JE, SABATO ILIANZIA KWA WAYAHUDI? JE, NI YA WAYAHUDI TU?

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya

Simu Namba: +255715678122

Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version: JE, SABATO ILIANZIA KWA WAYAHUDI? JE, NI YA WAYAHUDI TU?

Watu wengi wanajiuliza kwamba Sabato ilianzia kwa Wayahudi? Na kama ni hivyo basi sisi hatupaswi kutunza na kuishika maana niya Wayahudi. Katika hili tutaiuliza Biblia yenyewe iseme majibu, au siyo?

Biblia inatwambia Sabato ilianzishwa katika Bustani ya Edeni siku ya SABA baada ya uumbaji. Mwanzo.2:1-3, “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. NA SIKU YA SABA Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; AKASTAREHE SIKU YA SABA, AKAACHA KUFANYA KAZI YAKE YOTE ALIYOIFANYA, Mungu akaibariki siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, AKAACHA KUFANYA KAZI yake yote aliyoiumba na kuifanya.” Hapa tunaona kuwa Sabato ya kwanza kabisa katika historia ilikuwa Tarehe 07-01-01 au mwaka 4000K.K. Katika Sabato hii, kulikuwa na WATU WAWILI TU Adamu na Hawa ambao hawakuwa wayahudi sawa? Unajua kama Adamu na Hawa wangekua wayahudi basi watu wote tungekuwa wayahudi maana hawa walikuwa wazazi wetu wa kwanza ambamo watu wote tumetokea kwao.

Ibrahimu aliishi miaka karibia 2000 kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Uyahudi, kabla ya kipindi cha Musa cha kutoka Misri kwenda Kanani. Lakini biblia inamshuudia kuwa aliishika Sabato maana alishika amri na sheria za Mungu hata kabla hazijatolewa katika mlima Sinai kwa wana wa Israeli. Mwanzo. 26:5, inasema “Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na AMRI zangu, na hukumu zangu, na SHERIA zangu.” Hivyo Ibrahimu alishika amri za Mungu zote ikiwemo na sabato tazama Kutoka. 21:8-11, na zingatia pia Ibrahimu alishika amri zote za Mungu maana kama angevunja moja agekua hajazishika. Tazama Yakobo2:10 na Mathayo5:17-19. Pia wana wa Israeli walishika Sabato hata kabla hawajapewa amri za Mungu katika mlima Sinai hili Creation 1tunaliona katika Kutoka.16:23-27. Ndio maana wakati Mungu anatoa Amri zake kwa Israeli anasema “IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE siku sita ufanye kazi utende mambo yako yote….” Kutoka.20:8 aliwambia waikumbuke maana walikuwa wanaijua. Katika utumwa wa Misri wana wa Israeli walikuwa wamesahau sabato ya BWANA na kama wangekua hawaijui asimgewambia waikumbuke.

Yesu alipokuja alisema Sabato ilifanyika kwajili ya watu wote, Yesu “akawaambia, sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.” Marko.2:27 Hivyo tunaona kuwa Sabato ilifanyika kwa ajili ya MWANADAMU, ndugu je wewe nawe ni mwanadamu? Kama ndiyo basi mshukuru sana Mungu maana ameumba Sabato siku ya SABA ya juma kwa ajili yako uifurahie kwa pumziko takatifu.

Baada ya Yesu kwenda mbinguni, mitume waliendelea kushika Sabato pamoja na mataifa mengine wasiokuwa Wayahudi. Katika Matendo ya Mitume.13:42,44 tunaona mkutano uliofanyika siku ya Sabato ambao mataifa walimsihi Paulo arudie hubiri lake la sabato katika Sabato inayofata: ZINGATIA ‘Kama wangekuwa wanasali Jumapili, wale watu wangesema wakutane kesho yake lakini haikuwa ivyo maana walisema wakutane Sabato ijayo. Na Sabato iliyofata walikuja mji mzimakusikiliza hubiri la Paulo’ hadi wayahudi waliokuwa wapinzani wa kazi ya Mungu wakaanza kumwonea wivu. Tazama pia Matendo.18:4, Paulo “akatoa hoja zake katika sinagogi(kanisa) KILA SABATO akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.”

Biblia haisemi sehemu yoyote kuwa sabato ni ya wayahudi tu, hii kusema watu wengine wasio wayahudi hawatakiwi kushika Sabato ya  siku ya saba Jumamosi. Madai haya hayana ukweli maana kuvunja Sabato kunamfanya mtu awe mvunja sheria zote za Mungu kwani ukuvunja moja umevunja zote.

Karibu sana katika raha ya Sabato maana ni raha pekee kwa watu wa Mungu, Waebrania.4:9 inasema “basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.”

Karibu tena, kwa maswali, maoni na ushauri usisite kuwasiliana nasi.

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s