwa kuuza zaidi ili kuongeza kiasi cha faida. Kwa upande mwingine hasara ya kutojua mchango wa kila bidhaa katika biashara humfanya mfanya biashara aenende kwa giza tu bila kujua bidhaa gani inampa faida na kadhalika ipi inampatia faida kidogo.

Kwa mfano, mfanya biashara anayeuza duka la mahitaji madogomadogo ya nyumbani utakuta dukani ameweka kwa mfano, sabuni, mafuta ya kula, mafuta ya taa, vocha, soda, sharubati, maji, unga, mchele, dawa za meno, n.k Lakini ukimuuliza je, ni bidhaa gani inakupatia faida kubwa kuliko zote hajui na atabaki anashangaa tu. Wakati mwingine mfanya biashara anaweza akajibu kwa kutumia uzoefu wake wa biashara lakini jibu atakalokupatia linaweza lisiwe sahihi.

JE, UTAFANYAJE?

Hatua kwa hatua za kutambua/kujua faida ambayo mfanya biashara hupata kutoka kwa kila bidhaa. Au kwa lugha nyingine ni mchango wa kila bidhaa katika faida ya jumla ya biashara.

  1. TUNZA KUMBUKUMBU ZA MAUZO NA MANUNUZI

Ni jambo la mhimu na maana sana kwa mfanya biashara kutunza kumbukumbu zake za manunuzi na mauzo ya bidhaa zake. Kwa kila bidhaa lazima kumbukumbu zitunzwe juu ya bei ya kununulia na bei ya kuuzia pamoja na idadi ya bidhaa zote zilizonunuliwa au kuuzwa. Pia ili kuwa na uhakika wa biashara mfanya biashara atatunza kumbukumbu ya tarehe alizonunua au kuuza kila bidhaa.Accounting-vacancies

  1. KOKOTOA FAIDA KWA KILA BIDHAA.

Kwa kawaida ili kukokotoa faida, unachukua bei ya kuuzia unatoa bei ya kununulia bidhaa. Faida ni kile kiasi kinachobaki baada ya kutoa bei ya kununulia toka katika bei ya kuuzia.lakini faida hii haitupatii picha nzuri au halisi ya biashara maana haioneshi faida hiyo ni asilimia au sehemu gani ya bei ya kununulia/gharama ya bidhaa. Ili kupata kiasi cha faida ya kila bidhaa utatumia kanuni rahisi ifuatayo:-Bei ya kuuzia kila bidhaa toa bei ya kununulia kila bidhaa jibu utalopata gawanya kwa bei ya kununulia kila bidhaa kisha jibu lako zidisha kwa 100%. Yani Bei ya kuuzia – Bei ya kununulia/Bei ya kununulia X 100%

Jibu utakalolipata hapo juu litakuonesha kiasi cha faida kwa asilimia ambacho kila bidhaa huchangia katika faida ya jumla ya biashara. Mfanya biashara ikiwa akitaka kuanza kuuza aina mpya ya bidhaa, atazingatia bidhaa yenye kiasi kikubwa cha faida ukilinganisha na bidhaa nyingine lakini atafanya hivyo baada ya kuzingatia pia vihatarishi vingine vya biashara.

Mfano: katika biashara ya duka la mahitaji madogomadogo ya nyumbani, mfanya biashara alinunua na kuuza bidhaa zake kama ifuatavyo:-

Na. Bidhaa Bei ya kununulia (A) Bei ya kuuzia (B) Faida = (B-A)/A * 100%
1 Sabuni (mche)             750.00        1,000.00                   33.33
2 Sukari (1 KG)          1,800.00        2,100.00                   16.67
3 Unga (1 kg)             450.00           700.00                   55.56
4 Mafuta ya kula (1 Lita)          1,200.00         1,600.00                   33.33
5 Vocha             950.00         1,000.00                    5.26

Katika mfano huu, Unga ukifuatiwa na mafuta na sabuni ndiyo yenye faida kubwa ukilinganisha na bidhaa nyingine. Hivyo kwa kuzingatia vihatarishi mbalimbali vya biashara na aina ya biashara, mfanya biashara ataongeza mauzo ya unga, sabuni na mafuta ili kuongeza faida yake maana ndizo bidhaa zinazochangia asilimia kubwa katika faida yake.

