RAFIKI ALETAYE UTOFAUTI KATIKA MAISHA

 

Logo Template - Logo_44
Mahusiano ni msingi wa maisha ya mwanadamu. Urafiki ni nguzo muhimu sana katika mahusiano bora. Na hakuna mwanadamu asiye na Rafiki. Na urafiki unapokuwa mzuri, daima ushirikiano huwa mkubwa na hili huleta mafanikio mengi katika maisha.
Lakini sasa tunaishi katika ulimwengu ambao kwa sehemu kubwa mahusiano yameharibika na uzuri wa urafiki umepoteza Uthamani wake. Na matokeo ya kuharibika kwa mahusiano, ndiyo maana tunaona uvunjifu wa amani ndani ya jamii, huzuni, vita na mafarakano.
Moja ya changamoto zinazokabili mahusiano ya marafiki wengi leo ni Usaliti. Kulingana na tafiti iliyowahi kuripotiwa na Kituo cha Radio ya Morning Star, mwezi June 2013, iliripoti kuwa karibia 75% ya vifo vya kujitoa uhai, vinavyotokea kwenye vyuo vya vikuu barani Afrika, ulitokana na Usaliti wa Kimapenzi kwa wanafunzi hao. Hata hivyo, matokeo makubwa ya usaliti wa kimahusiano, unaonekana katika ongezeko kubwa la watoto wa mitaani. Matokeo ya usaliti wa kirafiki/kimapenzi au usaliti wowote wa kimahusiano; ni makubwa sana katika jamii yetu ya leo.
Changamoto nyingine ya mahusiano ya urafiki kwa watu wengi leo ni Kudhulumiwa. Kwa sababu ya ukaribu na urafiki miongoni mwa watu wengi leo, wamekubaliana kuungana pamoja kwa ajili ya kufanya mambo flani pamoja mfn kuanzisha biashara n.k. Lakini matokeo yake, wamaishia kudhulumiana, kugombana, kutengana na hata kuuana.
Mpendwa msomaji hebu nikwambie hili, Maisha yetu yametufundisha kuwa, tunahitaji kuwa na Rafiki wa Kweli, Mwaminifu katika Mahusiano, Anayejali Hisia zetu, Mwenye huruma, Anayetupenda kulingana na hali tuliyonayo, Rafiki atakayeleta Mtizamo chanya katika maisha, Rafiki ambaye ataamusha matumaini mapya katika maisha yetu.
Tena tunahitaji zaidi ya rafiki tuliowazoea wa ulimwengu huu. Tunahitaji mtu atakayegusa hisia zetu za mioyoni, na kutujaza Amani, Upendo na Furaha ndani ya mioyo yetu katika ulimwengu huu na katika ulimwengu ujao. Mpendwa msomaji wangu, nakuomba ufuatane nami katika mfululizo wa masomo yatakayokuwa yakimzungumzia Rafiki Anayeleta Utofauti katika maisha.

Karibu sana!

 

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s