Je, Siku Ya Bwana Haijulikani?

Evangelist John Mafuru Msibha

Evangelist John Mafuru Msibha

Na Muinjilisti: John Mafuru Musibha
Simu Namba: + 255764736335
Barua Pepe: johnmafuru22@gmail.com

Downloadable  Version: Je, Siku Ya Bwana Haijulikani

Hili ni swali ambalo sio geni masikioni mwetu. Kila mtu katika dunia hii anajibu lake, wengine husema ni Jumatatu, Jumapili na wengine husema Ijumaa na wengine wanadiliki kusema ya kwamba Mungu alificha jambo hilo kwa hiyo hamna ambaye anafahamu siku ya Bwana. Jambo la hatari zaidi wengine wanasema Yesu alitengua torati, hivyo siku yoyote ile inaweza kuwa yake.

“Je, wewe unadhani siku ya bwana ni ipi?”
Jibu lako laweza kuwa kweli au la!. Hebu kwa pamoja tufatilie Maandiko matakatifu ambayo Mungu alitupatia ili yawe dira katika maisha yetu. MWANZO 2:1-3 inasema hivi “1 Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. 2 Na siku ya saba Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; akastarehe siku ya saba, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoifanya. 3 Mungu akaibarikia siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, akaacha kufanya kazi yake yote aliyoiumba na kuifanya”. Kutoka katika kitabu cha Mwanzo tumeona kwamba Mungu aliumba vyote pamoja na binadamu kwa siku sita na siku ya saba alipumzika na kuitakasa na akasema hivi kutoka katika kitabu cha KUTOKA 20:8-10 “8 Ikumbuke siku ya Sabato uitakase. 9 Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote; 10 lakini siku ya saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. 11 Maana, kwa siku sita Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba; kwa hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato akaitakasa”. Je, hiyo ni siku gani?

Kutoka kwenye vitabu hivyo viwili tumekutana na neno “Sabato” na tumepata picha ya kuwa siku ya Bwana ni Sabato. Swali linakuja je, Sabato ni lini. Jamii fulani ya wakristo inaamini ya kwamba Yesu Kristo alivunja torati lakini Yesu Kristo mwenyewe asema hivi katika kitabu cha MATHAYO 5:17 “Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.”

Kwa wale wote wanaoamini ya kuwa torati limevunjwa Yesu mwenyewe aliwajibu ila ni kichwa ngumu chao tu na si vinginevyo. Na Yesu aliitilia mkazo kauli yake kwa kusema katika MATHAYO 5:18 “Kwa maana, amin, nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaoondoka, hata yote yatimie”.jesus and the sabbath

Je, siku ya Sabato ni ipi? Au siku ya Bwana ni ipi? Imani zote za kikristo huamini kwamba Yesu aliteswa na kusurubiwa siku ya Ijumaa, hii ndiyo siku ya Ijumaa kuu inayoazimishwa katika Ijumaa ya pasaka. Siku ya Ijumaa ambayo ni siku ya maandalio ya Sabato ya Bwana kama ilivyoandikwa katika kitabu cha LUKA 23:54 nayo yasema hivi “Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia.” Yusufu wa Arimathaya ndiye aliyemuomba Pilato ili akauhifadhi mwili kaburini (alikuwa mwanafunzi wa Yesu kwa siri; Tazama Yohana 19:38)

Kutokana na mafungu hayo tunaona kwamba siku ya Bwana ni Jumamosi na sio Jumapili wala Jumatatu wala Ijumaa na sio siku nyingine yoyote ile ambayo watu wanaamua tu kuipatia sifa. Mwanzilishi wa Sabato au siku ya Bwana ni Yesu Kristo (Utatu Mtakatifu) MWANZO1:26 “Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.” MARKO 2:28-29 nayo yasema hivi 27 Akawaambia, Sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya Sabato. 28 Basi Mwana wa Adamu ndiye Bwana wa Sabato pia.

