Je, Siku Ya Ibada Ya Mbinguni Ni Ipi?

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya
Simu Namba: +255715678122
Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: Je, Siku Ya Ibada Mbinguni Ni Ipi

Tumeona kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia siku mbalimbali katika juma kwajili ya ibada na kupumzika katika kazi za kila siku. Ibada hizo hufanyika katika siku za Ijumaa, Jumamosi, Jumapili, Jumatano na nyingine nyingi. Lakini swali ni hili, je tutakapokwenda mbinguni ni siku gani tutakayoabudu kati ya hizi? Je, Biblia inasemaje kuhusu hili?

Isaya. 66:22,23 “Kama vile MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na SABATO hata SABATO, WANADAMU WOTE WATAKUJA KUABUDU MBELE ZANGU ASEMA BWANA.” Mungu anasema katika Neno lake kuwa katika mbingu ambayo ameifanya kwajili ya watakatifu wake WOTE, kwamba watakuwa WANAMWABUDU katika kila siku ya SABATO yaani siku ya Jumamosi.

Ni ukweli kuwa Mungu atakuja kuchukua watakatifu wake “hao wazishikao AMRI za Mungu na imani ya Yesu”. Ufunuo.14:12 Kamwe hakuna mwenye dhambi hata mmoja atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. Si ndiyo? Sasa biblia inatoa maana rasmi ya neno dhambi katika 1 Yohana 3:4, “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwakuwa DHAMBI NI UASI.” Hivyo dhambi ni uasi wa sheria za Mungu, yaani waasi wote wa sheria hawataingia mbinguni.

Christ and RedeemedPia amri kumi za Mungu zapaswa kushikwa kwa ukamilifu wake zote kama zinavyoelezwa katika Kutoka. 20:3-17. Na kuvunja amri moja tu, ni sawasawa umevunja amri zote kumi. Yakobo2:10,11 inasema “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekua mvunja sheria.” Yaani ukishika amri za Mungu tisa tu, ukaacha kuishika sabato ya Jumamosi UMEKUA MVUNJA SHERIA. Na kwa wale ambao wanashika sabato tu na kuvunja zingine amekuwa mvunja sheria pia bali usalama upo katika kushika amri zote za Mungu ikiwemo sabato.

Quran nayo inasema katika suratun Nahl(16) kifungu cha 124 kuwa, “Hakika (adhabu ya kuvunja taadhima ya) Jumamosi iliwekwa juu ya wale waliohitilafiana kwa ajili ya hiyo (Jumaamosi), na kwa yakini Mola wako atahukumu baina yao siku ya kiama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana.” Hivyo hata Quran inatoa onyo kwa wavunja sheria ya Mungu hasa wavunja Sabato ya BWANA yaani siku ya Jumamosi.

Je, wavunja Sabato ya BWANA wote watapotea hata wanaovunja Sabato wakati wanatenda miujiza? Yesu alisema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwajina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo NITAWAAMBIA DHAHIRI, SIKUWAJUA NINYI KAMWE; ONDOKENI KWANGU NINYI MTENDAO MAOVU.” Mungu anasema kwamba kuna watu watamwendea wakimsihi waingie katika ufalme wake lakini atawakataa kwa maana hata wakati wanatenda miujiza hiyo hakuwajua maana hawakutii mapenzi ya Mungu.

Lakini tumaini lipo, Yesu alisema “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akisikia sautiyangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, name nitakula pamoja naye, nay0603135 eye pamoja name.” Ufunuo.3:20 Pia alisema kwakua “Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na SAUTI YANGU WATAISIKIA; KISHA KUTAKUWAKO KUNDI MOJA NA MCHUNGAJI MMOJA.” Yohana 10:16. Hivyo ndugu usalama utakuwa nao kama tu utaukubali wito wa Yesu leo.

Sasa kama tukienda mbinguni tutaabudu siku ya Jumamosi(SABATO). Je, kwanini tusianze kuzoea kuabudu siku hii tukiwa hapa duniani? Karibu basi katika ibada ya siku ya sabato. Tafadhali tafuta kanisa la waadventista wasabato lililokaribu nawe uanze kuwa na uzoefu huu wa ibada ya mbinguni.
Kwa maswali. Maoni au ushauri usisite kuwasiliana nasi. Bwana akubariki sana.

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s