Je, Ninawezaje Kuwa na Afya Njema?

Evangelist Mujaya Mujaya

Evangelist Mujaya Mujaya

Na. Mujaya Mujaya

Mobile: +255715678122 or +255768678122

Email: ev.mujaya@gmail.com

Maana ya Afya Njema

Kulingana na shirika la afya la Umoja wa Mataifa (WHO), afya maana yake ni hali ya ukamilifu mwema kimwili, kiakili na kijamii na wala si hali kutokuwa na ugonjwa au udhaifu. Kulingana na tafsiri ya WHO, Mtu anaweza asiwe katika hali ya ugonjwa au udhaifu lakini awe hana afya njema, lakini mtu anapokuwa katika hali njema kamilifu ya kimwili yaani msawazo wa kiakili, kimwili na kijamii ndipo anakuwa na afya njema. Afya njema si unene au kuwa na kitambi au tumbo kubwa sana.

Afya si kunawili au kuwa na pesa au mali mengi kama ambavyo baadhi ya watu huamini. Mtazamo wangu kuhusu maana ya afya unatofautiana na WHO ambao tangu wameitunga mwaka 1948 hawajaibadilisha. Tafsiri ya WHO inaacha nguzo mhimu ya afya njema au maisha ya kiafya, nayo ni afya ya kiroho.

Katika ukuaji na afya njema, hali au maisha ya kiroho yana mchango mkubwa. Kuhusu ukuaji wa Yesu biblia inasema, “…alikuwa katika hekima na kimo akimpendeza Mungu na wanadamu” Luka 2:52. Hekima: kufikiri sawasawa–afya ya akili.

 • Kimo: Kukua sawasawa–afya ya mwili.
 • Akimpendeza Mungu: Uhusiano mzuri na Mungu–afya ya kiroho.
 • Na wanadamu: Uhusiano mzuri na jamii–afya kijamii.

Hivyo tafsiri inayofaa kuhusu afya ni hali ya ukamilifu mwema kiroho, kiakili, kimwili na kijamii na wala si kutokuwa na ugonjwa au udhaifu. Sehemu zote nne yani akili, mwili, kiroho na kimwili huhusiana na kutegemeana ili kukamilisha afya ya mwanadamu hivyo haiwezekani kuzitenganisha. Hatahivyo mtu anahitaji kuwa katika uwiano sawa wa kila nguzo ili awe na maisha ya afya. Mtu mwenye afya ni mchangmfu sana, anaweza kupata zaidi, anaweza kuzalisha zaidi, amaweza kuwasaidia wengine zaidi, anaweza kuufahamu upendo wa Mungu zaidi na anaweza vema kuwaeleza na kushiriki na wengine kuhusu upendo wa Mungu zaidi.

Ni Mpango wa Mungu Tuwe na Afya Njema

Ni mpango na shauku ya Mungu tufanikiwe na tuwe na afya njema. 3 Yohana 2, ni ombi lake na shaukuWS yake tufanikiwe katika mambo yote mema tunayoshighulika nayo na katika afya pia. Katika uumbaji wa mwanadamu,

Mungu alizingatia uwepo mazingira bora kwajili ya afya njema: Maji, Hewa safi, Chakula, Mazoezi, Mwanga wa jua, Kiasi, Pumziko na imani kwa Muumbaji aliweka kwajili ya ustawi wa maisha ya mwanadamu. Hivyo ni Mungu aliye chimbuko la afya njema kwakuwa:

