MAANDALIZI YA SOYA YA CHAI, MAZIWA NA NYAMA

Evangelist Mujaya Mujaya

Evangelist Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti Mujaya Mujaya

Simu Namba: +255768678122 au +255715678122

Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: MAANDALIZI YA SOYA YA CHAI, NYAMA NA MAZIWA

Soya ni nafaka iliyopo katika jamii ya mikunde. Soya ni muhimu sana katika kujenga afya ya mwanadamu kwa sababu ya utajiri wa virutubisho vya chakula ndani yake. Bidhaa zinazotoka katika soya niza kichumi maana mtumiaji au mtengenezaji hatatupa kitu hata kimoja. Mabaki yanayopatikana ni mali ya kutengeneza vitu vingine kama tutakavyoona. MAHITAJI: Soya 2kg na robo; Malimao 10; Mafuta ya kupikia lita 1; Kifaa cha kusagia au kutwangia; na chekecheo au chujio. SOYA YA CHAI Anza kwa kuchambua soya yako robo kilo kuondoa mawe, nafaka zisizohitajika na soya zilizoharibika. Kisha loweka soya yako kwa masaa 24 yani kwa mfano umeloweka leo saa 1 asubuhi, iache hadi kesho saa 1 asubuhi. Kuloweka soya kunasaidia kuondoa sumu zote zilizomo ndani yake. Baada ya saa 24 kupita chukua soya yako ianike hadi itakapokauka vizuri. Soya ikiisha kauka ikaange bila mafuta kwa moto wa taratibu mpaka itakapobadilika rangi na kuwa rangi ya kahawia. Soya hii pia kwa kuweka chumvi kama vile unavyoandaa karanga za kutafuna unaweza kula baada ya kuzikaanga hivyo hivyo maana ni tamu sana kuliko hata karanga. Epua soya yako kisha itwange katika kinu kisafi hadi itakapolainika kama unga. Wengine wanatumia blenda kusaga soya vizuri na kwa wepesi zaidi. Baada ya kumaliza chekecha kuondoa mabaki ya soya ambayo hayakutwangika vizuri kasha itunze soya yako katika chombo kisafi na kikavu mahali salama. Sasa soya yako kwajili ya matumizi ya chai yatakuwa tayari. Soya hii unaweza kuitumia kama mbadala wa majani ya chai na kahawa vitu ambavyo vinadhuru afya

Soya Ikikaangwa kwa Moto wa Taratibu

Soya Ikikaangwa kwa Moto wa Taratibu

zetu. Unaweza kutumia katika maziwa, chai na uji. Katika kutumia weka soya ya kutosha (kijiko cha chakula katika kikombe 1 cha chai), maana kwa kadili unavyoitumia ndivyo unavyopata manufaa zaidi. FAIDA ZA SOYA YA CHAI

  1. Soya huwafaa sana wenye matatizo ya shinikizo la damu. Kama mtu ana shinikizo la damu ni vema akatumia soya kama kinywaji maana huweka mapigo ya moyo katika hali ya msawazo. Wakati mtu mwenye mapigo ya moyo ya kupanda hashauriwi kabisa kutumia majani ya chai au kahawa, hivyo kinywaji cha soya ni suluhisho kwake na mbadala sahihi.

Kwa mtu mwenye shinikizo la damu la kushuka anapaswa kutumia soya maana itaweka mapigo ya moyo katika hali ya kawaida. Kunywa majani ya chai au kahawa kunapandisha mapigo ya moyo na ikiwa ataendelea kutumia vinywaji hivi basi moyo huzoea; na siku mapigo ya moyo yakishuka anapata shida na kuingia gharama kubwa kununua madawa ya ghali sana ili kupandisha mapigo ya moyo. Hivyo namshauri kwamba atumie kinywaji cha soya ili siku mapigo ya moyo yakishuka anaweza akatumia sasa majani ya chai au kahawa kama dawa tu ili kupandisha mapigo ya moyo.