FAIDA YA JUMLA/WASTANI YA BIASHARA YOTE

Ili kujua faida ya jumla ya biashara yote, mfanya biashara atatumia kanuni rahisi ifuatayo:-

Faida ya jumla/wastani = Mauzo kwa mwezi – Gharama za manunuzi ya mwezi/Gharama za

manunuzi ya mwezi X 100%

Faida hii inatumika kufananisha mchango wa kila mradi baina ya aina mbili au zaidi ya miradi. Kwa

Unaweza Ukajua Faida Halisi ya Mradi Wako

Unaweza Ukajua Faida Halisi ya Mradi Wako

mfano: mfanya biashara ana biashara zaidi ya moja. Mfanya biashara anaweza akawa na duka la mahitaji madogomadogo ya nyumbani lakini wakati huo huo anaduka la kuuza nguo au vifaa vya ndani ya nyumba n.k

Hivyo kwa kanuni tajwa hapo juu, anaweza akajua ni biashara gani kati ya zote anazozifanya inampatia faida kubwa zaidi ya nyingine. Lakini pia ikiwa mfanya biashara ana mtaji na anajiuliza awekeze katika mradi/biashara ipi ambayo itampatia faida kubwa, inashauriwa kwamba akokotoe faida ya wastani ya biashara yote wa kila pendekezo la wazo la biashara alilonalo na kishaachague biashara yenye wastani mkubwa wa biashara yote baada ya kuzingatia vihatarishi vingine vya biashara.

Zingatia mfano ufuatao: Mfanya biashara baada ya kuangalia kumbukumbu zake za mauzo na manunuzi anatambua

Taarifa kutoka katika duka la mahitaji madogomadogo ya nyumbani ilikuwa kama ifuatavyo:

Na. Bidhaa Wastani wa idadi ya bidhaa zinazouzwa kwa mwezi Bei ya kununulia kila bidhaa moja Gharama ya bidhaa zilizouzwa Bei ya kuuzia bidhaa moja Mauzo kwa mwezi Faida ya kila bidhaa
A B AXB C AXC  c-B/B*100%
 01.  Mchele  1,000 KG  540  540,000  600  600,000  11.11%
 02.  Unga  1,000 KG  200  200,000  220  220,000  10%
 03.  Sukari  500 KG  500  250,000  540  270,000  8%
 04.  Mafuta  500 Litre  1,100  550,000  1,400  700,000  27.27%
 1,540,000  1,790,000
Faida Wstn 16.23%

Taarifa kutoka katika duka la nguo ilikuwa kama ifuatavyo:

Na. Bidhaa Wastani wa idadi ya bidhaa zinazouzwa kwa mwezi Bei ya kununulia kila bidhaa moja Gharama ya bidhaa zilizouzwa kwa mwezi Bei ya kuuzia bidhaa moja Mauzo ya bidhaa kwa mwezi Faida ya wastani
 A  B  AXB  C  AXC  C-B/B*100%
1 Suti 8 20,000 160,000 40,000 320,000 100%
2 Blauzi 22 7,500 165,000 15,000 330,000 100%
3 Magauni 10 20,000 200,000 25,000 250,000 25%
4 Mashati 25 8,000 200,000 15,000 375,000 87.50%
5 Viatu 30 8,000 240,000 14,000 420,000 75%
965,000 1,695,000
Faida Wastani                      75.65

Kutokana na taarifa hizo hapo juu, utagundua kwamba duka la nguo linampatia faida kubwa sana ukilinganisha na duka la mahitaji madogomadogo ya nyumbani. Hivyo mfanya biashara anashauriwa kuwekeza mtaji mkubwa katika duka la nguo kuliko duka la mahitaji madogomadogo ya nyumbani

Anza sasa kukokotoa faida inayopatikana katika kila bidhaa unayouza ili upate mwanga wa mchango wa kila bidhaa katika faida ya jumla ya biashara. Kama una swali, maoni au ushauri tafadhali wasiliana name kwa mawasiliano yafuatayo:

Simu: +255715678122, +255768678122

Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s