 • Ndiye muumbaji wetu: mwanadamu alitoka mikononi mwa muumbaji wake akiwa mwema na wakupendeza sana, Mwanzo 1:31, “Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana. Ikawa jioni ikawa asubuhi, siku ya sita”. Inahitajika miaka mingi ya masomo, utafiti na kufanya kazi kwa vitendo ili mtu awe mtaalamu wa kiungo kimoja tu cha mwili wa mwanadamu lakini Mungu haikumchukua muda kuufanya mwili wa mwanadamu nan i mtaalamu wa viungo vyote. Njia ya kusaidiana na Mungu katika kutunza viungo vyetu vyote vya mwili ni kufuata kanuni zote za afya njema. Madaktari wanatusaidia wakati tukiwa tumepata magonjwa lakini Mungu anataka kutusaidia tukiwa na afya njema ili tusipate magonjwa.
 • Muumbaji wa mazingira yetu. Mungu ametuumbia mazingira mema ya ukuaji na ustawi wa afya zetu.
 • Anatupenda. Mawazo ya Mungu ni mema siku zote kwa mwanadamu wala asipate magonjwa au maafa. Yeremia 29:11 “Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema Bwana, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.”

Ugonjwa ni Nini?

Ugonjwa ni jitihada za mwili kujikomboa kutoka katika tabia au matendo yanayosababisha uvunjaji wa kanuni za afya njema. Mwanadamu anakuwa amevunja kanuni za afya na katika jitihada za mwili kujikomboa katika hali hiyo ndipo mtu anajihisi katika hali ya ugonjwa.Picture50 Kuna sababu nyingi zinazosababisha ugonjwa. Sababu kubwa ni mfumo mbaya wa maisha, kuvunja kanuni 8 za afya na kuishi namna isiyo ya kiafya hutuongoza katika shinikizo la damu, kansa, TB, ukimwi, ugonjwa wa moyo, kisukari n.k Magonjwa mengine husababishwa na virusi, bakteria na vijidudu vidogo vya magonjwa. Mfano ni Surua, Kupooza, Homa ya uti wa mgongo, Kuharisha, Homa, kichomi, TB na ukimwi. Magonjwa mengine husababishwa na minyoo na wadudu wanaoambukiza. Kwa mfano: Malaria, Kichocho, Tegu, n.k

Magonjwa mengine husababishwa na ajali, miili kuzeeka na kuchakaa. Magonjwa mengine hurithiwa kwa wazazi na mengine tunayapata wakati wa kuzaliwa. Kuna milango mitatu kwa vijidudu vya magonjwa kuingia mwilini mwetu.

 • Mdomo: wadudu huingia kupitia chakula, hewa au maji machafu yenye vijidudu
 • Pua: tunapovuta hewa chafu au mbaya
 • Ngozi na utando wa kamasi: ngozi huzuia vijidudu isipokuwa kama kuna kidonda kilichoachwa wazi au kuumwa na mdudu wakati ambapo hatuzingatii usafi wa jumla.

Kazi ya Daktari Kazi ya daktari ni kuutafuta ugonjwa na kumsaidia mgonjwa kusahihisha sababu zilizopelekea kupata ugonjwa huo. Hivyo mtu anapopata ugonjwa ni lazima mambo yafuatayo yafanyike:-

 • Uchunguzi wa kina wa sababu za kupata uginjwa huo
 • Kusahihisha tabia ba sababu zote zilizosababisha upataji wa ugonjwa huo
 • Kuusaidia mwili katika jitihada zake za kujisafisha na kuanzisha tena hali ya mwili iliyo njema.

Katika utunzaji wa mwili wetu ni wajibu wa kila mtu kuwa makini katika utunzaji wa afya yake, kujilinda kwa kila kitu tunachokula, kunywa, kuvaa n.k kwa maana Mungu wetu hadhihakiwi kwa namna yoyote na kwamba tutavuna tunachokipanda. Wagalatia 6:7 Kazi ya Dawa Watu wanahitaji kujifunza kwamba madawa ya hospitalini hayatibu magonjwa.

