MATUMIZI YA VYAKULA VYA NYAMA

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya

Simu Namba: +255715678122

Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: MATUMIZI YA VYAKULA VYA NYAMA

Mpango wa awali wa chakula cha mwanadamu haukuwa ale vyakula vya nyama au vinavyotokana na wanyama mfano: nyama, maziwa, siagi, mafuta, mayai n.k Mpango wa Mungu tangu mwanzo ulikuwa mwanadamu ajishibishe kwa Nafaka. Kokwa, Matunda na Mbogamboga. Kwa muda zaidi ya miaka 2000 (Mileniamu 2) tangu uumbaji hadi baada ya gharika kinywa cha mwanadamu hakikuwahi kamwe kuonja radha ya chakula chochote kutoka kwa wanyama, samaki au ndege. Vyakula vya nyama havikuwa katika mpango wa awali wa Mungu kwa mwanadamu.

Baada ya gharika, dunia nzima iliangamizwa na hakukuwa na mche wowote wala matunda, nafaka wala mbogamboga na ndipo Mungu akaruhusu mpango wa dharula kumnusuru mwanadamu aliyemuumba kwa kumruhusu aanze kutumia vyakula vya nyama. Mwanzo 9:3, “Kila kiendacho kilicho hai 234kitakuwa chakula chenu, kama nilivyowapa mboga za majani, kadhalika nawapeni hivi vyote.”

Wakati huo ambao mwanadamu aliruhusiwa atumie vyakula vya nyama, Mungu alitoa maelekezo kwamba damu na mafuta hayapaswi kutumika. Mwanzo 9:4, Walawi 3:17, 7:23 “Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile… Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa… Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Msile mafuta yo yote, ya ng’ombe, wala ya kondoo, wala ya mbuzi.” Nyama ziliruhusiwa kutumika kwa uangalifu mkubwa kwamba damu yote na mafuta yote yawe yamekaushwa kabisa.

Wakati wana wa Israeli wametoka nchi ya Misri kuelekea katika nchi ya ahadi Kanani, Mungu aliwapatia chakula chema sana, Mana kutoka mbunguni. Kutoka 16:31-35, “Na nyumba ya Israeli wakakiita jina lake Mana; nacho kilikuwa mfano wa chembe za mtama, nyeupe; na tamu yake ilikuwa kama tamu ya maandazi membamba yaliyoandaliwa kwa asali. Musa akasema, Hili ni neno Bwana aliloliamuru, Pishi moja ya kitu hicho na kiwekwe kwa ajili ya vizazi vyenu; ili kwamba wao wapate kukiona kile chakula nilichowalisha ninyi barani, hapo nilipowaleta kutoka nchi ya Misri. Basi Musa akamwambia Haruni, Twaa kopo, ukatie pishi moja ya hiyo Mana ndani yake, uiweke mbele ya Bwana, ilindwe kwa ajili ya vizazi vyenu. Kama vile Bwana alivyomwagizia Musa ndivyo Haruni alivyoiweka hapo mbele ya Ushahidi, ili ilindwe. Na wana wa Israeli walikula Mana muda wa miaka arobaini, hata walipofikilia nchi iliyo na watu, wakala ile Mana, hata walipofikilia mipakani mwa nchi ya Kanaani.”K051

Kwa kutumia chakula hicho ambacho ni mpango wa Mungu wana wa Israeli walidumu jangwani siku zote licha ya jua kali wakati wa mchana, baridi kali wakati wa usiku, hatari zote za jangwani na vita mbalimbali walizopigama walidumu kuwa na afya njema siku zote. Kutoka 15:26, “akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya Bwana, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yo yote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi Bwana nikuponyaye.” Sisi pia kama wasafiri kuelekea katika nchi ya ahadi ya mbinguni tunapaswa kuzingatia mpango wa Mungu wa chakula chetu.

