Rafiki Aletaye Utotauti Katika Maisha, SEHEMU YA KWANZA

Karibu katika somo la leo,

UHITAJI WA RAFIKI ALETAYE UTOFAUTI!

Evangelist Daniel Buyaga Kitigani

Evangelist Daniel Buyaga Kitigani

Na. Muinjilisti Daniel Buyaga Kitigani

Mobile: +255768799730 na +255684280775

Email: buyagad@gmail.cpm

Kutoka katika kitabu cha zamani sana Biblia, tunakuta maelezo haya:

Yohana 15:13-15

“Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.”

Yesu huyu anayetuita sisi kama marafiki zake ni nani? Huyu ana sifa zipi za upekee zinazomtofautisha na marafiki wa dunia hii? Je, anastahili kuaminiwa na kufanywa kuwa rafiki wa kweli katika maisha yetu?

Katika kitabu hiki cha zamani, njoo pamoja nami, twende pamoja kutafuta majibu kwa maswali haya. Tukajifunze mambo kadhaa kwa mtu huyu anayetuita sisi kuwa marafiki zake!

Ushuhuda wa Maandiko:
Maandiko yalimzungumza mtu huyu kabla hajazaliwa

Jinsi atakavyozaliwa:
Unabii: Isaya 7:14 Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli.
Kutimizwa: Mathayo 1:22-23 Hayo yote yamekuwa, ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akisema, Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasiChrist - Birth - His Name Shall Be Called - Simon Dewey

Mahali alipozaliwa:
Unabii: Mika 5:2 Bali wewe, Bethlehemu Efrata, uliye mdogo kuwa miongoni mwa elfu za Yuda; kutoka kwako wewe atanitokea mmoja atakayekuwa mtawala katika Israeli; ambaye matokeo yake yamekuwa tangu zamani za kale, tangu milele

Kutimizwa: Mathayo 2:1 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema

Utume Wake. Maandiko yalitangulia kusema kuhusu kusudi la kuja kwake

Unabii: Isaya 61:1-2 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu Bwana amenitia mafuta niwahubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwaganga waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao. Kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa, na siku ya kisasi cha Mungu wetu; kuwafariji wote waliao;

Kutimizwa: Luka 4:16-19 Akaenda Nazareti, hapo alipolelewa; na siku ya sabato akaingia katika sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake, akasimama ili asome. Akapewa chuo cha nabii Isaya, akakifungua chuo, akatafuta mahali palipoandikwa, Roho wa Bwana yu juu yangu, Kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa kwao, Na vipofu kupata kuona tena, Kuwaacha huru waliosetwa, Na kutangaza mwaka wa Bwana uliokubaliwa. Kile awezacho kufanya: Kuganga mioyo ya wanadamu, kuwafariji waliovunjwa mioyo, kuwaweka huru wafungwa kutoka gereza la dhambi na kutangaza habari njema kwa maskini.

Kifo Chake:
Kimeandikwa katika Sura ya 53 ya Kitabu cha Isaya, (Agano la kale) na ndivyo ilivyotimia katika vitabu vya Injili (Agano jipya).

Usalitiwa
Unabiii: Zekaria 11:13 Kisha Bwana akaniambia, Mtupie mfinyanzi kima kizuri, hicho nilichotiwa kima na watu hao. Basi nikavitwaa vile vipande thelathini vya fedha, nikamtupia huyo mfinyanzi ndani ya nyumba ya Bwana.

Kutimizwa: Mathayo 27:3,5 Kisha Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, alijuta, akawarudishia wakuu wa makuhani na wazee vile vipande thelathini vya fedha, akasema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia… Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga.
Kutokana na ushahidi wa Maandiko haya ya Biblia, Mtu huyu ndiye Masihi aliyezungumzwa katika agano la kale na maisha yake yanaonekana katika agano jipya. Huyu ndiye anayezungumzwa kama kiini cha maandiko. Na wito wa Mungu kwa wanadamu kwa Nyakati zote, ni kwa ajili ya kuwaokoa kutokana na uharibifu wa dhambi kupitia Neema ya Kristo iliyo kwa njia ya Imani kwa Kifo cha Kristo.

Upekee Alionao Mtu Huyu:
Mtu huyu anatuita sisi marafiki zake, ametofautiana na marafiki zetu wengine tuliowazoea kwa sifa kadha kama tutakavyoangalia. Hapo kuna baadhi ya sifa za Mtu huyu aliyetuchaguwa kuwa marafiki zake:
1. Uwezo wa Kusamehe na Kuondoa Dhambi
Jesus ForgivingMaandiko hutushudia juu ya uwezo alionao Yesu wa Kusamehe Dhambi.
Na tazama, wakamletea mtu mwenye kupooza, amelala kitandani; naye Yesu, alipoiona imani yao, alimwambia yule mwenye kupooza, Jipe moyo mkuu, mwanangu, umesamehewa dhambi zako. (6) Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi. (Mathayo 9:2,6). Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake (1 Yohana 3:5).

2. Maandiko Yanamtambulisha kuwa ni Mwana wa Mungu Aliyehai
Nao waliokuwamo ndani ya chombo wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu. (16:16) “Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai”. Huyu si mwanadamu wa kawaida (Math 14:33, 16:16).

3. Amejaa Huruma kwa Wanadamu wote
Na alipowaona makutano, aliwahurumia, kwa sababu walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchungaji (Math 9:36). Katika ulimwengu huu, kila watu wanapokutazama, wanakuonaje? Yesu hukutazama kwa jicho la huruma. Hukutazama kama aliyechoshwa na dhambi na nanayehitaji msaada na asiye na uwezo wa kujisaidia.

