MATUMIZI YA VYAKULA VYA NYAMA

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya

Simu Namba: +255715678122

Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: MATUMIZI YA VYAKULA VYA NYAMA

Mpango wa awali wa chakula cha mwanadamu haukuwa ale vyakula vya nyama au vinavyotokana na wanyama mfano: nyama, maziwa, siagi, mafuta, mayai n.k Mpango wa Mungu tangu mwanzo ulikuwa mwanadamu ajishibishe kwa Nafaka. Kokwa, Matunda na Mbogamboga. Kwa muda zaidi ya miaka 2000 (Mileniamu 2) tangu uumbaji hadi baada ya gharika kinywa cha mwanadamu hakikuwahi kamwe kuonja radha ya chakula chochote kutoka kwa wanyama, samaki au ndege. Vyakula vya nyama havikuwa katika mpango wa awali wa Mungu kwa mwanadamu.

Baada ya gharika, dunia nzima iliangamizwa na hakukuwa na mche wowote wala matunda, nafaka wala mbogamboga na ndipo Mungu akaruhusu mpango wa dharula kumnusuru mwanadamu aliyemuumba kwa kumruhusu aanze kutumia vyakula vya nyama. Mwanzo 9:3, “Kila kiendacho kilicho hai 234kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.”

Wakati huo ambao mwanadamu aliruhusiwa atumie vyakula vya nyama, Mungu alitoa maelekezo kwamba damu na mafuta hayapaswi kutumika. Mwanzo 9:4, Walawi 3:17, 7:23 “Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile… Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa… Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yo yote, ya ng’ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi.” Nyama ziliruhusiwa kutumika kwa uangalifu mkubwa kwamba damu yote na mafuta yote yawe yamekaushwa kabisa.

Wakati wana wa Israeli wametoka nchi ya Misri kuelekea katika nchi ya ahadi Kanani, Mungu aliwapatia chakula chema sana, Mana kutoka mbunguni. Kutoka 16:31-35, “Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na tamu yake ilikuwa kama tamu ya maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali. Musa akasema, Hili ni neno Bwana aliloliamuru, Pishi moja ya kitu hicho na kiwekwe kwa ajili ya vizazi vyenu; ili kwamba wao wapate kukiona kile chakula nilichowalisha ninyi barani, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri. Basi Musa akamwambia Haruni, Twaa kopo, ukatie pishi moja ya hiyo Mana ndani yake, uiweke mbele ya Bwana, ilindwe kwa ajili ya vizazi vyenu. Kama vile Bwana alivyomwagizia Musa ndivyo Haruni alivyoiweka hapo mbele ya Ushahidi, ili ilindwe. Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arobaini, hata walipofikilia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikilia mipakani mwa nchi ya Kanaani.”K051

Kwa kutumia chakula hicho ambacho ni mpango wa Mungu wana wa Israeli walidumu jangwani siku zote licha ya jua kali wakati wa mchana, baridi kali wakati wa usiku, hatari zote za jangwani na vita mbalimbali walizopigama walidumu kuwa na afya njema siku zote. Kutoka 15:26, “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.” Sisi pia kama wasafiri kuelekea katika nchi ya ahadi ya mbinguni tunapaswa kuzingatia mpango wa Mungu wa chakula chetu.

Wakati fulani wana wa Israeli walijaribiwa wakamnung’unikia Mungu kwa chakula ambacho aliwapatia wakataka nyama na samaki ili wale kinyume na mpango wa Mungu wa chakula cha Mana, chakula kutoka mbinguni. Mungu akawaacha, wafate tama zao akawaletea kware ambao waliwasababishia madhara makubwa. Hesabu 11:4-10, 18-20, 32-33. “Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule? Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola… kabla ya kesho, nanyi mtakula nyama; kwa maana mmelia masikioni mwa Bwana, mkisema, Ni nani atakayetupa nyama, tule? Maana huko Misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo Bwana atawapa nyama, nanyi mtakula. Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala siku kumi, wala siku ishirini; lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hata hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa Bwana aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?… Watu wakaondoka mchana huo wote, na usiku huo wote, na siku ya pili yote, kuwakusanya hao kware; yeye aliyepata ya upungufu kuliko wenziwe alipata kiasi cha homeri kumi; nao wakawaanika wote kando-kando ya kambi kuizunguka pande zote. Kisha hapo hiyo nyama ilipokuwa ikali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira za Bwana ziliwaka juu ya watu, Bwana akawapiga watu kwa pigo kuu mno.”

Wasafiri wenzetu wakiwa njiani kuelekea katika nchi ya ahadi walitamani kula samaki na nyama maana kama tulivyo sisi leo tunaona ya kwamba chakula ambacho ni mpango wa Mungu kwa afya zetu hakifai na hivyo kufuata chakula cha nyama kukidhi tamaa zetu na tunaishia magonjwa makubwa ya ajabu ambayo tusingeyapata ikiwa tungerejea kupendezesha meza zetu kwa nafaka, matunda na mbogamboga.