Wakati fulani wana wa Israeli walijaribiwa wakamnung’unikia Mungu kwa chakula ambacho aliwapatia wakataka nyama na samaki ili wale kinyume na mpango wa Mungu wa chakula cha Mana, chakula kutoka mbinguni. Mungu akawaacha, wafate tama zao akawaletea kware ambao waliwasababishia madhara makubwa. Hesabu 11:4-10, 18-20, 32-33. “Kisha mkutano wa wafuasi waliokuwa kati yao, wakashikwa na tamaa; wana wa Israeli nao wakalia tena, wakasema, N’nani atakayetupa nyama tule? Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hii mana tu. Na hiyo mana ilikuwa mfano wa chembe za mtama na kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake bedola… kabla ya kesho, nanyi mtakula nyama; kwa maana mmelia masikioni mwa Bwana, mkisema, Ni nani atakayetupa nyama, tule? Maana huko Misri tulikuwa na uheri. Basi kwa sababu hiyo Bwana atawapa nyama, nanyi mtakula. Hamtakula siku moja, wala siku mbili, wala siku tano, wala siku kumi, wala siku ishirini; lakini mtakula muda wa mwezi mzima, hata hapo nyama hiyo itakapotoka katika mianzi ya pua zenu, nanyi mtaikinai, kwa sababu mmemkataa Bwana aliye kati yenu, na kulia mbele zake, mkisema, Tulitoka Misri kwa maana gani?… Watu wakaondoka mchana huo wote, na usiku huo wote, na siku ya pili yote, kuwakusanya hao kware; yeye aliyepata ya upungufu kuliko wenziwe alipata kiasi cha homeri kumi; nao wakawaanika wote kando-kando ya kambi kuizunguka pande zote. Kisha hapo hiyo nyama ilipokuwa ikali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira za Bwana ziliwaka juu ya watu, Bwana akawapiga watu kwa pigo kuu mno.”

Wasafiri wenzetu wakiwa njiani kuelekea katika nchi ya ahadi walitamani kula samaki na nyama maana kama tulivyo sisi leo tunaona ya kwamba chakula ambacho ni mpango wa Mungu kwa afya zetu hakifai na hivyo kufuata chakula cha nyama kukidhi tamaa zetu na tunaishia magonjwa makubwa ya ajabu ambayo tusingeyapata ikiwa tungerejea kupendezesha meza zetu kwa nafaka, matunda na mbogamboga.

Wakati Mungu aliporuhusu mwanadamu ale vyakula vya nyama pia alitoa mwongozo wa wanyama wa kuliwa na wasio wa kuliwa. Mungu muumbaji wetu na wa wanyama, ndege, samaki na wadudu hao aliona kwa hekima yake makundi yafaayo kutumiwa na mwanadamu ya wale yasiyofaa.

Nikukumbushe tena vyakula vya nyama viliruhusiwa baada ya gharika maana nchi yote ilikuwa imeharibiwa. Lakini kabla ya gharika, Mungu alimpatia maelekezo Nuhu juu ya namba ambayo wanyama wangeingia nR099dani ya safina kwamba wanyama wote walio safi (wasio najisi) waingie saba saba mme na mke na wanyama wachafu (najisi) waingie wawili wawili mme na mke lengo likiwa kuhifadhi mbegu ya nchi. Mwanzo 7:2-4, “Katika wanyama wote WALIO SAFI ujitwalie saba saba, mume na mke; na katika wanyama WASIO SAFI wawili wawili, mume na mke.Tena katika ndege wa angani saba saba, mume na mke; ILI KUHIFADHI HAI MBEGU JUU YA USO WA NCHI YOTE.”

Mgawanyiko na ufafanuzi huu wa wanyama safi na wachafu unapatikana katika Walawi 11 na Kumbukumbu 14. Mungu anasema wazi kwamba wanyama wanaopaswa kuliwa ni wale walio safi na wachafu hawapaswi kutumiwa kwa chakula na hata wakifa mizoga yao haipaswi hata kuguswa.