  1. Matatizo ya vidonda vya tumbo. Matumizi ya soya ya chai ni rafiki kwa mazingira ya tumbo kutokana na kufanya kazi vema katika mazingira ya tindikali ya tumbo.
  2. Gharama ndogo. Maandalizi ya soya ya chai ni rahisi na hugharimu kiasi kidogo tu cha fedha huku yakikuhakikishia manufaa mengi sana kiafya. Soya robo kilo (250mg) inakupatia pia soya ya chai robo kilo (250mg) pia, hivyo hakuna kinachopotea na waweza kuitumia kwa muda mrefu sana.

MAZIWA YA SOYA Anza kwa kuchambua soya yako 2KG (Kilo 2) ili kuondoa mawe, nafaka zisizohitajika na soya zilizoharibika. Kisha osha na loweka soya yako kwa masaa 24 yani kwa mfano umeloweka leo saa 1 asubuhi, iache hadi kesho saa 1 asubuhi. Baada ya saa 24 kupita twanga soya yako kwa kutumia kinu au blenda mpaka itakapolainika vizuri. Hakikisha chombo unachotwangia ni kisafi kabisa ili maziwa yasichafuke na kupunguza thamani yake. Kisha changanya soya ulizozitwanga na maji safi na salama lakini zingatia kutochanganya maji mengi sana hata maziwa yako yakawa mepesi sana.

Maziwa Yakiwa Tayari Kwa Kuchujwa

Maziwa Yakiwa Tayari Kwa Kuchujwa

Baada ya kuchanganya maji na soya uliyoitwanga, chuja kwa kutumia kitambaa cheupe kisafi chenye nafasi ndogo sana ili kuzuia chembechembe za soya kupenya. Hapo utakuwa umepata maziwa ya soya. Mabaki ya soya uliyokamua yanaweza kutumika kutengeneza bagia kwa kuyachanganya na viungo na unga wa ngano kidogo kwajili ya kushikiza bagia zako. Au unaweza kutumia kama chakula cha ziada kwa kuku kama mbadala wa dagaa au uduvye. Kisha chemsha maziwa yako hadi yaive kabisa. Ikumbukwe kwamba maziwa ya soya yana tabia sawa na maziwa mengine ya wanyama katika utaratibu wa kuyaandaa. Hivyo katika kuchemsha maziwa ya soya, weka chombo chini ya sufuria au chungu chako ili kuepuka kuganda kwa maziwa katika sufuria au chungu na kufulumia kwa maziwa. Yakishachemka na kuiva vizuri unaweza kuyatumia kwa chakula au kwa kitafunwa chochote. Unaweza kuongeza soya ya chai kama unataka upate chai ya maziwa. Ili unufaike sana na maziwa haya basi tumia asali badala ya sukari. FAIDA YA MAZIWA YA SOYA 1.Maandalizi rahisi kwa unafuu mkubwa. Matumizi ya maziwa ya soya yanakulahisishia gharama za kupata maziwa mengi kwa mahitaji yako ya nyumbani maana kwa 2kg za soya unaweza ukapata maziwa zaidi ya lita 10.

  1. Utajiri wa virutubisho vya chakula. Maziwa ya soya yana mchango mkubwa kwa mtumiaji kwani yamesheeni virutubisho vyote vilivyopo hata katika maziwa ya wanyama lakini faida yake kubwa zaidi ya maziwa ya wanyama, maziwa ya soya hayana mafuta ya lehemu yanayoganda na kudhuru mwili wa mtumiaji. Maziwa ya soya hayana pia vimelea vya magonjwa mbalimbali vilivyomo ndani ya maziwa ya wanyama.
  2. Watoto wadogo. Maziwa ya soya yana mchango mkubwa katika ukuaji wa watoto wadogo bila kujali umri wa mtoto. Kwa wale watoto ambao wameachishwa ziwa la mama kwa sababu mbalimbali kama kifo, magonjwa, kutengana n.k wanaweza wakakua vizuri kwa kutukia maziwa ya soya kuliko aina yoyote ile ya maziwa. Maziwa ya soya ni mdabala na jibu sahihi kwa mahitaji yako ya maziwa.
  3. Yanaweza yakaganda na kuwa mtindi. Ikiwa mtumiaji atataka apate mtindi basi atayachukua maziwa ya soya baada ya kuchemshwa, kuiva vizuri na kupoa katika chombo cha kugandishia maziwa nayo yataganda kwa utaratibu uleule kama yagandishwavyo maziwa ya wanyama. Kisha waweza kuyatumia kwa chakula chochote.