Wakati Mungu aliporuhusu mwanadamu ale vyakula vya nyama pia alitoa mwongozo wa wanyama wa kuliwa na wasio wa kuliwa. Mungu muumbaji wetu na wa wanyama, ndege, samaki na wadudu hao aliona kwa hekima yake makundi yafaayo kutumiwa na mwanadamu ya wale yasiyofaa.

Nikukumbushe tena vyakula vya nyama viliruhusiwa baada ya gharika maana nchi yote ilikuwa imeharibiwa. Lakini kabla ya gharika, Mungu alimpatia maelekezo Nuhu juu ya namba ambayo wanyama wangeingia nR099dani ya safina kwamba wanyama wote walio safi (wasio najisi) waingie saba saba mme na mke na wanyama wachafu (najisi) waingie wawili wawili mme na mke lengo likiwa kuhifadhi mbegu ya nchi. Mwanzo 7:2-4, “Katika wanyama wote WALIO SAFI ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama WASIO SAFI wawili wawili, mume na mke.Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ILI KUHIFADHI HAI MBEGU JUU YA USO WA NCHI YOTE.”

Mgawanyiko na ufafanuzi huu wa wanyama safi na wachafu unapatikana katika Walawi 11 na Kumbukumbu 14. Mungu anasema wazi kwamba wanyama wanaopaswa kuliwa ni wale walio safi na wachafu hawapaswi kutumiwa kwa chakula na hata wakifa mizoga yao haipaswi hata kuguswa.

Ni kosa kubwa kudhani kwamba Yesu alimruhusu mwanadamu ale wanyama, ndege, samaki na wadudu wachafu. Kamwe Yesu aliye ufunuo wa Mungu hakuruhusu wala kupingana na mpango wa chakula wa Mungu, na hakuwafundisha watu na wanafunzi wake kukiuka mpango wa Baba yake. Baadhi ya mafungu ya Biblia yanayotumika kwa kupotosha ili kuhalalisha matumizi ya nyama chafu ambayo ni:-

  • Si kila kimuingiacho mtu kinamtia unajisi bali kitokacho
  • Kilichotakaswa na Mungu wewe usikiite najisi, chinja ule.

Tafiti mbalimbali za kisayansi zimeweka wazi kwamba vyakula vya nyama kutoka kwa wanyama, ndege, samaki na wadudu wachafu vimebeba vimelea vingi sana vya magonjwa sugu na hatari. Licha ya matokeo ya tafiti hizo binadamu bado wanatumia vyakula hivyo ili kukidhi tama za miili yao. Baadhi ya tafiti kuhusu nyama ya nguruwe ni kwamba imejaa minyoo ambayo hata ukiipika kwa joto gani haifi.

Katika ulimwengu tunaoishi sasa pia, vyakula vya nyama vimekuwa chanzo cha magonjwa mengi yanayosababisha vifo vingi vya watu wazima na watoto. Na tatizo hili halipo tu katika siku zetu lakini katika siku za wazee wetu pia, maana kabla Mungu hajaruhusu watu kula nyama wanadamu waliishi miaka mingi sana hadi 900 na walikuwa na maumbile makubwa lakini leo kwa kula nyama watu tunaishi miaka michache sana kama miaka 60-80 tu! na tuna maumbile madogo.

Utamu unaopatikana katika vyakula vya nyama hutokama na damu au mafuta ya wanyama hao iliyopo katika minofu yake. Endapo nyama itapikwa kwa kuondoa damu na mafuta yote isingekuwa na radha yotote ya kuvutia walaji. Lakini Mungu ametoa mwongozo kwamba matumizi ya nyama sharti yasiwe pamoja na damu au mafuta.R097

Hivyo ni vema kurudi katika mpango wa kwanza wa chakula chetu, maana japo Mungu aliruhusu matumizi ya vyakula vya nyama baada ya gharika lakini hakuvipa vyakula vya nyama nafasi ya kwanza ya mlo wetu. Hili tunaliona wakati wa safari ya wana wa Israeli kwenda nchi ya ahadi, Mungu hakuwapa vyakula vya nyama kama nafasi ya kwanza ya mlo wao bali mana tu.

Pia kwa kuwa tunatakiwa kubadilisha tabia na mfumo wetu wa maisha kuelekea chakula ambacho Mungu ametupatia, mabadiliko hayo hayatakiwi kuchukuliwa kwa pupa. Lazima tujifunze kwanza namna ya kuandaa vizuri chakula cha nafaka, matunda na mbogamboga ili kiwe na matokeo mema mwilini mwetu.

Endelea kufatilia mada mbalimbali maana tutajifunza maandalizi ya vyakula vya kiafya. Pia tutajua kwa hakika maandalizi ya vyakula vizuri na vitamu kama mbadala wa vyakula vya nyama. Usikose!!!

Kwa maswali, maoni au ushauri juu ya mada hii au nyingine nyingi usisite kuwasiliana nasi.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s