Ni kosa kubwa kudhani kwamba Yesu alimruhusu mwanadamu ale wanyama, ndege, samaki na wadudu wachafu. Kamwe Yesu aliye ufunuo wa Mungu hakuruhusu wala kupingana na mpango wa chakula wa Mungu, na hakuwafundisha watu na wanafunzi wake kukiuka mpango wa Baba yake. Baadhi ya mafungu ya Biblia yanayotumika kwa kupotosha ili kuhalalisha matumizi ya nyama chafu ambayo ni:-

  • Si kila kimuingiacho mtu kinamtia unajisi bali kitokacho
  • Kilichotakaswa na Mungu wewe usikiite najisi, chinja ule.

Tafiti mbalimbali za kisayansi zimeweka wazi kwamba vyakula vya nyama kutoka kwa wanyama, ndege, samaki na wadudu wachafu vimebeba vimelea vingi sana vya magonjwa sugu na hatari. Licha ya matokeo ya tafiti hizo binadamu bado wanatumia vyakula hivyo ili kukidhi tama za miili yao. Baadhi ya tafiti kuhusu nyama ya nguruwe ni kwamba imejaa minyoo ambayo hata ukiipika kwa joto gani haifi.

Katika ulimwengu tunaoishi sasa pia, vyakula vya nyama vimekuwa chanzo cha magonjwa mengi yanayosababisha vifo vingi vya watu wazima na watoto. Na tatizo hili halipo tu katika siku zetu lakini katika siku za wazee wetu pia, maana kabla Mungu hajaruhusu watu kula nyama wanadamu waliishi miaka mingi sana hadi 900 na walikuwa na maumbile makubwa lakini leo kwa kula nyama watu tunaishi miaka michache sana kama miaka 60-80 tu! na tuna maumbile madogo.

Utamu unaopatikana katika vyakula vya nyama hutokama na damu au mafuta ya wanyama hao iliyopo katika minofu yake. Endapo nyama itapikwa kwa kuondoa damu na mafuta yote isingekuwa na radha yotote ya kuvutia walaji. Lakini Mungu ametoa mwongozo kwamba matumizi ya nyama sharti yasiwe pamoja na damu au mafuta.R097

Hivyo ni vema kurudi katika mpango wa kwanza wa chakula chetu, maana japo Mungu aliruhusu matumizi ya vyakula vya nyama baada ya gharika lakini hakuvipa vyakula vya nyama nafasi ya kwanza ya mlo wetu. Hili tunaliona wakati wa safari ya wana wa Israeli kwenda nchi ya ahadi, Mungu hakuwapa vyakula vya nyama kama nafasi ya kwanza ya mlo wao bali mana tu.

Pia kwa kuwa tunatakiwa kubadilisha tabia na mfumo wetu wa maisha kuelekea chakula ambacho Mungu ametupatia, mabadiliko hayo hayatakiwi kuchukuliwa kwa pupa. Lazima tujifunze kwanza namna ya kuandaa vizuri chakula cha nafaka, matunda na mbogamboga ili kiwe na matokeo mema mwilini mwetu.

Endelea kufatilia mada mbalimbali maana tutajifunza maandalizi ya vyakula vya kiafya. Pia tutajua kwa hakika maandalizi ya vyakula vizuri na vitamu kama mbadala wa vyakula vya nyama. Usikose!!!

Kwa maswali, maoni au ushauri juu ya mada hii au nyingine nyingi usisite kuwasiliana nasi.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

JE, SABATO ILIANZIA KWA WAYAHUDI? JE, NI YA WAYAHUDI TU?

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya

Simu Namba: +255715678122

Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable version: JE, SABATO ILIANZIA KWA WAYAHUDI? JE, NI YA WAYAHUDI TU?