4. Mchungaji wako anayejali Usalama wako kiasi cha kuutoa Uhai wake
Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Upendwe upendweje, hutapata mwandamu aliye tayari kuutoa uhai wake kwa ajili yako. YESU alitoa Uhai wake ili atupatie usalama hata katika ulimwengu huu uliojaa shida za kila aina, na hivyo tukimwendea, kwake huyo htumehakikishiwa usalama wa Kiuchumi, Kiafya, Kiroho na mwaminifu katika kulinda mahusiano Mahusiano. Unajua mimi sioni sababu ya wewe kutojitoa kwa Kristo Yesu!!!

5. Upendo wake Usio na Sababu kwetuChrist and Lamb - Copy
Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali kwamba yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. (19) Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza (1 Yohana 4:10,19). Unajua ukipendwa bwana, sharti na wewe upende.

Je, msomaji wangu, ungependa uwe na rafiki wa aina gani? Unajuwa, ubora wa rafiki uliye naye, hutegemea sifa alizo nazo. Na kulingana na uchunguzi, hizi ni sifa za mtu anayestahili awe rafiki yako. Na labda niwe tu muwazi kwa hili, mimi nimekwisha kumkubali awe rafiki yangu. Nikushauri, mkubaliki awe rafiki yako, maana haishii kuwa na sifa nzuri tu, bali anato mwaliko wa kukuomba umkubali ufanye urafiki naye na ataleta utofauti katika maisha yako.

Mwaliko wake wa Urafiki.
Anatualika mtu yeyote kumwendea. Mwaliko wake unaenda kwa watoto wadogo, vijana na watu wakubwa. “Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao” (Luka 18:16).

Anatualika watu wote ambao tunateseka na tumefungwa katika dhambi tumwendee.

“Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu. (19) Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; (20) bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya” (Isaya 1:18-20).
Anatualika wanadamu wote tuliochoshwa na mizigo ya maisha haya tuwamwendee ili atupe pumziko la moyoni na furaha nafsini mwetu.
“Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. (29) Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu” (Mathayo 11:28-29)

The InvitationAnatualika watu wote tumwendee akitupatia uhakika wa kutupokea jinsi tulivyo.

“Wote anipao Baba watakuja kwangu; wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe” “…na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.” (Yohana 6:37, Mathayo 28:20).

Zingatia hili, wazo la kuwa Rafiki na Yesu, halitoki kwako. Limetoka kwake na anapolileta kwako leo, unaliamuaje? Utaungana na watu wengi leo wanaompokea na kuukubalia mwito wa Yesu kwa kujitoa kwake ili uwezo wake ufanye jambo flani tofauti katika maisha yako, au utampuuza kama wengine pia wafanyavyo? Lamda ungehitaji ujiridhishe kwamba, kwanini huna budi kuyatoa maisha yako kwake?

Kwa nini Huna Budi Kumpa Yesu Maisha yako yote Leo?

Tunapaswa kuwa na ujasiri kwa Rafiki huyu kwa Sababu zifuatazo:

1. Ukaribu wake.
Hakuna rafiki anayeweza kuelewa mawazo ya moyo wako, isipokuwa Yesu kwa sababu Yeye hukaa ndani yao wote waliomkubali wakampokea na kumpa maisha yao yote. Yohana 14:18 Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Ufunuo 3:20 Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Mathayo 28:20 “…na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.”

2. Ana Uwezo wa Kujaza Amani Moyoni Mwako.
Wakati mwingine si lazima dhoruba za maisha ziondolewe, bali hata katikati ya dhoruba, Yesu anaahidi kuwapa Rafiki zake amani na utulivu mioyoni mwao. Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. (Yohana 16:33) Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

3. Yesu Ana uwezo wa kuujza Furaha Ndani ya Moyo wako Unapomwendea.
Wito wa Yesu ni kwa ajili ya kuwapa furaha ndani ya Nafsi zao. Mathayo 11:28-29 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. (29) Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu; (Yohana 16:24) Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu

4. Mwaliko wa Yesu ni ili atuokoe;
Yohana 3:16-17 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. (17) Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.

5. Ahadi ya Uzima wa Milele kwa wote Waliomwamini.
Yohana 7:38 Aniaminiye mimi, kama vile maandiko yalivyonena, mito ya maji yaliyo hai itatoka ndani yake. Yohana 11:25 Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi:Christ and Family - Copy

6. Yesu huwapatia wote wanaompokea na kumwamini uwezo wa kufanyika wana wa Mungu.
Yohana 1:12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; 1Yohana 3:1-2 Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. (2) Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Hii ni wazo la Mungu kwa mwanadamu, na hii ni hadhi ya Juu sana kuliko ulimwengu uwezavyo kutoa.

7. Ahadi ya Kutawala pamoja Naye katika Ufalme wake wa Ulimwengu Ujao.
Mpango wa Mungu ni kumrejeshea mwanadamu hadhi aliyoipoteza baada ya dhambi. Mwanzo 1:26 Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Ufunuo 3:21 Yeye ashindaye, nitampa kuketi pamoja nami katika kiti changu cha enzi, kama mimi nilivyoshinda nikaketi pamoja na Baba yangu katika kiti chake cha enzi.

“Karibu sana katika somo linalofuata. Ubarikiwe sana.”

Kwa maswali au maoni wasiliana nasi kupitia:-

Simu: +255768799730, +255715678122 na +255756534710

email: buyagad@gmail.com

Advertisements

One comment on “Rafiki Aletaye Utotauti Katika Maisha, SEHEMU YA KWANZA

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s