KWANINI TUNAPATA MAGONJWA???

Yesu ni tabibu wetu

Yesu ni tabibu wetu

Mungu ametupatia zawadi ya mwili wetu ili tuweze kuutunza, kuulinda na kuwa na afya njema. Hakika hatuwezi kumtenganisha Mungu na afya njema maana yeye hutaka kila mtu afanikiwe katika afya ya kimwili kama vile afaanikiwavyo kiroho pia. Magonjwa, maradhi sugu, vifo n.k sio mpango wa Mungu. Mungu alimuumba mwanadamu katika hali njema ya kutopata lakini dhambi (anguko la mwanadamu) imepelekea watu kuugua na kupata maradhi mengi.

Mungu siyo msababishi wa magonjwa na vifo bali ni utaratibu wetu wa maisa tuliochagua kuishi ambao unatupelekea kupata magonjwa mbalimbali na Hivyo kupelekea vifo. Mfano, Mungu hasababishi magonjwa ya zinaa pamoja na ukimwi bali uchaguzi wetu wa kuishi maisha ya anasa na zinaa ndio hunasababisha kupata magonjwa hayo; pia Mungu hasababishi malaria, kipindupindu, kichocho na kifua kikuu bali ni maisha tulioyachagua kuishi na matendo tunayoyafanya kila siku hutupelekea kupata magonjwa hayo.

Ni ukweli usiopingika kuwa vifo vingi kwa sasa husababishwa na mfumo wa maisha ya mwanadamu. Ulevi wa pombe na madawa ya kulevya, uvutaji wa sigara, tumbaku, bangi na gundi kumepelekea vifo vingi kwa magonjwa ya kansa za aina mbalimbali. Kadhalika ulaji mbaya usiopangiliwa umewapelekea watu kupata magonjwa ya kansa, utapia mlo, maralia, shinikizo la damu n.k

Mungu pekee ndiyo jibu la afya njema, wala hatupaswi kutafuta afya njema mahali pengine popote mbali ya kanuni zilizotolewa na Mungu. Mungu aliyeuumba mwili bila shaka anajua hakika kinachohitajika katika mwili ili uwe na afya njema. Jambo la kuzingatia pia ni kwamba Mungu ni jibu si la afya ya mwili tu bali pia na afya ya kiroho. Dawa ya pekee ya kutibu magonjwa yetu ni kubadili kabisa mfumo wa maisha yetu yani kula kwetu, kuvaa kwetu, malazi yetu, maburudisho yetu, vinywaji vyetu, n.k na mabadiliko haya huja pale Mungu anapotawala maisha yetu kwa njia ya Roho Mtakatifu.

Advertisements
By ShareHope Ministries Posted in Health

Hitimisho la juma la uamsho kundi la SDA Peko Misegese lafana

IMG_20140712_120450

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akitoa somo katika huduma kuu ya kuhitimisha juma la uamsho katika kundi la Peko Misegese SDA

IMG_20140712_120633

Washiriki wa Peko Misegese SDA Church wakati wakisikiliza somo la kuhitimisha juma la uamsho kundini hapo

IMG_20140712_131334

Baadhi ya watoto waliohudhuria ibada ya kuhitimisha juma la uamsho

IMG_20140712_120715

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akitoa somo la mwisho wakati wa huduma kuu. Somo lililokuwa na maudhui ya “Kazi ya Roho Mtakatifu katika Kanisa Lake”

IMG_20140712_134122

Baadhi ya washiriki wa kundi la Peko Misegese SDA Church katika picha ya pamoja. Kulia mwisho aliyeketi ni mkuu wa kundi Ndg. Laurent Faustine, nyuma yake ni Muinjilisti mlei Ndg. Suleiman Ally

C360_2014-07-12-13-51-13-239

Muinjilisti Mujaya Mujaya katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa kundi la Peko Misegese SDA Church mara baada ya ibada ya kuhitimisha juma la uamsho

IMG_20140712_160631

Mkuu wa kundi la Peko Misegese SDA Church akimtukuza Mungu kwa wimbo

IMG_20140710_180827

Muinjilisti Mujaya Mujaya akitoa somo la unabii wa matukio ya siku za mwisho katika kundi la Peko Misegese SDA Church wakati akiendesha juma la uamsho