Watu wengi wanajiuliza kwamba Sabato ilianzia kwa Wayahudi? Na kama ni hivyo basi sisi hatupaswi kutunza na kuishika maana niya Wayahudi. Katika hili tutaiuliza Biblia yenyewe iseme majibu, au siyo?

Biblia inatwambia Sabato ilianzishwa katika Bustani ya Edeni siku ya SABA baada ya uumbaji. Mwanzo.2:1-3, “Basi mbingu na nchi zikamalizika, na jeshi lake lote. NA SIKU YA SABA Mungu alimaliza kazi yake yote aliyoifanya; AKASTAREHE SIKU YA SABA, AKAACHA KUFANYA KAZI YAKE YOTE ALIYOIFANYA, Mungu akaibariki siku ya saba, akaitakasa kwa sababu katika siku hiyo Mungu alistarehe, AKAACHA KUFANYA KAZI yake yote aliyoiumba na kuifanya.” Hapa tunaona kuwa Sabato ya kwanza kabisa katika historia ilikuwa Tarehe 07-01-01 au mwaka 4000K.K. Katika Sabato hii, kulikuwa na WATU WAWILI TU Adamu na Hawa ambao hawakuwa wayahudi sawa? Unajua kama Adamu na Hawa wangekua wayahudi basi watu wote tungekuwa wayahudi maana hawa walikuwa wazazi wetu wa kwanza ambamo watu wote tumetokea kwao.

Ibrahimu aliishi miaka karibia 2000 kabla ya kuanzishwa kwa taifa la Uyahudi, kabla ya kipindi cha Musa cha kutoka Misri kwenda Kanani. Lakini biblia inamshuudia kuwa aliishika Sabato maana alishika amri na sheria za Mungu hata kabla hazijatolewa katika mlima Sinai kwa wana wa Israeli. Mwanzo. 26:5, inasema “Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na AMRI zangu, na hukumu zangu, na SHERIA zangu.” Hivyo Ibrahimu alishika amri za Mungu zote ikiwemo na sabato tazama Kutoka. 21:8-11, na zingatia pia Ibrahimu alishika amri zote za Mungu maana kama angevunja moja agekua hajazishika. Tazama Yakobo2:10 na Mathayo5:17-19. Pia wana wa Israeli walishika Sabato hata kabla hawajapewa amri za Mungu katika mlima Sinai hili Creation 1tunaliona katika Kutoka.16:23-27. Ndio maana wakati Mungu anatoa Amri zake kwa Israeli anasema “IKUMBUKE SIKU YA SABATO UITAKASE siku sita ufanye kazi utende mambo yako yote….” Kutoka.20:8 aliwambia waikumbuke maana walikuwa wanaijua. Katika utumwa wa Misri wana wa Israeli walikuwa wamesahau sabato ya BWANA na kama wangekua hawaijui asimgewambia waikumbuke.

Yesu alipokuja alisema Sabato ilifanyika kwajili ya watu wote, Yesu “akawaambia, sabato ilifanyika kwa ajili ya mwanadamu, si mwanadamu kwa ajili ya sabato.” Marko.2:27 Hivyo tunaona kuwa Sabato ilifanyika kwa ajili ya MWANADAMU, ndugu je wewe nawe ni mwanadamu? Kama ndiyo basi mshukuru sana Mungu maana ameumba Sabato siku ya SABA ya juma kwa ajili yako uifurahie kwa pumziko takatifu.

Baada ya Yesu kwenda mbinguni, mitume waliendelea kushika Sabato pamoja na mataifa mengine wasiokuwa Wayahudi. Katika Matendo ya Mitume.13:42,44 tunaona mkutano uliofanyika siku ya Sabato ambao mataifa walimsihi Paulo arudie hubiri lake la sabato katika Sabato inayofata: ZINGATIA ‘Kama wangekuwa wanasali Jumapili, wale watu wangesema wakutane kesho yake lakini haikuwa ivyo maana walisema wakutane Sabato ijayo. Na Sabato iliyofata walikuja mji mzimakusikiliza hubiri la Paulo’ hadi wayahudi waliokuwa wapinzani wa kazi ya Mungu wakaanza kumwonea wivu. Tazama pia Matendo.18:4, Paulo “akatoa hoja zake katika sinagogi(kanisa) KILA SABATO akajaribu kuwavuta Wayahudi na Wayunani.”