Je, na vitabu vingine vyasemaje kuhusiana na siku ya Bwana yaani Sabato Qur-an 4:47 bismillah rahmani rahim “enyi mliopewa kitabu, aminini tuliowatelemshia yanayosadikisha yale yaliondani kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni au kabla ya kuwalaani kama tulivyowalaani watu walioharibu utukufu wa jumamosi, na amri ya mwenyezi mungu lazima kufanywa”. Qurani inathibitisha kuwa Jumamosi ndio siku ya Bwana na wote ambao hawaifuati wanalaaniwa sijasema mimi qur-ani ndo imesema. Quran 4:154 fafanuzi kipengele c “Na baada ya kutoka katika hiyo miji na vijiji vya shamu waliambiwa waidhamishe siku ya jumamosi kwa kuifanya siku ya ibada tu na sio siku ya kazi wakatiatia hila zao mpaka ikawa siku ya kazi”. Huu ni uthibitisho wa hali ya juu unao thibitisha kuwa siku ya Bwana niCoran Jumamosi. Qur-an 2:65 bismillah rahmani rahim “na kwa yakini mmekwisha kujua habari za wale walio hasi miongoni mwenu katika amri ya kuiheshimu jumamosi, basi tukawaambia kuweni manyani madhalilifu yaani manyani yasiyokuwa na akili.

Ndugu msomaji wa makala hii naamini kwa neema ya Bwana wetu Yesu Kristo utakuwa umepata kitu muhimu sana katika maisha yako. Usifikirie vibaya na kuona nakandamiza kile ambacho unakiamini ila nataka kukueleza ukweli ili usipotee kwa kufuata maagizo ya wanaadamu wenzetu ambao walikaa na kuamua siku fulani ndiyo iwe siku ya Mungu bila kuzingatia Maandiko yake matakatifu. Msikilize Roho Mtakatifu ambaye ananena nawe kuhusu Mungu anachotaka pia piga magoti umuombe Mungu kwa roho ya kweli na unyenyekevu yeye atakufunulia ukweli wote. Kutokana na Maandiko matakatifu na kitabu rejea sasa tumeelewa ya kwamba siku ya Bwana ni Jumamosi na sio siku nyingine.

ANGALIZO KWA WATU WA MUNGU
Kitabu cha mkusanyiko/muungano wa makanisa ya kipentekoste (Methodist) ukurasa 197 aya ya pili ikizungumzia kuhusu utitiri madhehebu yanayoabudu Jumapili nami nanukuu kama ifuatavyo “madhehebu si ya Mungu hayajawahi kuwa na hayatakuja kuwa kamwe, ni roho mbaya anayewatenganisha watu wa Mungu katika madaraja ya makasisi na washiriki, na kwa hiyo basi, ni roho mbaya anaebagua watu na watu hivyo ndivyo shirika na madhehebu yafanyavyo katika kuijundia madhehebu wao hujitenga na neno la Mungu na kujiingiza katika uzinzi wa kiroho”

Hebu anza katika Jumamosi ya juma hili kuiadhimisha siku ya Bwana inayoshuhudiwa na maandiko yote na vitabu. Tafuta kanisa la waadventista wa Sabato lililo jirani nawe na uwe miongoni mwa mamilioni wa wasafiri wa kweli wanaomngojea Yesu.

Kwa maswali, maoni au ushauri usisite kuwasiliana nasi. Au tembelea kanisa lolote la waadventista wa Sabato lililopo karibu nawe ili upate ufafanuzi zaidi.

Advertisements

One comment on “Je, Siku Ya Bwana Haijulikani?

  1. Asante kwa somo nzuri na linabariki pia.Nina swali ambalo liko tofauti kidogo na mada ila si sana,watu wengi husema wasabato ni sawa na waisalamu ila tumetofautiana siku tu,usawa huu uko kwenye vyakula,kujipamba na mavazi pia husema waislamu walikuwa wasabato ila walijitenga miaka ya nyuma baada ya Ismail kuzaliwa mwana wa Ibrahimu na kijakazi wake. Naomba ufafanuzi kama haya ni ya kweli..Asante

    Like

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s