Kanuni Mhimu Za Afya Bora

Evangelist Mujaya Mujaya

Evangelist
Mujaya Mujaya

Na Mujaya Mujaya

Mobile: +255715678122 or +255768678122

Email: ev.mujaya@gmail.com

Mashine ni kitu chochote kunachotumika kurahisisha kazi. Kitu ambacho bila kukitumia utendaji kazi utakuwa mgumu na utatumia muda mrefu. Mwili wa mwanadamu ni mfano wa mashine tata, mashine ambayo imejengwa kwa mifumo mingi inayotegemeana katika utendaji kazi wake. Ufanisi wa mfumo mmoja huchochea ufanisi wa mifumo mingine na pia kushindwa au matatizo katika mfumo mmoja huchangia matatizo katika mifumo mingine.pic

Mifumo inayounda mwili wa mwanadamu ni mingi sana mfano: Hewa, Chakula, Utoaji taka mwili, Damu, Fahamu, Uzazi, Kinga, n.k Mifumo hii hufanya kazi kwa kushirikiana.

Ili mashine yoyote ifanye kazi zake sawasawa, isichakae au kuharibika upesi, kuna kanuni muhimu za kuzingatia ambazo hutolewa na mtengenezaji wa mashine husika kusudi mashine ifanye kazi zote zilizokusudiwa. Mungu alipomuumba mwanadamu aliweka kanuni ambazo zikifuatwa mwanadamu atafanya kazi zake bila matatizo ya kiafya na mifumo ya mwili haitaugaugua. Kanuni ambazo zitasaidia mwanadamu asichakae mapema, aishi kwa muda mrefu na furaha.

Kanuni hizo ni matumizi bora ya Chakula, Mazoezi, Maji, Mwanga wa jua, Kiasi, hewa safi, na Kumtegemea Mungu. Kanuni hizi zote hufanya kazi kwa kushirikiana, zote ni sawa na hakuna iliyo ndogo au isiyo ya masingi kuliko nyingine. Jambo la kustaajabu ni kwamba Mungu alimpatia mwanadamu mahitaji haya yote kabla hata hajamuumba. Kabla mwanadamu hajaumbwa, Mungu alikuwa ameandaa mazingira tayari kwa ustawi wa maisha ya kiafya ya mwanadamu. Kanuni hizo zitakuwa kitovu cha mada zetu mbalimbali zinazokuja.

Kwa kuzifiata kanuni hizi utakuwa salama na afya bora. Mwili wako na mifumo yake yote itafanya kazi zake kwa uzuri na hivyo kukuhakikishia afya njema, imara na maisha marefu ya furaha bila kuugua ugua.

Kanuni za afya zinahitajika kuwa mtindo wetu wa maisha ya kila siku maana mtindo wa maisha ukiwa wa kuzingatia afya bora basi tutakuwa na afya njema. Hivyo kuwa na afya bora hutegemea mtindo wa maisha ambao mtu amechagua kuishi. Pia maamuzi ya kuwa na afya bora huanzia katika maamuzi ya kubadili mtindo wa maisha na kuamua kuishi maisha ya kufuata kanuni zote za maisha ya afya bora.

Mungu ni chanzo cha afya njema wala si magonjwa, na kama Mungu si chanzo cha magonjwa basi ni ukweli kwamba Mungu si chanzo cha vifo vitokanavyo na magonjwa mbalimbali. Magonjwa yote hutokana na uvunjwaji wa kanuni hizo za maisha ya kiafya na si vinginevyo. Na mtu anapogeuka kuziacha kanuni hizi husababisha mazingira ya magonjwa mbalimbali ambayo yangeweza kuzuiwa kwa kuzingatia kanuni za afya. Hivyo ni heri ikiwa utazifahamu, kuzitambua, kuzithamini na kuzitendea kazi kanuni zote za afya njema.pic2

Watu wengine wamejikuta katika magonjwa ya hatari na kuingia gharama kubwa katika matibabu kwa sababu hawajui kanuni za kuendesha miili yao au wanajua kanuni za utunzaji mwili lakini hawazitii wala kuzifuata.

Ni bora kujikinga na ugonjwa kuliko kuutibu, kwa mfano ni bora kulala katika chandarua, kula chakula bora, mazoezi na maji ya kutosha ili usipate Maralia kuliko kutibu ugonjwa baada ya kuupata maana utakuzuia kufanya shughuli za kipato na hivyo kukupotezea pesa ambazo ungezipata ikiwa ungekuwa na afya njema, utatumia gharama kubwa za matibabu, mawasiliano, nauli, chakula cha mgonjwa n.k

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

One comment on “Kanuni Mhimu Za Afya Bora

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s