Biblia haisemi sehemu yoyote kuwa sabato ni ya wayahudi tu, hii kusema watu wengine wasio wayahudi hawatakiwi kushika Sabato ya  siku ya saba Jumamosi. Madai haya hayana ukweli maana kuvunja Sabato kunamfanya mtu awe mvunja sheria zote za Mungu kwani ukuvunja moja umevunja zote.

Karibu sana katika raha ya Sabato maana ni raha pekee kwa watu wa Mungu, Waebrania.4:9 inasema “basi imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu.”

Karibu tena, kwa maswali, maoni na ushauri usisite kuwasiliana nasi.

Je, Siku Ya Ibada Ya Mbinguni Ni Ipi?

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya
Simu Namba: +255715678122
Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: Je, Siku Ya Ibada Mbinguni Ni Ipi

Tumeona kuwa watu wengi wamekuwa wakitumia siku mbalimbali katika juma kwajili ya ibada na kupumzika katika kazi za kila siku. Ibada hizo hufanyika katika siku za Ijumaa, Jumamosi, Jumapili, Jumatano na nyingine nyingi. Lakini swali ni hili, je tutakapokwenda mbinguni ni siku gani tutakayoabudu kati ya hizi? Je, Biblia inasemaje kuhusu hili?

Isaya. 66:22,23 “Kama vile MBINGU MPYA NA NCHI MPYA, nitakazofanya, zitakavyokaa mbele zangu asema BWANA, ndivyo uzao wenu na jina lenu litakavyokaa. Na itakuwa, mwezi mpya hata mwezi mpya, na SABATO hata SABATO, WANADAMU WOTE WATAKUJA KUABUDU MBELE ZANGU ASEMA BWANA.” Mungu anasema katika Neno lake kuwa katika mbingu ambayo ameifanya kwajili ya watakatifu wake WOTE, kwamba watakuwa WANAMWABUDU katika kila siku ya SABATO yaani siku ya Jumamosi.

Ni ukweli kuwa Mungu atakuja kuchukua watakatifu wake “hao wazishikao AMRI za Mungu na imani ya Yesu”. Ufunuo.14:12 Kamwe hakuna mwenye dhambi hata mmoja atakayeingia katika ufalme wa mbinguni. Si ndiyo? Sasa biblia inatoa maana rasmi ya neno dhambi katika 1 Yohana 3:4, “Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwakuwa DHAMBI NI UASI.” Hivyo dhambi ni uasi wa sheria za Mungu, yaani waasi wote wa sheria hawataingia mbinguni.

Christ and RedeemedPia amri kumi za Mungu zapaswa kushikwa kwa ukamilifu wake zote kama zinavyoelezwa katika Kutoka. 20:3-17. Na kuvunja amri moja tu, ni sawasawa umevunja amri zote kumi. Yakobo2:10,11 inasema “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa juu ya yote. Maana yeye aliyesema, Usizini, pia alisema, Usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini umeua, umekua mvunja sheria.” Yaani ukishika amri za Mungu tisa tu, ukaacha kuishika sabato ya Jumamosi UMEKUA MVUNJA SHERIA. Na kwa wale ambao wanashika sabato tu na kuvunja zingine amekuwa mvunja sheria pia bali usalama upo katika kushika amri zote za Mungu ikiwemo sabato.

