Chakula Tunachopaswa Kula Ili Tuwe na Afya Bora

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya
Simu Namba: +255715678122
Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: Chakula Tunasopaswa Kula Ili Tuwe Na Afya Njema

Mungu ni mwema sana kwakuwa kabla ya kumuumba mwanadamu alimuandalia chakula bora na safi ambacho angekitumia kuunufaisha mwili wake kwa virutubisho vyote muhimu. Watu wengi hawajui chakula ambacho Mungu alimpatia mwanadamu aliyemuumba na hivyo tunabuni wenyewe vyakula mbalimbali ambavyo si chaguo la Muumbaji wetu. Watu wengine wanajua chakula ambacho Mungu alitupatia tukitumie lakini kwa kujiona wana hekima sana au kwa shauku na tama wanaepa na kujibunia vyakula vyao. Vyakula vingi vinavyotumika leo havipo katika mpango wa muumbaji wetu wa chakula chenye manufaa katika mwili wa mwanadamu. Mingu ametuumbia mazingira manyofu na mema kwa chakula chema cha kiafya lakini tumebuni vyakula vyetu. Mhubiri 7:29

“Tazama, hili tu nimeliona; Mungu amemfanya mwanadamu mnyofu, lakini wamebuni mavumbuzi mengi.”

Vyakula tulivyojichagulia kwa kutojua au kujua lakini kwa kufuata tama za miili yetu vimejaa vimelea mbalimbali vya magonjwa, vimekosa virutubisho vya kiafya na kutokidhi mahitaji ya mwili na hivyo kudhoofisha mwili. Siku ya tatu ya uumbaji, Mungu aliumba chakula cha mwanadamu.Mwanzo 1:11-12

“Mungu akasema, Nchi na itoe majani, mche utoao mbegu, na mti wa matunda uzaao matunda kwa jinsi yake, ambao mbegu zake zimo ndani yake, juu ya nchi; ikawa hivyo. Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.”

Mungu aliandaa chakula cha mwanadamu kabla hajamuumba, alijua ya kwamba chakula hiki kinafaa sana kwa ustawi wa mwili wake. Matunda na Nafaka zilikuwa ndiyo chakula chetu kutoka mikononi mwa Muumbaji wetu. Mwanzo 1:29-30

“Mungu akasema, Tazama, nimewapa kila mche utoao mbegu, ulio juu ya uso wa nchi yote pia, na kila mti, ambao matunda yake yana mbegu; vitakuwa ndivyo chakula chenu; na chakula cha kila mnyama wa nchi, na cha kila ndege wa angani, na cha kila kitu kitambaacho juu ya nchi, chenye uhai; majani yote ya miche, ndiyo chakula chenu; ikawa hivyo.”SAM_0411

Lakini baada ya dhambi au anguko la mwanadamu, Mungu aliongeza mboga za majani katika mlo wa mwanadamu. Mwanzo 3:18

“michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni;”

Hivyo vyakula vya kwanza kwa mwanadamu ni Nafaka, Mbogamboga na Matunda tu. Chakula cha kwanza tulichopewa na Muumbaji wetu hakikuhusisha nyama au vyakula vitokanyo kwa wanyama kama nyama, maziwa, mayai, samaki n.k Kuna kisa katika Biblia kuhusu vijana wa nne walioazimu moyoni mwao kwamba hawatakula chakula chochote ambacho ni tofauti na kile ambacho

Mungu alikitoa kama mlo wa mwanadamu aliyemuumba. Ilikuwa kusudi kwamba wapewe chakula na vinywaji vyote anavyokula mfalme wa Babeli taifa la kipagani, vyakula na vinywaji ambavyo vilikuwa mbali sana na mpango wa Mungu wa chakula cha mwanadamu. Lengo lilikuwa wawe na afya njema, akili, hekima, busara na ufahamu wa hali ya juu ili watumike katika ikulu ya Babeli na majimbo yote ulimwengu mzima. Vijana hao walikataa chakula cha mfalme lakini cha kushangaza baada ya miaka mitatu ya masomo yao kwisha walipewa mtihani mbele ya mfalme wa Babeli na vijana wale wanne waliokataa posho ya chakula cha mfalme walionekana kuwa bora zaidi mara kumi zaidi ya wale waliojishibisha kila siku kwa chakula na vinywaji vya mfalme wa Babeli.

Matokeo ya mafanikio yao kimwili, kiakili na kiroho yalitokana na kujishibisha kwa chakula ambacho Mungu alikitoa kwa mwanadanu yani nafaka, kokwa, mbogamboga, matunda na maji tu.

Ni kosa kubwa kudhania kwamba kwa kutumia chakula ambacho Mungu alikitoa kwa mwanadamu tutadhoofika na kupungukiwa. Ni kosa kudhani kwamba kujitosheleza haja zetu za chakula kwa nafaka, kokwa, matunda na mbogamboga tu kunatuletea upungufu katika afya zetu. Wakati tutakapoamua kutawala meza zetu kwa chakula ambacho Muumbaji wetu alitupatia ndipo tutaonekana wema mara kumi zaidi ya wale wasiofanya hivyo. Isaya 55:2

“Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.” Daniels and  Friends

Licha ya faida kubwa zinazoweza kupatikana katika vyakula ambavyo Mungu alitupatia lakini uangalifu mkubwa na tahadhali yapasa kuchukuliwa katika uchaguzi, maandalizi na utumiaji wake. Usikose mfululizo wa masomo haya kwani tutajifunza kuhusu namna ya kuchagua, kuandaa na kutumia vyakula ambavyo Mungu alitupatia. Wakati wa gharika dunia yote iliharibiwa kwa maji na hakukuwa na aina yoyote ya nafaka, matunda wala mbogamboga ndipo Mungu aliruhusu matumizi ya vyakula vya nyama. Mwanzo 9:3, 7:23.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s