Ni ukweli kwamba wakati fulani yanaweza yakaleta unafuu kwa mgonjwa au mgonjwa akaonekana kama amepona kwa kuyatumia; hii nikwa sababu mwili una nguvu kubwa ya kuondoa sumu na kusahihisha hali iliyopelekea kuwepo kwa ugonjwa.Picture29 Afya hupatikana licha ya matumizi ya madawa ya viwandani. Lakini kwa kiasi kikubwa madawa ya viwandani hubadilisha aina na sehemu ya ugonjwa. Hata ivyo madhara ya sumu ya madawa haya huonekana kana kwamba yameisha kwa muda kitambo, lakini matokeo ya sumu hizo hubaki katika mfumo wa mwili na huwa na madhara makubwa siku za usoni.

Afya si Matokeo ya Bahati Nasibu

Afya njema si matokeo ya bahati au kinyume chake kifo si matokeo ya bahati mbaya au siku yako imefika. Kuna watu wengi wanawaisha vifo vyao kwa kutokana na mtindo mbaya wa maisha wanaoishi. Wengine wanasema kifo ni kazi ya Mungu haina makosa, au wengine wanasema “kweli tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi”. Kusema hivi ni kumfanya Mungu kuwa msababishi wa vifo yani ni kazi yake kuuwa watu na kutoa uhai wa watu kwa kisingizio cha kuwapenda. Lakini biblia inapingana na dhana hii kwa kusema upendo wa Mungu hutaka tuwe na uzima tena uzima wa milele, Yohana 3:16. Mungu alikuja ili tuwe na uzima tele, Yohana 10:10.

Vifo vingi vinatupata kwa sababu ambazo zinaweza kuzuilika, kwa mfano magonjwa ya ulaji wa chakula, unywaji wa maji, uvutaji au matumizi ya vileo na dawa za kulevya yanazuilika kwa kuepuka na kuacha tabia hizo. Mwanadamu ndiye msababishi wa magonjwa kwa kutotoa uzito wowote katika kujali kanuni za afya.

Tunawezaje Kuwa na Afya Njema

 • Kumtukuza Mungu kwa kila tufanyacho. Kwa chochote tunachokula au kunywa jambo linalopaswa kubebwa mawazoni ni kumtukuza Mungu. 1 Wakorintho 10:31
 • Kumcha Mungu. Kutoka 15:26, Kumcha Mungu humaanisha kuwa na hofu ya Mungu katika maisha yani kwa kila ufanyacho jiulize kama Mungu muumbaji wako anayejali afya yako anaruhusu tendo hilo lifanyike? Jiulize je, Yesu angekuwepo katika mazingira kama hayo, angetenda katika mwelekeo kama huo? Kumcha Mungu kunahusisha:-  Kusikiliza kwa bidii sauti ya Bwana. Mungu ndiye muumbaji wetu na mifumo ya miili yote ya miili yetu. Hivyo ni kwa njia ya kusikiliza sauti ya Muumbaji kuhusu namna ya kuitunza ndipo tunaweza kuwa na afya njema.  Kufanya yaliyoelekea mbele zetu. Mungu ametoa maelekezo ya namna bora ya kutunza afya zetu na kwa kufuata maelekezo yake tunakuwa na afya njema.  Kufata maagizo yake namna ya kuitunza miili yetu iliyo ya thamani kubwa mbele zake.  Kushika amri zake. Katika mwili wa mwanadamu kuna mambo ya kufanya na kutofanya kabisa. Mungu Muumbaji wetu ndiye mwandishi wa sharia hizi wakati akiumba mifumo ya miili yetu na kwa kuzitii tutakuwa na afya njema.
 • Kumtumikia Mungu. Kutoka 23:25
 • Kuzingatia kanuni au sheria za afya.  Kula chakula bora  Kufanya mazoezi  Matumizi bora ya maji  Mwanga wa jua  Kuwa na kiasi katika mambo yote  Kuvuta hewa safi  Kupumzika  Kumtegemea Mungu. Tutaziangalia kwa undani kanuni hizi moja baada ya nyingine kwa undani sana katika mada zinazofuata.
Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s