Quran nayo inasema katika suratun Nahl(16) kifungu cha 124 kuwa, “Hakika (adhabu ya kuvunja taadhima ya) Jumamosi iliwekwa juu ya wale waliohitilafiana kwa ajili ya hiyo (Jumaamosi), na kwa yakini Mola wako atahukumu baina yao siku ya kiama katika yale waliyokuwa wakihitalifiana.” Hivyo hata Quran inatoa onyo kwa wavunja sheria ya Mungu hasa wavunja Sabato ya BWANA yaani siku ya Jumamosi.

Je, wavunja Sabato ya BWANA wote watapotea hata wanaovunja Sabato wakati wanatenda miujiza? Yesu alisema “Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwajina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi? Ndipo NITAWAAMBIA DHAHIRI, SIKUWAJUA NINYI KAMWE; ONDOKENI KWANGU NINYI MTENDAO MAOVU.” Mungu anasema kwamba kuna watu watamwendea wakimsihi waingie katika ufalme wake lakini atawakataa kwa maana hata wakati wanatenda miujiza hiyo hakuwajua maana hawakutii mapenzi ya Mungu.

Lakini tumaini lipo, Yesu alisema “Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akisikia sautiyangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, name nitakula pamoja naye, nay0603135 eye pamoja name.” Ufunuo.3:20 Pia alisema kwakua “Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na SAUTI YANGU WATAISIKIA; KISHA KUTAKUWAKO KUNDI MOJA NA MCHUNGAJI MMOJA.” Yohana 10:16. Hivyo ndugu usalama utakuwa nao kama tu utaukubali wito wa Yesu leo.

Sasa kama tukienda mbinguni tutaabudu siku ya Jumamosi(SABATO). Je, kwanini tusianze kuzoea kuabudu siku hii tukiwa hapa duniani? Karibu basi katika ibada ya siku ya sabato. Tafadhali tafuta kanisa la waadventista wasabato lililokaribu nawe uanze kuwa na uzoefu huu wa ibada ya mbinguni.
Kwa maswali. Maoni au ushauri usisite kuwasiliana nasi. Bwana akubariki sana.

JE, KWANINI SABATO NI SIKU YA JUMAMOSI?

Ev. Mujaya Mujaya

Ev. Mujaya Mujaya

Na Muinjilisti: Mujaya Mujaya

Simu Namba: +255715678122

Barua Pepe: ev.mujaya@gmail.com

Downloadable Version: Je, Kwanini Siku Ya Sabato Ni Siku Ya Jumamosi

Watu mbalimbali wamekuwa wakichanganyikiwa kuhusu siku ya Sabato kuwa ni ipi katika juma lakini leo tutaacha vitabu vikuu vya imani nyingi pekee vitupatie ufumbuzi wa jambo hili. Baadhi ya watu kwa kutofahamu Sabato ya kweli katika maandiko, wamekuwa wakishika na kuheshimu siku nyingine tofauti na Sabato ya kweli na hivyo wapo katika hatari ya kupotea.

Tuanze na biblia Mungu anasema mahali fulani kuwa Sabato ni siku ya saba, Kutoka.20:8-11, “Ikumbuke SIKU YA SABATO uitakase. Siku sita fanya kazi utende mambo yako yote; lakini SIKU YA SABA NI SABATO YA BWANA, Mungu wako siku hiyo usifanye kazi yo yote, wewe, wala mwana wako, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako. Wala mnyama wako wa kufuga, wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita BWANA alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe SIKU YA SABA; kwa hiyo BWANA akaibarikia siku ya sabato akaitakasa.” Hapa tunaona kuwa siku ya SABA NI SABATO ya BWANA MUNGU, hivyo katika juma moja la siku saba, basi siku moja ni Sabato ya BWANA. Katika siku hiyo Mungu anasema usifanye kazi yako yo yote wewe, mali zako hata watu wa nyumbani kwako.

