KWANINI TUNAPATA MAGONJWA???

Yesu ni tabibu wetu

Yesu ni tabibu wetu

Mungu ametupatia zawadi ya mwili wetu ili tuweze kuutunza, kuulinda na kuwa na afya njema. Hakika hatuwezi kumtenganisha Mungu na afya njema maana yeye hutaka kila mtu afanikiwe katika afya ya kimwili kama vile afaanikiwavyo kiroho pia. Magonjwa, maradhi sugu, vifo n.k sio mpango wa Mungu. Mungu alimuumba mwanadamu katika hali njema ya kutopata lakini dhambi (anguko la mwanadamu) imepelekea watu kuugua na kupata maradhi mengi.

Mungu siyo msababishi wa magonjwa na vifo bali ni utaratibu wetu wa maisa tuliochagua kuishi ambao unatupelekea kupata magonjwa mbalimbali na Hivyo kupelekea vifo. Mfano, Mungu hasababishi magonjwa ya zinaa pamoja na ukimwi bali uchaguzi wetu wa kuishi maisha ya anasa na zinaa ndio hunasababisha kupata magonjwa hayo; pia Mungu hasababishi malaria, kipindupindu, kichocho na kifua kikuu bali ni maisha tulioyachagua kuishi na matendo tunayoyafanya kila siku hutupelekea kupata magonjwa hayo.

Ni ukweli usiopingika kuwa vifo vingi kwa sasa husababishwa na mfumo wa maisha ya mwanadamu. Ulevi wa pombe na madawa ya kulevya, uvutaji wa sigara, tumbaku, bangi na gundi kumepelekea vifo vingi kwa magonjwa ya kansa za aina mbalimbali. Kadhalika ulaji mbaya usiopangiliwa umewapelekea watu kupata magonjwa ya kansa, utapia mlo, maralia, shinikizo la damu n.k

Mungu pekee ndiyo jibu la afya njema, wala hatupaswi kutafuta afya njema mahali pengine popote mbali ya kanuni zilizotolewa na Mungu. Mungu aliyeuumba mwili bila shaka anajua hakika kinachohitajika katika mwili ili uwe na afya njema. Jambo la kuzingatia pia ni kwamba Mungu ni jibu si la afya ya mwili tu bali pia na afya ya kiroho. Dawa ya pekee ya kutibu magonjwa yetu ni kubadili kabisa mfumo wa maisha yetu yani kula kwetu, kuvaa kwetu, malazi yetu, maburudisho yetu, vinywaji vyetu, n.k na mabadiliko haya huja pale Mungu anapotawala maisha yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s