Kumpa Yesu Nafasi

“Kupitia hili nilijifinza kuwa Mungu ni wa ajabu na anasikia ombi lolote, kwa wakati wowote na mahali popote”

RAFIKELSimulizi na: Rafikiel Alfred

Mobile: +255653113103

Email: arafikiel@gmail.com

Ilipofika jioni muda wa kurudi nyumbani kutoka shuleni ulifika, na kama kawaida huwa tunakuta mama ametuandalia chakula kwa ajili ya kupooza njaa. Tulifurahia chakula tulichoandaliwa na baada ya hapo nilianza kufanya shughuli za nyumbani huku mdogo wangu akiwa katika michezo yake ya kila siku. Wakati huo nilikuwa na umri wa miaka 12 na mdogo wangu alikuwa na miaka 9. Baada ya muda mfupi mama alirejea nyumabani huku uso wake ukiwa si wa furaha na alionekana kuna tatizo na hata hivyo aliwahi kurudi nyumbani. Mama hakutaka kutuogopesha hivyo baada ya salamu tu aliingia chumbani na kupumzika. Haikuchukua muda mrefu aliniita na kuniambia tumbo lilikuwa linamsumbua hivyo alitaka niende nikamtafutie maziwa. Niliona ni jambo geni maana mama alikuwa akilia kuonyesha alikuwa na maumivu makali nilinyanyuka haraka na kukimbia kwenda kutafuta maziwa, mara nilirejea na kuyachemsha yale maziwa. Nilipoingia chumbani kwa ajili ya kumpatia mama maziwa nilimkuta mdogo wangu akiwa amelala pembeni ya mama naye akilia nilimshi na kumwambia sio vizuri japo nami nilitamani kulia kutokana na hali ya mama. Mama aliyanywa yale maziwa lakini baada ya muda aliyatapika yote jambo ambalo lilizidi kututia hofu.

Mama aliniita na kuniambia nimpigie baba simu na kumwambia kuwa anajisikia vibaya sana. Nilichukua simu lakini baba alikuwa hapatikani hewani. Ndipo mama alinyanyuka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda hospitali lakini alionekana asiye na nguvu tulimsihi amsubiri baba lakini alikataa akisema alikuwa akijisikia vibaya hivyo aliondoka mwenyewe kuelekea hospitali huku akituacha na hofu kwa jinsi hali yake ilivyokuwa.

Baada ya mama kuondoka, haukupita muda mrefu baba alirejea na baada ya salamu alituuliza mama yuko wapi, tulimwambia hali ya mama ilivyokuwa na hakuingia tena ndani akaondoka kumfuata mama. Tulikaa hadi muda wa saa nne usiku ndipo mama na baba waliporejea lakini hali ya mgonjwa bado haikuwa nzuri. Baba alituagiza kuchemsha tena maziwa kwasababu mama hakutaka chakula chochote, tulifanya hivyo aliyanywa lakini tunamshukuru Mungu hakutapika. Licha ya hayo, bado alilalamika tumbo lilikuwa likimuuma na akilia kwa uchungu jambo ambalo lilitufanya wote kulia.

Hatukuweza kulala tulikaa na wazazi wetu hadi alfajiri baba akasema inabidi warudi tena hospitali. Lakini muda wote tulikuwa tukiomba Mungu amponye mama. Baba alitusihi kuomba kila mara alipoona tunalia, na tulikuwa tukiomba maombi mafupi mafupi ya Mungu msaidie na umponye mama.

Baba aliniambia tusiende shule maana tulikuwa tumechoka kwani hatukuweza kula wala kulala hivyo tulibaki nyumbani tu. Hatukuwa na njia ya kuwasiliana nao hivyo ilitubidi kusubiri mpaka watakaporejea. Mpaka ilipofika jioni ndipo baba alirejea lakini alikuwa pekeyake tulimkimbilia na bila salamu tulimuuliza mama yuko wapi? Alitabasamu na kusema “yupo salama”. Nilimshukuru Mungu japo hatukuamini maana bado alionekana bila furaha na alituambia tujiandae na kumwandalia mama baadhi ya vitu maana alikuwa amelazwa. Tuliondoka lakini njia nzima baba hakuongea chochote na aliendesha gari taratibu sana tulipofika hospitali tulishuka na kuelekea wodini. Njia nzima nilikuwa nikisali “Yesu msaidie mama” hadi nilipoingia wodini. Mini na mdogo wangu tupomuona mama tulimkimbilia katika kitanda alicholazwa na kumkumbatia kwa furaha huku akionesha uso wa tabasamu kwa kutuona. Baba naye alifurahi kumuona mama akitabasamu maana alipoondoka alikuwa katika mapumziko hivyo hakuweza kuzungumza naye.

Tuliandaa chakula na tukala kwa pamoja japo mama hakuwa na nguvu. Hivyo alikula chakula kidogo tu, lakini tulimshukuru Mungu kwa chakula alichokula. Tulimuuliza alikuwa akisumbuliwa na nini na tulishangaa baada ya kutuambia kuwa ilikuwa ni sumu iliyokuwa katika chakula alichokula wakati akiwa kazini. Tulimtukuza Mungu maana daktari naye alisema ni jambo la kumshukuru Mungu aliwahishwa hospitali na kufanyiwa matibabu mapema. Tuliomba na kumshukuru Mungu na tuliondoka kurejea nyumbani na kumuacha mama hospitali kwa ajili ya matibabu zaidi. Mama aliruhusiwa baada ya siku chache na kurejea nyumbani japo bado alikuwa dhaifu lakini Mungu alimpigania hadi akapona kabisa.

Mara nyingi tunapopatwa na matatizo au majaribu ya kutuumiza au kututushtua sana tunasahau kumuita Yesu na kumwambia haja ya mioyo yetu. Yesu ambaye anajishughulisha sana kwa fadhaa zetu za maisha. 1 Petro 5:7 “huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu.” Na tunasahau ahadi ambazo Yesu ametupatia katika Neno lake kwa mfano: “Niite nami nitakuitikia…nitakuonesha mambo makubwa magumu usiyoyajua..” “Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.” “Nanyi ombeni kwa jina la mungu wenu…Mungu yule ajibuye kwa moto, na awe ndiye Mungu.” “ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema” “Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu” Yeramia 33:3, Mathayo 7:7-8, 1 Wafalme 18:24, Malaki 1:9 na Yohana 16:24. Maana yatupasa kudai ahadi kutoka Kwake. Kupitia hili nilijifinza kuwa Mungu ni wa ajabu na anasikia ombi lolote, kwa wakati wowote na mahali popote. Tumtangulize na tumuite Yesu katika shida na majaribu yetu naye atatuinua pasipo shaka yoyote haijalishi tuanapitia nini aliahidi kuwa nasi milele na kutujibu maombi yetu.

Kwa sasa Rafikiel anasoma Shahada ya Usimamizi wa Rasilimali watu ya Chuo Kikuu Mzumbe Morogoro Tanzania. Wazazi wake wanafurahia miaka 26 katika ndoa iliyojaa upendo, amani na baraka za Bwana. Mungu amewajalia familia yenye watoto wanne Rafiki, Rafikiel, Younze na Timothy. Mungu akubariki unapoendelea kumtumaini na kumtegemea. Wala usisahau “Kumpa Yesu Nafasi”.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Ushuhuda

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s