Kundi Jipya la Kanisa Laanzishwa!!!! Watu 13 Wabatizwa!!!

Na Mujaya Mujaya

Kundi jipya la Mongwe Kariakoo limeanzishwa baada ya mkutano mkubwa wa injili kufanyika katika kijiji cha Mongwe Kariakoo, mkutano ambao uliendeshwa kwa ushirikiano kati ya Kanisa la Waadventista wa

Muinjilisti Emmanuel Samwel

Muinjilisti Emmanuel Samwel

Sabato Mzumbe na TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe. Mhutubu katika mkutano huo alikuwa muinjilisti Emmanuel Samwel(katika picha kulia) kutoka TUCASA Mzumbe ambaye pia ni mhudumu wa ShareHope Ministries. Mkutano huo uliendeshwa kwa muda wa majuma mawili na kushuhudia watu kumi na tatu(13) wakimkubali Yesu kama Bwana na mwokozi wao binafsi na kubatizwa kwa maji mengi kama tangazo au uthibitisho wa imani hiyo.

Tangu mwaka 2013 kumekuwa na jitihada za TUCASA Chuo Kikuu Mzumbe kufungua kazi ya Mungu katika jamii za kutoka safu za milima ya uluguru mkoani Morogoro. Mwaka 2013 kundi la Peko Misegese lilianzishwa ambalo hadi leo linaendelea vizuri kwa kuhudumiwa na muinjilisti mlei ambae anahudumia kundi la Mongwe pia. Washiriki na waumini wote kutoka Peko na Mongwe hukusanyika sehemu moja kila Sabato kwajili ya ibada ya pamoja na kutiana joto la kiroho.

Mwaka 2014 TUCASA Mzumbe walielekeza juhudi zao katika kundi kongwe la kanisa la Mzumbe SDA lililopo Tangeni lakini mwaka huu(2015) jitihada zilipelekwa Mongwe ambalo ni eneo jipya.

Mungu aibariki kazi yake katika safu ya milima ya Uluguru. Tuendelee kuombea maendeleo ya kazi ya Mungu katika nchi ya Tanzania na ulimwengu kwa ujumla.

Muinjilisti Emmanuel Sanwel akitoa hutuba kuu za mkutano ambazo ziligusa sana maisha ya watu wa Mongwe Kariakoo.

Muinjilisti Emmanuel Sanwel akitoa hutuba kuu za mkutano ambazo ziligusa sana maisha ya watu wa Mongwe Kariakoo.

Ibada ya kufunga mkutano ilihudhuriwa na watu wengi sana

Ibada ya kufunga mkutano ilihudhuriwa na watu wengi sana

Kwaya ya TUCASA Mzumbe ikimtukuza Mungu kwa njia ya wimbo ambao uliwaandaa wana mkutano kukutana na Mungu katika Neno la Uzima.

Kwaya ya TUCASA Mzumbe ikimtukuza Mungu kwa njia ya wimbo ambao uliwaandaa wana mkutano kukutana na Mungu katika Neno la Uzima.

Miss Rebeka Mchome akiendesha kipindi maalumu cha watoto katika mkutano(watoto hao hawakuwa wakiadventista lakini Mungu aliwaongoza kufanya vipindi vya pekee sana kwa utukufu wa jina lake).

Miss Rebeka Mchome akiendesha kipindi maalumu cha watoto katika mkutano(watoto hao hawakuwa wakiadventista lakini Mungu aliwaongoza kufanya vipindi vya pekee sana kwa utukufu wa jina lake).

Njoo! Njoo! Njoo! Unakawilia nini? Tazama kile ambacho Yesu amekifanya kwa ajili ya maisha yako!!! Njoo leo Njoo sasa usikawie. Wito wa pekee kuwainua wana mkutano wamtazame Yesu na kumfuata.

Njoo! Njoo! Njoo! Unakawilia nini? Tazama kile ambacho Yesu amekifanya kwa ajili ya maisha yako!!! Njoo leo Njoo sasa usikawie. Wito wa pekee kuwainua wana mkutano wamtazame Yesu na kumfuata.

Wana mkutano wakisimama baada ya kuitikia wito wa kumkabidhi Mungu maisha yao

Waliojitoa kwa ubatizo wakisimama tayari kwa kuapishwa na kungoja zoezi la kihistoria maishani mwao la ubatizo wa maji mengi kama vile Yesu alivyobatizwa

Waliojitoa kwa ubatizo wakisimama tayari kwa kuapishwa na kungoja zoezi la kihistoria maishani mwao la ubatizo wa maji mengi kama vile Yesu alivyobatizwa

Wabatizwa wakiwa mbele ya umma wa wanamkutano kwajili ya kuthibitishwa na kukili imani yao kwa Yesu kabla ya ubatizo

Wabatizwa wakiwa mbele ya umma wa wanamkutano kwajili ya kuthibitishwa na kukili imani yao kwa Yesu kabla ya ubatizo

Mashuhuda wa ubatizo wakiwa pembezoni mwa mto wakati ubatizo ukiendelea

Mashuhuda wa ubatizo wakiwa pembezoni mwa mto wakati ubatizo ukiendelea

Ubatizo ulifanyika ambapo watu kumi na tatu(13) walitoa maisha yao na kumkili kwa njia ya ubatizo

Ubatizo ulifanyika ambapo watu kumi na tatu(13) walitoa maisha yao na kumkili kwa njia ya ubatizo

SAM_3262 SAM_3235

Muinjilisti Basilio Maliwanga akitoa Neno La Uzima kwa waumini wa kundi la Peko na Mongwe katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika kundi la Peko Misegese.

Muinjilisti Basilio Maliwanga akitoa Neno La Uzima kwa waumini wa kundi la Peko na Mongwe katika ibada ya pamoja iliyofanyika katika kundi la Peko Misegese.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in News

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s