Kusoma Biblia

Na Mujaya Mujaya

+255 715 678 122

m.mujaya@yahoo.com

ev.mujaya@gmail.com

Biblia ni kitabu cha maana sana katika maisha yetu, kukisoma inapaswa kuwa jambo la msingi. Ni heri kusoma, kusikia na kuyashika maandiko matakatifu. Biblia inasema,  “Heri asomaye na wao wayasikiao maneno ya unabii huu, na kuyashika yaliyoandikwa humo;..”. Ufunuo.1:3 SUV

Katika ulimwengu uliojaa mafundisho ya uongo, na mashauri au maoni potofu ya watu kuhusu maandiko matakatifu ni busara kudumisha biblia kama kipimo pekee cha kiwango cha maisha na ujumbe wa Mungu kwajili yetu.  “Mungu anataka watu wadumishe Biblia na Biblia pekee, kama kipimo cha mafundisho yote na msingi wa matengenezo yote.” (Tumaini Kuu, 359:5) Matengenezo yote yapasa yatoe msingi wake katika neno la Mungu maana ni msingi wa imani ya kweli maana “…imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo” Warumi.10:17 SUV.

Kujifunza maandiko kunapaswa kufanyike kwa maombi ya kina na moyo wazi kwajili ya Roho Mtakatifu kuujaza kwa maneno ya uzima. Kwa kusoma maandiko bila maombi na akili ya kujifunza hatutaelewana nayo maana, “Wakati ambapo kujifunza Maandiko kutafanywa bila roho ya maombi na inayokubali kufundishwa fungu lililo wazi kabisa litapotoshwa kutoka kwenye maana yake ya kweli.” (Tumaini Kuu, 321:1)

Ni makusudi ya shetani kwamba Neno la Mungu lisiwe na mvuto au kuwafikia watu ambao amekusudia kuwashika katika madanganyo yake, “(shetani) Anapomwona mjumbe wa Mungu akichunguza Maandiko, huliwekea alama somo litakalotolewa. Kisha hutumia ujanja na werevu wake ili kwamba ujumbe usiwafikie wale ambao anawadanganya kuhusiana na somo lile.” (Tumaini Kuu, 319:3) Hivyo shetani atafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba anatoa usikivu wako kwa maandiko matakatifu ikiwa usomaji wa neno hautaambatana na maombi ya kina. Wakati wa kusoma maandiko shetani huwapa watu shughuli nyingi na sababu mbalimbali ambazo watu huziona kama sababu za msingi za kutosoma maandiko.  “Yule ambaye atalihitaji sana lile onyo atasukumwa kuwa na jambo fulani la kufanya ama kwa njia yoyote nyingine atazuiwa kusikiliza neno”. (Ibid)

Lengo kubwa la shetani ni kuhakikisha kwamba tunashindwa kwa mashambulizi yake kwa kutoa usikivu wetu kwa maneno matakatifu. “Shetani anajua kwamba wale wote wanaopuuzia maombi na Maandiko watashindwa kwa mashambulizi yake. Kwa hiyo anabuni kila mbinu iwezekanayo kuishughulisha akili” (Tumaini Kuu, 319:5)

Kwa kadiri tunavyoelekea mwisho wa wakati, muda mwingi ungetengwa katika kuyatafakari maandiko matakatifu. Maandiko yanayosomwa wakati huu wa amani ni akiba kwa ajili ya nyakati za tabu na kukatishwa tama katika siku za usoni. “Ili kuvumilia majaribu, ni lazima wayaelewe mapenzi ya Mungu kama yalivyofunuliwa katika neno lake. Ni wale tu watakao kuwa wamezijenga akili zao kwa kweli za Biblia ndio watakaosimama katika pambano kuu la mwisho.” (Tumaini Kuu, 359:2)

Dondoo mhimu za kusoma maandiko

Fuata mwongozo wa kujifunza maandiko kwa mwaka mzima.

Ili kusoma maandiko kwa mpangilio na uwiano sawa unaweza kutumia mpango wa usomaji wa biblia wa mwaka mzima, mwongozo unaoweza kuupata katika tovuti, http://www.bibleyear.com. Kisha jiwekee utaratibu mzuri wa kukamilisha sura ulizopangiwa kwa siku katika mwongozo huo.

Anza kwa kusoma sura fupi fupi.

Kusoma Biblia kunahitaji nidhamu, utaratibu na mpangilio. Wengi wamekuwa wakichoka kusoma maandiko kwa kuona kwamba sura za biblia ni ndefu sana hivyo kuwashindwa kuzimaliza. Katika jambo hili ni vema kama mtu ataweka utaratibu mzuri wa kusoma biblia akianza na vitabu vifupi vifupi.