By ShareHope Ministries Posted in News

Mashindano ya masomo Shule ya msingi Misegese yachochea uhusiano wa wanafunzi na kanisa

IMG_20140710_120336

Wanafunzi wakisikiliza maelekezo kuhusu masomo yatakayohusika na sheria za mchezo

IMG_20140710_120528

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akitoa maelekezo ya masomo, kanuni na sheria zitakazotumika katika shindano

IMG_20140710_120308

Timu ya Venus kutoka darasa la saba ikisikiliza swali lao

IMG_20140710_122357

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akitoa maswali kwa timu moja shindani toka darasa la saba

IMG_20140710_124443

Baadhi ya washindani wakipekua majibu katika kitabu wakati shindano likiendelea ili kujiimarisha zaidi kwajili ya zamu yao

IMG_20140710_125335

Majaji wa shindano wakisikiliza kwa making maswali na majibu kwa kila timu. Kulia ni Mary Musa na kushoto ni Lilian Suleiman

IMG_20140710_131611

Timu ya Mikumi kutoka darasa la sita wakijadili swali lao kabla ya kutoa jibu. Timu hii ilishika nafasi ya pili

IMG_20140710_134103

Wanafunzi wa madarasa mengine walilazimika kuchungulia mlangoni ili washuhudie timu itakayoibuka kidedea

IMG_20140710_134135

Wanafunzi wengine walidandia madirishani ili wasipitwe na tukio hill muhimu

IMG_20140710_132314

Umakini ulitawala katika shindano zima

IMG_20140710_140419

Mwalimu Elias kutoka S/M Misegese akitoa zawadi kwa mshindi mmojawapo anaejulikana kama Zitta Abdala

IMG_20140710_135503

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akitoa swali kwa timu ya Mikumi katika fainali ambapo timu hiyo iliibuka na nafasi ya pili

IMG_20140710_140756

Washindi kutoka timu mbalimbali wakionesha zawadi zao baada ya kukabidhiwa

IMG_20140710_140901

Timu zilizoshinda toka darasa la saba katika picha na majaji na mwl. Elias aliyemwakilisha mkuu wa shule ya Misegese

IMG_20140710_143128

Baadhi ya wanafunzi waliojipanga foleni kujaribu kujibu swali la chemsha bongo

IMG_20140710_141005

Mwinjilisti akiwa majaji na mwalimu Elias aliyemwakilisha mkuu wa shule ya msingi Misegese

IMG_20140710_141055

Mwinjilisti mlei wa Peko Misegese SDA ndg. Suleiman Ally akionesha zawadi kwa washindani

IMG_20140710_141531

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akitoa zawadi kwa washindi wa maswali ya chemsha bongo papo kwa papo

By ShareHope Ministries Posted in News

Darasa la sita na saba kutoka Shule ya msingi Misegese yaingia katika ushindani wa masomo wakati Mwinjilisti Mujaya Mujaya akitembelea shule hiyo ili kukuza uhusiano wa kanisa na jamii

IMG_20140708_122636

Wanafunzi wa darasa la sita na saba wakisikiliza maelekezo ya mashindano ya kimasomo yatakavyoendeshwa

IMG_20140708_122934

Mwalimu Elias kutoka S/M Misegese akisaidiana na Mwinjilisti Mujaya Mujaya katika upangaji wa timu huru za mashindano

IMG_20140708_123435

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akiendelea na zoezi la uundaji wa timu za ushindani wa masomo S/M Misegese

IMG_20140708_124303

Mwinjilisti Mujaya Mujaya akiandikisha timu za mashindano baada ya kuundwa

IMG_20140708_123412

Wanafunzi wanaounda jumla ya timu nane zitakazochuana kumpata mshindi mmoja

IMG_20140708_122720

Wanafunzi wa darasa la sita na saba wakisikiza kwa makini maelekezo kuhusu ushiriki wa mashindano na jinsi yatakavyoendeshwa

IMG_20140708_123344

Baadhi ya timu kutoka darasa la saba

IMG_20140708_123535

Baadhi ya timu shiriki kutoka darasa la sita

By ShareHope Ministries Posted in News