NYAMA YA SOYA Anza kwa kuchambua soya yako 2KG (Kilo 2) ili kuondoa mawe, nafaka zisizohitajika na soya zilizoharibika. Kisha osha na loweka soya yako kwa masaa 24 yani kwa mfano umeloweka leo saa 1 asubuhi, iache hadi kesho saa 1 asubuhi. Baada ya saa 24 kupita twanga soya yako kwa kutumia kinu au blenda mpaka itakapolainika vizuri. Kisha changanya soya ulizozitwanga na maji safi na salama lakini zingatia kutochanganya maji mengi sana hata

Mama Akimnywesha Mwanae Maziwa Ya Soya

Mama Akimnywesha Mwanae Maziwa Ya Soya

maziwa yako yakawa mepesi sana. Baada ya kuchanganya maji na soya uliyoitwanga, chuja kwa kutumia kitambaa cheupe kisafi chenye nafasi ndogo sana ili kuzuia chembechembe za soya kupenya. Hapo utakuwa umepata maziwa ya soya. ZINGATIA: Usitupe mabaki ya soya baada ya kuchuja maana ni mali. Rejea utengenezaji wa maziwa ya soya. Kisha chemsha maziwa yako hadi yaive kabisa. Ikumbukwe kwamba maziwa ya soya yana tabia sawa na maziwa mengine ya wanyama katika kuyaandaa. Hivyo katika kuchemsha maziwa ya soya, weka chombo chini ya sufuria au chungu chako ili kuepuka kuganda kwa maziwa katika sufuria au chungu na kufulumia kwa maziwa. Maziwa yakishaiva, kamua malimao 10 na kisha weka maji ya malimao katika maziwa. Wingi wa malimao utategemea wingi wa maziwa yaliyopo. Ukishaweka maji ya malimao katika maziwa utaona yakiganda na kufanya mabongemabonge. Maziwa yashakiganda au kuweka mabongemabonge, yachuje tena kwa kukamua kutumia kitambaa cheupe ili kutenganisha maji na mabonge uliyoyapata. Kamua kwa nguvu upate kitu kigumu chenye umbo la mpira au duara. Tumia kisu kukata mduara wako, ukubwa wa vipande na umbo kama utakavyopenda. Ukishapata vipande vyako vikaange katika mafuta ili kuvipa rangi ya nyama na kuvifanya vidumu kwa muda mrefu. Ukishavikausha katika mafuta unaweza ukaviunga kwa kadili upendavyo kwa kadili ya matumizi yako. FAIDA ZA NYAMA YA SOYA Mbadala sahihihi wa nyama za wanyama na ndege. Nyama ya soya ni mbadala sahihi maana zina virutubisho vyote muhimu, utamu na utoshelevu mkubwa. Nyama ya soya haina mafuta hatari yanayoweza kusababisha magonjwa hatari ya shinikizo la damu, sukari, kiharusi, homa za wanyama n.k Nyama ya soya inaweza ikatumiwa kwa chakula chochote kulingana na mahitaji ya mlaji. Unaweza ukaiandaa kwa urahisi na bei yake ni nafuu ukilinganisha na nyama za wanyama na ndege. Hivyo kwa watu wanaojali afya, furaha na uchumi wa familia zao, nyama ya soya ni mbadala sahihi kwa nyama za wanyama na ndege. Nyama ya soya ni tamu sana na rafiki wa familia yako, ukiikaribisha mezani mwako itakuletea afya, kukukinga na magonjwa, kulinda pesa yako na kukupa utamu wa pekee kwa utoshelevu wa chakula chako. Kwa maswali au maoni: Wasiliana nami; Ndg. Mujaya Mujaya 0715678122 ev.mujaya@gmail.com

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

2 comments on “MAANDALIZI YA SOYA YA CHAI, MAZIWA NA NYAMA

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s