Mfano, Ndugu X alihitaji kusoma biblia yake kutoka kitabu cha mwanzo hadi ufunuo. Aliandika orodha ya vitabu vyote 66 katika karatasi lake kwa kuzingatia urefu wa kitabu. Vitabu vifupi vifupi vilianza juu wakati vile virefu aliviweka mwisho. Alianza kusoma biblia yake kwa kusoma vitabu vifupi na kila kitabu alichokimaliza alikiwekea tiki (√) katika orodha yake kwenye karatasi aliloliandaa. Aliendelea hivyo mpaka alipomaliza vitabu vyote vifupi na kuanza virefu mpaka alipomaliza zoezi lake ya usomaji.

Fuatilia vitabu vya maandiko kwa kuzingatia historia na namna vilivyoandikwa.

Watu wengi ambao wameanza kusoma maandiko kwa mwaka mzima au kwa kipindi fulani cha wakati wamejikuta wakiishia njiani kwa sababu ya kutoelewa mtiririko wa kimawazo wa baadhi ya sura za biblia na hivyo kufanya zoezi la usomaji lionekane linalochosha au lisilowezekana. Mbinu ya kusoma kwa kuzingatia historia imeleta unafuu kwa baadhi ya watu na kukuta uelewa wao wa maandiko unakuwa na wanafurahia zoezi la kusoma biblia nzima.

Mfano, soma agano jipya ukianzia kitabu cha  Luka, kisha Mathayo na Marko uku ukimaliza mlolongo wa injili kwa kitabu cha Yohana. Kitabu cha Luka kinavutia sana kutokana na historia yake, yani maneno ya Daktari Luka akimsimulia Theofilo.

Kabla ya kusoma nyaraka za Paulo kwanza soma kitabu cha matendo ya mitume hasa sura ya 15 maana ni katika sura hiyo kazi na utume wa Paulo kwa mataifa umeweka msingi wake na mambo aliyokuwa anayafundisha na kuyakemea katika nyaraka zake kwa makanisa mbalimbali.

Kuwa na rafiki wa kusoma naye maandiko.

Rafiki wa karibu wa kusoma naye maandiko ni njia nyingine ya kumsaidia mtu kusoma maandiko na kuimaliza biblia. Tafuta rafiki ambaye mtasaidiana kwa pamoja kukamilisha zoezi la usomaji wa Biblia.

Mfano, Dada T na R ni marafiki wa karibu sana. Baada ya kupata wito wa kusoma maandiko waliamua kusaidiana kusoma biblia kwa pamoja. Ili kufikia lengo lao waliamua kuweka baadhi ya siku katika juma kujadili masomo waliyojifunza katika biblia, kukumbushana wakati wa kusoma, kuombeana, kutembeleana kwajili ya kusoma maandiko. Wakati mwingine walilazimika kubadilishana biblia zao kwa miadi kwamba wasingerudishiana mpaka wamefikia sura fulani jambo ambalo liliwapa motisha ya kusoma zaidi. Kusoma pamoja kuliwawezesha kuimaliza biblia maana walitiana moyo, walijadili mambo magumu waliyokutana nayo katika usomaji wakaombeana wapate ufunuo wa Roho mtakatifu kwa mambo ambayo hawakuyaelewa.

Kuwa na wakati na mahali pa kusomea Biblia yako.

Muda na mahali pa kusomea neno ni jambo la msingi sana. Wakati ufaao wa kusoma maandiko ni alfajiri unapoamka kabla haujafanya kazi yoyote au usiku wa manane ikiwa utaamka kwa maombi. Katika siku wakati wa kusoma maandiko unapaswa kuwa wa kwanza kabla akili haijachafuliwa kwa tabu, misukosuko na masumbufu ya maisha haya.

Chagua mahali pa kusomea maandiko na nenda ukasome kwa wakati uliouchagua na Bwana atakubariki.

 

 

VITENDEA KAZI

Biblia

Kamusi

Husaidia kupata maneno magumu ambayo hatuyaelewi.

Itifaki

Hutupatia maelezo ya ziada kuhusu maneno ambayo yamevuta usikivu wetu na hivyo kutuwezesha kuyasoma tena mahali yalipoandikwa tena katika maandiko.

Mtandao

Wanafunzi wa maandiko

Programu za tarakilishi

 

Advertisements

ShareHope Ministry is the independent ministry which aims to proclaim the three angels message of Revelation 14 in the theme of Seventhday Adventist Church. The programs are designed include all people without regarding social, political, econimical and geographical boundaries.

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s