K108ALakini je, katika juma siku ya Saba ni ipi? Au kwa maana nyingine siku ya Sabato ni ipi? Biblia inatoa jibu kuwa Sabato ni SIKU YA JUMAMOSI, Mathayo.28:1,5 inasema “Hata SABATO ilipokwisha, ikipambazuka SIKU YA KWANZA ya juma, Mariamu Magdalene, na Mariamu Yule wa pili, walikwenda kulitazama kaburi. Malaika akawajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnamtafuta Yesu aliyesulibiwa. Hayupo hapa; kwani AMEFUFUKA kama alivyosema.” Kumbe Sabato yaani siku ya saba ni siku inayotangulia kabla ya siku ya kwanza ya juma. Katika biblia ya Kiswahili cha kisasa ya habari njema fungu hili linasomeka vizuri kabisa kuwa “Baada ya SABATO, karibu na mapambazuko ya SIKU ILE YA JUMAPILI, Maria Magdalene na yule Maria mwingine walikwenda kutazama lile kaburi.” Hapa biblia inaonesha kuwa siku ya Sabato ni siku moja kabla ya Jumapili, maana Sabato ikiisha Jumapili huanza. Je, siku hiyo ni ipi? Jibu ni rahisi sana nalo ni JUMAMOSI.

Hadi leo, watu wote wanajua kuwa Yesu aliteswa na kufa siku ya Ijumaa, akalala kaburini siku ya Jumamosi na Jumapili akafufuka. Siku hii ya mateso na kifo cha Yesu inaitwa IJUMAA KUU, ni siku ya IJUMAA. Kipindi kile siku hii iliitwa SIKU YA MAANDALIO YA SABATO, Luka. 23:53-54 “Akaushusha(mwili wa Yesu), akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake. Na SIKU ILE ILIKUWA SIKU YA MAANDALIO, na SABATO ikaanza kuingia.” Hivyo siku moja kabla ya Sabato inaitwa siku ya Maandalio yaani Ijumaa nayo ilikuwa siku ya kujiandaa maana siku ya Sabato hawakufanya kazi yoyote. Biblia ya Kiswahili cha kisasa ya habari njema inasema, “Siku hiyo ilikuwa IJUMAA, na maandalio ya siku ya SABATO yalikuwa yanaanza”. Kwahiyo Sabato ni siku iliyo katikati ya siku ya IJUMAA NA JUMAPILI ambayo ni Jumamosi si ndiyo?

Hata Quran nayo inashuhudia kuwa Sabato ni siku ya saba yaani Jumamosi nayo inatakiwa kutumikaJesus and the Law kwajili ya ibada, katika surat Al-Baqarah(2) kifungu cha 65 imendikwa; “Na kwa yakini mmekwisha kujua khabari za) wale walioasi miongoni mwenu katika (amri ya kuihishimu) jumamosi. Basi tukawaambia: “kuweni manyani wadhalilifu”. Hapa tunaona kuwa Quran inasema siku ya Jumamosi ni siku inayotakiwa kuheshimiwa na kutofanya hivyo ni uasi yaani ni dhambi. Pia surat Al-Aaraf(7) kifungu cha 163a inakazia kuwa “Na waulizeni habari za mji ambao ulikuwa kando ya bahari;(watu wa mji huo) walipokuwa wakivunja (sheria ya) Jumamosi (ambayo waliambiwa wasifanye kazi katika siku hiyo, wafanye ibada tu.” Hapa tunaona Quran ikiunga mkono Biblia kwamba siku ya Sabato yaani Jumamosi ni siku ya kutofanya kazi kabisa bali ni siku ya kufanya ibada tu.

Nawe msomaji wa ujumbe huu haijalishi imani yako ni ipi au itikadi yako ni ipi Biblia na Quran vinakutaka leo urudishe utukufu wa Bwana katika Sabato yake takatifu siku ya Jumamosi wala si katika siku nyingine yoyote. Nenda katika kanisa lolote Jumamosi ya juma hili, uungane na waabuduo halisi wamwabuduo Mungu katika Roho na Kweli.

Kwa maswali, maoni au ushauri, usisite kuwasiliana nasi. Ubarikiwe sana.