JE, DESTURI YA YESU NA MITUME NI IPI?

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na. Muinjilisti: Mujaya Mujaya

Downloadable Version: Je, Desturi Ya Yesu Na Mitume Ni Ipi?

Desturi ni neno la Kiswahili linalomaanisha “jambo linalofanywa mara kwa mara”. Inafurahisha kuwa Biblia inazungumzia desturi ya Yesu ambayo kila mtu anatakiwa kuenenda vile vile kama Yesu, alivyoenenda. 1Yohana 2:6, Yeye asemaye ya kuwa anakaa ndani yake, imempasa kuenenda mwenyewe vile vile kama yeye alivyoenenda.” Yesu alitupatia kielelezo ili kama alivyoenenda nasi tupate kuenenda.

Katika Luka.4:16 inasema kama ilivyokuwa desturi ya Yesu “Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na SIKU YA SABATO akaingia katika sinagogi KAMA ILIVYOKUWA DESTURI YAKE, akasimama ili asome.” Hapa tunaona desturi ya Yesu ilikuwa kwenda katika nyumba ya ibada kila Sabato.

Yesu hakuvunja Sabato kamwe. Bali alisema, Mathayo.12:12, “..Basi ni halali kutenda mema siku ya Sabato.” Ni halali kutenda matendo mema ya lazima ya kuokoa maisha ya watu na kulegeza mizigo na masumbuko ya watu kama Yesu alivyofanya katika siku ya Sabato. Hivyo ni halali kuponya, kula, kutibu/kutibiwa, kutazama wagonjwa, wafungwa na mayatima n.k. Yesu ni Bwana wa siku ya Bwana (Ufunuo.1:10), Yesu ni Bwana wa Sabato(Marko.2:28).

Kwa kuwa dhambi ni uasi wa sheria(1Yohana.3:4), Yesu angekuwa ametenda dhambi kwa kuvunja Sabato; lakini Yesu hakuvunja sheria za Mungu. Yesu alisema katika, Yohana.15:10 “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; KAMA VILE MIMI NILIVYOZISHIKA AMRI za Baba yangu na kukaa katika pendo lake”. Pia Yesu alikataa kwamba alikuja kuzitangua sheria za Mungu ikiwemo Sabato, Mathayo.5:17,18 “msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie.” Yesu alisema hata mbingu zitakapoondoka nukta ya amri zake haitaondoka.Sermon of the Mount

Mitume nao wakiongozwa na Paulo baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu walikuwa na Desturi kama ya Yesu ya kupumzika siku ya Sabato, Matendo.17:2 “Na Paulo kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahojiana nao kwa maneno ya maandiko Sabato tatu,” Hivyo hapa tunaona Paulo akiwa na desturi kama ya Yesu kwenda katika nyumba ya ibada siku ya Jumamosi, akitoa hoja toka katika neno la MUNGU Matemdo.18:4. Biblia inasema pia, Matendo.16:13 “Siku ya Sabato tukatoka nje ya lango, tukaenda kando ya mto, ambapo tukadhani ya kuwa pana mahali pa kusali; tukaketi, tukasema na wanawake waliokutana pale.” Mafungu haya yanaonesha Sabato ilivyotunzwa baada ya kufa na kufufuka kwa Yesu (Luk.23:54-56, Matendo.13:14,27,43-44; 15:21; 18:4)

Kama haushiriki Sabato ya BWANA, Mungu wako karibu leo katika desturi hii ya Yesu na mitume ya kushika Sabato takatifu. Kamwe hawakufanya ibada siku tofauti na Sabato ya Jumamosi. Maana biblia inafundisha kuwa hadi mbinguni tutakapokwenda desturi hii itaendelea kuwepo, Isaya.66:22-23. “Kama vile mbingu mpya na nchi mpya, nitakazofanya……..Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na Sabato hata Sabato, wanadamu wote watakuja kuabudu mbele zangu, asema BWANA.”

 

Kwa maswali, maoni au ushauri tafadhali wasiliana nami: +255715678122 au +255768678122

Au barua pepe: ev.mujaya@gmail.com

Advertisements

One comment on “JE, DESTURI YA YESU NA MITUME NI IPI?

  1. Asante kwa somo ambalo linazidi kutupanulia uelewa wa biblia, ila kuna swali nakutana nalo mara kwa mara nikiwa na wenzangu katika kujadiliana maandalizi ya siku ya sabato, nimesoma vizuri na nimeona swala la kula pia ni halali katika siku ya sabato.Swali ni kwamba je kupika siku ya sabato ni dhambi?kama ndio je kwa wagonjwa na sehemu za joto wanashauriwa nini?Asante

    Like

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s